Upigaji wa kura nchini Uganda hivi karibuni; hii ndio dawa ya uchakachuaji?

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,507
2,000
uganda1.jpg
Masanduku ya kura kwenye uwanja wa wazi!

uganda2.jpg

Kuhesabu kura kwa uwazi!

uganda3.jpg
Kutangaza matokeo hap hapo kwa uwazi!

Ndivyo ilivyotokea Uganda na kama ilivyotegemewa chama tawala ililala.


 

JAKOBO

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
934
0
Tanzania na Zimbabwe ndizo nchi pekee zilizobaki hapa duniani zenye binadamu wa kale tena wenye IQ ndogo,miongoni Mwao ndio wale wakisikia Kinana amejamba wanampa pole eti ameumia!
 

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Ndiyo ilivyokuwa hata 2011 General Election ambapo Yoweri Kaguta Museveni na chama chake tawala cha National Resistance Movement party (NRM) walipata ushindi.

Point ninayotaka kusema, hiyo siyo dawa ya kuzuia uchakachuaji wa kura, ila inaweza kusaidia kwa kiwango fulani.

Siri ya ushindi wa Brenda Nabukenya ni vyama vikubwa vya upinzani viliunganisha nguvu na kumuweka huyu mwana dada kwa vile alishinda hata uchaguzi wa kwanza na mahakama ikaamua urudiwe tena.

Kitu kingine kilichosaidia ni kwa baadhi ya viongozi mashuhuri kutoka chama cha Yoweri Museveni kama aliyekuwa Makamu wa Rais, Prof. Gilbert Bukenya kupiga kampeni za kutaka achaguliwe huyu mwanadada, Brenda Nabukenya. Ushindi wa kwanza kulikuwa na tofauti ya kura 30 lakini uchaguzi wa sasa baada ya kupata msaada wa political heavyweight, tofauti ya kura imeongezeka na 16,000,

Mimi huwa ninashangazwa na baadhi yetu Watanzania tunapoanza kutoa mifano ya kisiasa ya nchi mbali mbali za Afrika na kuanza kujilinganisha nazo.

Nchi za East Afrika ziko tofauti sana kwenye mambo ya siasa achilia mbali kulinganisha na nchi zote za Africa. Siasa za Kenya huwezi kulinganisha na siasa za Tanzania. Vivyo hivyo kwa siasa za Uganda, Rwanda, Burundi na Congo

Nchi za Kiafrika zinaweza zikawa zinashabihiana sana kwenye maswala ya kijamii, lakini linapokuja swala la kisiasa, zinakuwa na tofauti sana.
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Tanzania na Zimbabwe ndizo nchi pekee zilizobaki hapa duniani zenye binadamu wa kale tena wenye IQ ndogo,miongoni Mwao ndio wale wakisikia Kinana amejamba wanampa pole eti ameumia!
teh teh, mkuu mbavu zangu mie...
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Duh, kwa Tanzania ilipaswa kuwe hivo, nadhani watoa rushwa kwenye uchaguzi wangeumia sana...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom