Upendo huanzia ndani ya moyo

Upendo huanzia ndani ya moyo

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
HABARI WAKUU

Nimeahidimika sana mjengoni hapa kwa kuwa nilikuwa na ubize fulani ila kwa sasa niko huru kidogo

Marafiki zangu leo nimeona niseme japo machache yaliyomo ndani ya moyo wangu kuwagusia sana
na kuwaasa wale ambao wanaona mapendo ni nje ya moyo au kumpenda mtu ni kwa ajili ya vitu au
kitu fulani la hasha hata ikiwa hivyo vitu navyo inachukua sehemu ndogo sana ya upendo,

Mara nyingi hutaona watu wakipenda mtu kwa kitu au kwa jinsi vile alivyo na wimbi hilo wanalosana
ndugu zetu WANAUME wao hupenda kwa kuangalia nje ya mtu na sio kumpenda mtu kwa kuangalia
ndani ya mioyo yao je unapenda au unawapenda kwa mantiki gani au kitu gani kimekuvutia kwake?

UPENDO HUANZIA NDANI YA MOYO

Ninapozungumzia upendo umegawanyika katika sehemu kuu tatu

a) kuna upendo wa kindugu, familia
b) kuana upendo wa fileo yaani rafiki/ mahusiano nk
c) kuna upendo wa agape (huu ni ule upendo ambao haungalii huyu mtu yukoje unapendo wa kindani zaidi)

Leo nazungumzia upendo wa mahusiano ya kiurafiki /kimpz ambao siku hizi wa vijana wa kileo wao
huangalia kwa kumtamani mtu kwa nje na sio kumpenda kama kupenda kwa ndani ya moyo wake yeye
huangalia huyu mtu ana nini ambacho ataweza kunitimizia au awe na murano, bmw au pochi ya kuaminika
iliyotuna hivyo ni vigezo ambavyo vijana wengi huangalia awaangalii upendo ule wa kiundani ambao hata kama mtu ana kitu unapenda tu ilimradi moyo umependa pale, uwe nacho au usiwe anacho ila vijana wa kileo utasikia
wakazi gani mm huyo nimpende ana mbele waala nyuma , katika maisha vijana wenzangu kuna mapitio mengi
huwezi jua yule unayemwona leo kachoka sana ana mbele wala nyuma mpe miaka 2 utakuja ona alivyostawi na
kuchanua na ukashangaa ana familia yake ndipo utakapojuta na kusema laiti ningekuwa naye kipindi kile alivyokuwa
chokambaya ? sasa hapo unakuja kusema wakati kumeshapambazuka wewe unavuta shuka kweupe kunang'aa
na jua la asubuhi limechomoza

Kijana mwenzangu hebu jaribu kumpenda mtu kwa moyo wa dhati wa upendo uliomo ndani ya moyo wako sio kwa
kuona kitu kwake eti ndo unampenda je ikatokea hivyo vitu vimeungua au havipo Upendo wako utaupimaje?
utaupima kwa hivyo vitu au kwa utu wa huyo mtu, Vijana wenzangu tubadilike tufumbue macho kukiwa bado mapema
wakati kabla usiku haujaingia.

Kuna wengine wako katika mahusiano na watu wao wanaonesha upendo wao kwa kumtwanga mwenzake utafikiri
yule anayemtwanga ni gunia lisiloumia yeye anaoona fahari kubwa kuwa upendo ni KUTWANGANA kumbe anakosea
hajui kuwa mapz ni kubembelezana na kuheshimiana na kupendana pasipo magomvi anasahau kuwa huyo anayemtwanga naye ni mtu kama yeye anasahau kuwa aliumbwa kwa ajili ya yake kwanini anamtwanga eti anadai kua hapo ndo anaonesha mapenzi yakweli kuwa anampenda kumbe ndo anahatarisha ndoa yake na mahusiano yake.
Vijana upendo sio kutwangana upendo ni ile hali ya kumuonesha mwenzio kuwa unamcare na kumhandle mwenzio
yeye aliumbwa kwa ajili yako nawewe kwa ajili ayake acheni tabia za kuiga toka uarabuni jamani mapenzi ni kupendana
na kutakiana heri na umahabuba sio mitwango usiku na mchana kisa waonesha kumpenda na kujali nani amewaambia kuwa NDODI ni sehemu ya mapendo MSIDANGANYIKE JAMANI MPENDE MWENZIO KAMA NAFSI YAKO

Nawatakia kila kheri kwa wale walioko kwenye mahusiano mema, na kwa wale wanaojiandaa na kwa wale mabestito
wenzangu wote tuamke kwani usiku umesonga na mchana unakaribia

Nawapenda wote

Wasalaamu

Ladyf
 
karibu tena best

mapenzi haya ya digital ukipeda kutoka rohoni mmmh utashagaa kwani kama umekariri neno kaunta ni bar unapata vinywaji ila kuna neno kaunta police
 
whatever !!!!!
huyu binti nampenda sana zaidi ya sana ila hajui
 
Ni kweli mkuu ila wako wengine wanampenda mtu kwa kitui alichonacho na sio vile alivyo huyo mtu sasa hapa kuna upendo au ndo kutamani best
upendo unakuja automatic....huwezi kumpenda mtu kwa kumuonea huruma eti ngoja nimuoe tu kwa kuwa unamuonea huruma....
 
nipende kwa moyo wangu wote alafu mimi nijibakishie nini? hawa wanaume wa siku hizi ni shida
 
Asante kwa somo zuri..... ila tuvumiliane tu ktk dunia ya sasa upendo ni wa kuutafuta na tochi sijui kwanini yan daaaa
 
Vijana wa siku hizi hawajui kutofautisha upendo na tamaa, utakuta mtu kakutamani tu lakini atakuambia ninakupenda tena kutoka moyoni
 
siku hz kama unampenda sana usimwambie we kausha tu ukijitia kihere here kumwambia utakuwa unalia kila siku hata miss chagga analijua hilo!!!!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli,asante kwa somo zuri,palipo na upendo wa kweli kila kitu kinakuwa sawa.Mungu ni pendo yatupasa hata sisi kupendana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom