Upimaji wa ardhi shirikishi Mwanza

Upimaji wa ardhi shirikishi Mwanza

Nsubhi

Senior Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
159
Reaction score
51
Ndugu waziri wa ardhi(LUKUVI), kumekuwa na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa baadhi ya mitaa ya jiji la Mwanza.
Unalo tamko ambalo ulitamka kuhusiana na kurasmisha maeneo yote ambayo siyo rasmi(maeneo ambayo tayari watu walishajenga na wanaishi lakini hayajapimwa), kumekuwa na danadana zinaendelea hasa kwenye eneo la mtaa wa MWALUKILA, kata ya LWANHIMA Wilaya ya NYAMAGANA, kila wana mtaa wanapoomba kupimiwa maeneo yao wanaambiwa eneo hilo lina mgogoro mara eneo hilo kuna makaburi mara eneo hilo lipimwe kulingana na mchoro wa jiji. Sisi wanamtaa tunashindwa kuelewa kiini hasa kiko wapi?

Mh. Waziri ninayo maswali ya kuuliza
1. Mtaa wa mwalukila ni sehemu ya tanzania au ni nje wa Tanzania. Na kama ni sehemu ya Tanzania kwanini waandamizi wako hawafuati maelekezo yako?

2. Kama eneo hili linahitajika kwa ajiri ya shughuli za serikali kwanini haitotewi barua ya zuio la watu kujenga na tadhimini ifanyike ili watu watambue hasa nini kinachoendelea?

3. Kwanini mkurugenzi na timu yake wanataka eneo hili lipimwe kulingana na mchoro wa jiji ikiwa maeneo mengine ya jiji hili la mwanza yanapimwa kwa upimaji shirikishi?

4. Hivi kweli waandamizi wako wanayo dhamira ya kweli ya kuisaidia serikali ya Magufuli kukusana mapato yake yenyewe na kuacha utegemezi kwa nchi wahisani?

Ndugu waziri migogoro mingi ya ardhi katika nchi hii, inasababishwa na viongozi wa serikali na watendaji wa ardhi wasio waaminifu.

Inaaminika sasa katika vichwa vya wanamtaa wengi kuwa maeneo haya kuna viongozi wa serikali wanayataka kwa faida zao binafsi baada ya kuona eneo hili ni potential.

Waziri nimeandika uzi huu ili kukujuza kwamba kuna sehemu katika jiji la Mwanza haziendi sawa katika sehemu ya ardhi. Hivyo nakuomba ufanye hima kuwashitua watendaji wako wa chini wasiwe wabinafsi na watende haki kulingana na maagizo yako.
Maana sasa katika nchi hii tunaanza kuona double standard za waziwazi zikifanywa na watendaji wa chini.
Ndugu Lukuvi watu wanakuamini lakini pia wanaani serikali katika wizara hii lakini unataka kupakwa matope na watu wa chini yako.

Ahsante Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom