UPINZANI 2020: Njia za Kwenda Magogoni na Bungeni Zimeota MBIGIRI

Ndugu zangu wa upinzani, hivi tumefikaje hapa?

Upinzani mahiri uliotikisa chama tawala kabla ya 2015 sasa umesambaratika kiasi hiki cha kurundikwa kundi moja na wakina ACACIA na wahujumu uchumi?

Mliteleza wapi maswahiba wangu?

Najua kuna watu ndani ya upinzani wenye uelewa wa kindani sana kuliko mimi kuhusu mikakati ya kisiasa. Hivyo basi sitathubutu kuwaelekeza cha kufanya ili kuliokoa hili basi la upinzani lisiingie mtaroni.

Ninachoweza kusema tu ni kuwa muwe wakweli kuhusu uchaguzi wa 2020.

Nawasihi msipoteze rasilmali zenu nyingi kwenye kiti cha uraisi. Njia ya kwenda Magogoni imeota mbigiri ndugu zangu. Cut your losses please.

Nafikiri pia muangalie ni viti gani vya ubunge vinapaswa kupiganiwa kwa nguvu zote - hapa sina uhakika. Madiwani wapiganiwe kwa nguvu zote na pengine resources nyingi zinaweza kuelekezwa huko.

Kwa sasa tafuteni mikakati mbadala (counter narratives) ya kuwaletea wananchi maendeleo na sio kufuata chambo cha kupinga maamuzi yote ya raisi Magufuli.

Labda hiki hamtakifurahia lakini Raisi Magufuli is for real. He is not fake and is resolute in his governance. Watanzania wamekiona hiki na kwa kupinga wholesale ni kuwapinga Watanzania. Don't do it.

La mwisho.
Kuna vijana wenu mumewaweka huku mtandaoni kujibu mapigo. Wengi wa hawa ni marika ya wajukuu au watoto wetu. Huwezi kuamini mitusi tunayozabwa nayo. I guess hii ndio price ya kushiriki kwenye anonymous social media kama JF. Mimi binafsi, hayaniumizi hata kidogo. Tatizo ni kuwa sijui wengine wanalichukuliaje.

This is neither here nor there. Nitaliacha kama lilivyo.

Mimi sina chama. Chukueni kinachowafaa, tupeni yaliyobaki.

Wa-khatab-a-hu
Kifyatu.
Umezoezwa kuabudu watu
 
Kwa lipi hawa,au hili la mchanga ndio unadhani kuwa litampeleka huyo Magu Magogoni tena,waliokuwa wakidai mikataba ipelekwe bungeni ni huyu Magu au hao wapinzani kuwa na akili wewe.
 
Infact Leo huwez sikia Mada yoyote ya kukosoa Maana think tank wao hajakosoa
Kwny twitter yake kaunga mkono
Ila kesho kukicha akishaambiwa na Mbowe kuwa tumepoteza credit kwa kuunga hoja Za JPM ndipo atabadilika na kuanzia hapo atapost vitu vya ajabu.. IT IS THEN UTAWAONA watakavyojitokeza kuunga mkono kwa mkurupuko kwa kila upuuzi na kutuko atakachokisema think tank wao.. So far akil kwa sasa ziko stagnant Maana hajazifungua mwenye ufunguo
Unachekesha hivi unajua anaengoza nchi hii ni nani wewe fisi,hapo Magu na mafisi wanangojea Lissu aongee waanze kuweweseka yaani tukio la nchi lkn mafisi yanakalia eti Lissu amekomolewa,sasa sijui Lissu ndo aliesaini hiyo mikataba fisi ni fisi tu.
 
Uchaguzi ulikuwa wa 2020 magufuli atapita bila ubishi. Ila mimi nahisi ni kwamba wapinzani hawataki tu kuadmit jamaa ni JEMBE. Najua deep inside mioyo yao inasema huyu ndie raisi bwana. Ila kwa vile job description yao ni UPINZANI so wanaendelea kupinga tu.
 
Hivi kwenye ile list ya watu waliolisababishia hasara kubwa taifa letu kuna mpinzani!! ?? Yaani mtu unakuja hapa unapost utumbo tu!!!! Urghhhhhhh!!!!!
Pengine hamna mpinzani. Lakini anaerekebisha mambo sasa kwani ni mpinzani wa CCM?
 
Tunahitaji bunge lenye walau 50-50, hatutaki bunge la wale jamaa wapiga makofi na wazee wa ndio kila mara. Huko mbelez mabunge mengi yapo balanced, bunge letu lina waliokunywa maji ya kijani...
Unajua, kama si ule uamuzi wa 2015, saa hii pengine upinzani ungekuwa umeshika dola.

Bado uwezekano wa kuongeza wabunge wa upinzani upo lakini mikakati lazima ibadilike.
 
Kazi kweli kweli...yaani watu wanakosa madawa shuleni huku wengine wanalaumu wapinzani kwa suala la maknikia. Ombeni tu wasifukuzwe Bungeni na hizo sheria zirudi bungeni ndo mtajua kua wapinzni ni nani hapa Tanzania.

Yaani unategemea kua kibajaji akajenge hoja na atunge sheria ya kuzuia ACACIA kutuibia! au Maji marefu au Mhagama akatunge sentensi ata moja ya kiingereza kinachoweza kuwafikirisha wazungu?

Yaani unategemea AG Masanju yule aliekua anaambiwa na Anna Makinda " AG sasa tusaidie hapo tuandikaje yeye anajibu kua wenda MTU mwingine atunge hilo sentensi kwa haraka maana mimi siyo mzuri sana kwenye hilo" zirudisheni huko Bungeni huku mmeshampa spika kazi ya kufanya dhidi ya watu wengine kama mtaleta faida kwa nchi hii.
 
[HASHTAG]#RipotiYaKwanza[/HASHTAG]

Lissu: Tusihangaike na udongo, tuhangaike na mikataba na sheria mbovu za madini zilizotufikisha hapa. Tuangalie tulipojikwaa, tusiangalie tulipoangukia.

CCM: Lissu analinda wezi. Mikataba na sheria za madini hazina shida. Shida ipo kwenye udongo wenye makinikia. Tumeibiwa sana kwenye udongo. Hatukubali.

[HASHTAG]#RipotiYaPili[/HASHTAG]

JPM: Tumelogwa na nani? Watanzania tumeibiwa sana. Naagiza mikataba yote na sheria zote za madini zipitiwe upya.

CCM: Rais wetu mzalendo. Amefanya kazi kubwa sana. Tumuombee.!!

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Lugha ileile aliyoongea Lissu akaambiwa amehongwa, ndiyo aliyoongea JPM leo akaitwa mzalendo. Akili za CCM kama kifurushi cha jaza ujazwe .!!!! C & P
Umesahau kimoja:

Lissu
Msizuie mchanga. Hii ni mali yao. Watawapeleka kwenye mahakama za wazungu za kimataifa. Mtashughulikiwa kweli kweli. Mtakiona cha mtema kuni.

Huyu ni mwana sheria. Hivi hakujua kuwa kwa kuwakamata ACACIA kwa kosa la udanganyifu (ambao ni kosa la jinai - wizi) basi itatufungulia lango la kurekebisha kila kitu kuhusu mambo ya madini?

Hapo zamani tulisema Magufuli amecheza kama Pele. Ame-fake kushoto, ACACIA akaruka na goli likaingia kulia.

Nilimtegemea Lissu aipe serikali mkakati kama huu badala ya yeye kupinga tu na kuitisha serikali.

Anyway, all-is-water-under-the-bridge. Yamepita haya. Namshauri Lissu aisaidie serikali wakati akiwa bungeni ili tupate sheria na mikataba ya madini yenye tija kwa Watanzania wote.
 
Zungusheni madish yakae sawa
Magu kawasaidia wapinzani wakawaeleze waliowabeza wakitoka bungeni wakati wa uoitishwaji wa sheria za wizi huku anayejiita mpambanaji sasa akiwa mmoja wa wapitishaji.

Nampongeza kwa kuminye domokrasia angejuta kuchukuwa fomu na kugombea na hata urais angeyamani auache
Anayaishi na kutumia maneno ya wapinzani mazuzu mnaona kuna anachofanya
Anamtaja Karamagi kwani hakuwepo bungeni wakati Zitto anamtaja na kufukuzwa ?
Anakubali mapendekezo kuzipitia sheria hakuwepo wapinzani waliokuwa wanazilalamikia ?
Sijui nani kawaroga in maguz voice
Sijui kama nimekuelewa. Hivi unasema Magufuli asiinyooshe hii nchi kwa sababu walioipindisha ni tawala za CCM zilizopita?
 
We ni Kifyatu kwelikweli. Hivi inawezekanaje mtu mzima ukaanza kuwaza mambo ya 2020 kwa mazamo wa kitoto hivyo!?. Kuna mambo mangapi hapa kati mpaka kufika huko unakokusema!? Ndio kusema hujui kwamba mtu anaweza kujenga heshima yake kwa muda mrefu sana Ila akaja iharibu kwa sekunde!? Kama huna chama kaa kimya,kila chama kina utaratibu wa kupeana ushauri.
Mimi ni Mtanzania.

Wanachofanya serikalini, bungeni, na mahakamani yananihusu moja kwa moja. Serikali itajibweteza pasipokuwa na upinzani kabambe.

Kwa hiyo nina interest na serikali inayofanya mazuri, kama serikali ya Magufuli, lakini pia nina shauku ya kuimarisha upinzani kwa sababu sio kila raisi atakuwa kama Magufuli.
 
Kwa msaada wa polisi Magu atabaki lakini kidemokrasia hana cha kumbakisha
Hizi kiki za kitoto ni kwa ninyi uzao wa wale walioamini maji yanayeshusha risasi enzi za Kinjeketile Ngwale
Ni ninyi ninyi Mafisiemu
Hii nitaichukulia kama mzaha. Lakini kama hutanii basi haya. Kusanyeni hela za kampeni ya uraisi. Kila la kheri.
 
Kwa lipi hawa,au hili la mchanga ndio unadhani kuwa litampeleka huyo Magu Magogoni tena,waliokuwa wakidai mikataba ipelekwe bungeni ni huyu Magu au hao wapinzani kuwa na akili wewe.
Tunaweza kusema yoyote yale yanayotufurahisha. Mimi nimetoa rai kwa upinzani kuwa wajipime kuhusu nafasi ya uraisi ifikapo 2020.

Inawezekana nimekosea. I hope you are right.
 
SIJUI NI NANI ALIYETUROGA WATANZANIA . YAANI HOJA IKITOKA UPINZANI HATA KAMA NI YA MAANA KWA TAIFA, HAINA MAANA KWA CCM. HII INAPELEKEA PIA HATA HOJA YA MAANA IKITOKA CCM INAONEKANA PIA HAINA MAANA KWA WAPINZANI. TAIFA LINAANGAMIA TUNAPINGANA WENYEWE KWA WENYEWE . KWANINI TUNABAGUANA KWA HOJA ZA KITAIFA?? KWANI MMOJA AKISHUKA NA KUKUBALI HOJA YA MWENZAKE KWA AJILI YA MASLAHI YA TAIFA, ATAONEKANA MJINGA?

BORA KUWA MJINGA HUKU UNAPATA UNACHOTAKA KULIKO KUWA MJANJA HUKU UNAPOTEZA.

MUNGU TUHURUMIE, WAPE HEKIMA YA KUONGOZA NA KUONGEA VIONGOZI WETU, WAWE NA AKIBA YA MANENO. WAEPUKE MANENO YA KUTUTENGANISHA, BALI WATUUNGANISHE
 
Mimi ni Mtanzania.

Wanachofanya serikalini, bungeni, na mahakamani yananihusu moja kwa moja. Serikali itajibweteza pasipokuwa na upinzani kabambe.

Kwa hiyo nina interest na serikali inayofanya mazuri, kama serikali ya Magufuli, lakini pia nina shauku ya kuimarisha upinzani kwa sababu sio kila raisi atakuwa kama Magufuli.
Hujajibu nilichokuuliza,rudi tena ukasome ndio urudi!!
 
Back
Top Bottom