Upendo Furaha Peneza: Gold in the rough. Vijana CHADEMA mpo?

Tuwahamasisheni vijana kutoka kila mahala nchini watoe mchango wao wa kisiasa hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi.
 
Mkuu sweya lugendo baada ya kuusoma vizuri huu uzi wako, nimegundua kuwa unayemzungumzia hapa ni Binti mmoja aitwaye UPENDO PENEZA bila shaka, ingawa sijawahi kukutana naye ana kwa ana, ila nimemfahamu kupitia ukurasa wake wa facebook "Upendo Peneza", na niliwahi kuisoma Post yake iliyohusu huyo Kiongozi wa upinzani wa Uganda unayemsema.

Kubwa zaidi, tunamtaka yeye mwenyewe ajitokeze hadharani kupitia ID na Account zake za mitandaoni atupe maelezo ya ndoto zake hizo, na aambatanishe CV na wasifu wake ili tuanze mjadala kama atatutosha kweli kwenye nafasi anayoitaka.
 
Hili jina sio geni masikioni mwangu,nafikiri kwa hapa Dar anakaa jimbo la Segerea!!!
 
Tuwahamasisheni vijana kutoka kila mahala nchini watoe mchango wao wa kisiasa hasa wakati huu tunapoelekea uchaguzi.

Hili ni tatizo na limeishaingia kwenye bongo na mifumo ya damu ya wahusika. Mifano ipo hai kwani hata tulio watumainia mwisho wa siku wamegeuka "viloja" na "gumzo". Na tatizo kubwa hapa kuiingiza "si hasa" katika maisha yetu ya kila siku kuliko Mungu.
 
Mara ya kwanza kumwona na kumsikiliza live ilikuwa Kakola Kahama,mara ya pili juzi Nyang'hwale,nimemsoma akiwa Uganda na aliyekuwa kiongozi mathubuti wa chama pinzani Besigye na kwenye mijadala kadhaa ya gesi akitokea Norway.

Ni kijana binti mdogo mwenye uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja za kitaifa na kimataifa,huwezi kumsikiliza usimpongeze vinginevyo uwe na wivu uliopitiliza mno.

Naomba achukue fomu ya uongozi wa juu kabisa wa Bavicha taifa na asiogope vitisho na mbwembwe za wengine, vijana wenzake wamuunge mkono maana kakamilika.

Nawasilisha kama kuna mwenye kumfahamu zaidi amwagike.

Mkuu sweya lugendo, Binti huyu UPENDO PENEZA ni miongoni mwa Wanawake ambao ni Great thinkers wenye mtazamo chanya katika mambo ya Kitaifa na Kimataifa.

Mimi binafsi namsihi sana asikate tamaa kujaribu kujitokeza na kujipima uwezo wake dhidi ya vijana wenzake, yeye ajaze fomu asiogope na aonyeshe nia ya kweli.
 
Last edited by a moderator:
Namfahamu kwa kiasi Fulani huyo Dada, nimpiganaji mwenzetu katika Kata ya Segerea...no mtu makini sana..anayejitoa kufanya Kazi ya chama
 
Namfahamu kwa kiasi Fulani huyo Dada, nimpiganaji mwenzetu katika Kata ya Segerea...no mtu makini sana..anayejitoa kufanya Kazi ya chama
Ubarikiwe sana kwa kusema juu ya Upendo.
Upendo ni kijana makini,binti anayejitoa sana kwa chama nje ya Segerea.Hata huko Geita Upendo amekuja mara nyingi.
 
Kwao ni Geita lkn wazazi wake wapo Kaluta-Mwanza!Hana chembechembe zozote hata za kinasaba na Rwanda!
Sijui lolote kuhusu mustakabali wake kwenye mahusiano maana hajawahi andika kuhusu hayo!
 
Huyu Si alisoma pale Baptist secondary miaka hiyo.mi sidhani kama anaiweza nafasi ile. Labda aje aongoze familia yenu.
 
Halima Mdee ni namba moja wangu go west go east,wa pili kusema kweli ni Upendo
Furaha Peneza,alikuja kwetu Kakola na Kamanda Mawazo,ukweli
nilimpenda,jana nimemsikilza kupitia "you tube" akiwa Musoma
ni nouma.Msikie anavyojenga hoja juu ya roles of youth in bringing
change,mchakato wa uvunaji gesi,madini yetu na laana ya raslimali
nk.utasisimkwa...YOU KEEP WONDERING LIKE"WHERE HAS SHE BEEN ALL THAT
TIME"Niweke bayana kwamba kama hana madhaifu mengine ndani ya chama
chake ajitokeze jukwaa la vijana "BAVICHA"
 
There is only one woman who is very powerful in CHADEMA...Josephine..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom