Upepo wa Membe mtaani usipime

Mkuu muulize tu tangu JPM aingie madarakani ni mradi upi aliouanzisha yeye na umekamilika akafanikiwa kuuzindua????.....mimi naweza kumsaidia kwa kuanza kumtajia miradi hii...ujenzi wa ukuta mererani,ujenzi wa benki ya crdb chatto,ujenzi wa uwanja wa ndege chatto....kwangu mimi iyo ndo miradi mikubwa aliyoifanya jpm
 
Mimi ni mpinzani ila kama membe atasimama 2020 nampa kura yangu.MEMBE RAIS WA WAWATANZANIA.
 
Acha kabisa Mkuu hili likitokea la Bugirichato kupigwa chini furaha itakayokuwepo nchi nzima itakuwa haina mfano.

Watanzania wengi watalia machozi ya furaha na wengine walioathiriwa na huyo dhalimu kwa namna mbali mbali yatakuwa machozi ya huzuni.
Huku jamii forum mmejifungia watu mnaoota mchana,,, hali halisi ya jamii forum ni tofauti na huku mtaani kulivyo...ngoja tuone mwisho wa hizi ndoto za mchana
 
Anaweza badili katiba , chama kijitenge na serikali kabla ya uchaguzi, na akafanya kampeni kwa makada wote wa ccm kura za ndio zitashinda, nguvu aliyonayo ni kubwa kuliko kijani chenu, yuko hapo mtoeni muone effect yake.

Hivi unajua hii jambo la kumtoa ni yule mwanaharakati ndo kalileta? Halafu ukaandikwa waraka kumlalamikia huyo mwanaharakati, Halafu zikavujishwa clip za sauti? Mpaka hapo huoni kuna tatizo?

Hakuna sababu ya hii vita na kutunishiana misuli na watu ambao mwenyekiti ana nguvu kuwashinda. Awaite aWape maelekezo anataka nini asiyefuata maelekezo atumie nguvu na mamlaka yake kuadhibu,sasa ukiona hakuna hatua basi ujue ili linalozungumzwa si la kweli(la mitandaoni tu) ama lipo Ila wahusika wanafata taratibu za chama hivyo mwenyekiti hana sababu ya kuwaadhibu maana kazi kubwa ya kiongozi wa chama ni kuleta umoja na mshikamano chamani.

Hakuna Mtu mwenye uwezo wa kumtoa mwenyekiti bila kufata taratibu, ni taratibu za chama kumpitisha mgombea kwa miaka kumi Ila pia ni taratibu za chama kuruhusu mtu mwingine yoyote anayetaka kujaribu hiyo nafasi, halafu wanachama akiwemo mwenyekiti aliyepo wampime kama atafaa. Sasa vita ya nini? Tunaongea kama vile mwenyekiti anataka kuyang'anywa cheo chake kimabavu wakti ni taratibu tu za chama. Usisahau kuwa taratibu hizo ndo zimempa hiyo nafasi.

NB: sina tatizo na Utendaji wa raisi, anajiahidi na vitu anavyofanya vinaonekana. Juzi nilisafiri na lindege Nikasema huyu jamaa anafanya vizuri na kama ni kura kati yake na upinzani ningempa yeye maana sioni mtu kwa upande wa upinzani. Lakini naipenda demokrasia, na siwezi sema mawazo yangu mm ni lazima yawe mawazo ya wote. Mawazo ya wengi lazima yaheshimiwe. Ndivyo siku zote tunavyoenda, ndio msingi wa utulivu wetu.

Mwisho Watu ambao hawaeleweki ni nyie mnaodhani kwamba raisi ni mkubwa kuliko chama. Kabla hujang'ang'ana na hili fahamu kwanza idadi ya wafuasi na wanachama wa kijani ndani na nje ya mfumo. Halafu ukumbuke wajibu wa chama kwa serikali.
 
Piga chini Magugumaji, hatutaki ujinga!
 
Ndoto nyingine bwana zinachekesha kama siyo kufurahisha. Anyway, tunaambiwa na waatamu tuishi kwa ndoto zetu. Ha ha ha ha
 
Nitawapoteza wote hao!
 
Watanzania Kwa jinsi tunavyomkubali magu 2022 tutaomba kura ya maoni ili raisi aongoze Kwa vipindi vinne ili tumuongezee magu miaka kumi mingine tuhakikishe kizazi cha mafisadi kimepotea kabisa
 

Hiyo ndo tunaita ‘day dreaming’ ndoto za mchana! Yaani kakamtu alikuwa Rais na mdogo mtu ndo achukue mandaraka na chama tawala kishatoka kule kilipokuwa nusu mfu 2015!!!!!! Yaani tukabidhi nchi kwa manyangau, wapiga madili!!! Wale wale waliouza viwanda na mashirika ya umma yote!!!!! Kabisa haingii akilini! Bahati waliikosa 2015 na sasa wajaribu 2035!
 
Siasa ya leo ndiyo ina determine mjukuu wangu ataishije mwaka 2060 wakati mi sipo hapa duniani...kuwaachia hawa wana siasa watuamulie wanavyoona inafaa kwao ni kosa kubwa sana ambalo hata Mwenyezi Mungu hawezi kutusamehe..

Hawa dawa yao ni mguu kwa mguu...bandika bandua...

Kachero Membe chukua form...2020.
 
Uwenyekit pembenii kwenye nec


Na usilolijua kisu kipo kwa wachinjaji...
 
Mh rais ndugu Bernard Kamilius Membe...
Ina sound vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…