mkuu kwanini upate shida na wataalamu wapo? nenda halmashauri ya jiji la tanga ,ulizia zilipo office za idara ya ardhi, waambie wakuonyeshe afisa ardhi wa jiji husika(ningekutajia hata jina na no. ya simu but noma), atakupokea kwa bashasha, kaa nae kitako mweleze eneo unalotaka kununua/kujenga,uliza kama lina master plan na general planning scheme tayari ama la, uliza matumizi yaliyoainishwa kwenye plan kama ipo tayari,kama haipo atakupa ushauri nini cha kufanya, acha kuzunguka humu wakati watendaji uko nao jirani . usifanye decision yoyote kabla ya kumwona afisa ardhi.ushauri na taarifa zote hizo ni bure wala usihofu kutolewa upepo, ukijisikia kumpa ya chai poa, usipompa pia sio kesi, hawana njaa hao kwani wanafwa na matajiri wa nchi hii!