Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,355
- 80,010
Anaandika, Robert Heriel
Vijana wenye Dharau na kiburi mnawaona Watu wazima wenye age 45-70. Msiwaone wapole😂😂 msiwaone Kama wamezubaa
😊 Walikuwa wanaringa Kama ninyi, walikuwa na Dharau na kiburi Kama ninyi. Ila Dunia imewafundisha, somo limewaingia.
Ujana maji ya Moto wahenga walishasema, ukishaanza kupevuka/kubalehe unakuwa na Dunia yako kichwani, unakuwa Kama upo ndotoni. Kuna Ile namna unajichukulia na kujiona vile baadaye utakavyokuwa mtu mwenye mafanikio. Ni nadra Sana ukiwa umri huo kujikatisha tamaa.
Kijana wa Umri huo ni rahisi kumdharau binti asiye na vigezo vyake halikadhalika Binti wa umri wa kijana yaani miaka 13-25 ni rahisi kudharau Vijana au wanaume wa namna Fulani.
Jambo moja la uhakika ni kuwa Dunia ndiye Mwalimu Bora atakayehakikisha kila Mwanafunzi atafaulu masomo yote.
1. Dunia itakufundisha Kutokudharau wengine, na utafaulu tuu!
2. Dunia itakufundisha kozi ya KUTOWALAUMU wengine na utafualu tuu.
3. Dunia utajifunza Kozi ya KUTOMUAMINI NA KUWEKA MATEGEMEO KWA MTU, na utafaulu tuu upende usipende.
4. Dunia utakufundisha kozi ya Mipango sio matumizi na utafaulu tuu.
5. Dunia itakufundisha kozi ya Time management, na utafaulu tuu.
6. Dunia itakufundisha Use na Reuse Course na utafaulu tuu.
Yaani Dunia hii itakufundisha Kwa namna ambayo utaelewa Kwa urahisi kuliko ambavyo ungekaa darasani. Alafu mitihani ni tofauti ingawaje kozi ni Ileile, silabasi ni tofauti lakini kozi ni Ileile.
Dunia ninachoipendea ni kuwa hakuna mtu kiburi ambaye kiburi chake hakitatiishwa, hakuna mtu mwenye Dharau ambaye Dharau zake hazitatiishwa.
Wakati unawadharau watu Kwa maumbile Yao Kwa sababu umejaliwa uzuri au hata huna huo uzuri wenyewe basi dunia utakunyoosha Kwa namna ya kukuacha mdomo wazi.
Siku utakapozaa Watoto Wabaya, labda wafupi, au wenye Sura za kuchukiza ndipo Dharau zako zitakapoisha kudharau watu Kwa maumbile.
Watu wengi waliokuwa na Dharau wakidharau wanaume/wanawake wasio na maumbile mazuri dunia iliwapa zaawadi ya watoto wa namna Ileile ya watu waliokuwa wanawadharau. Hapo ndipo mwisho wa Dharau zao zilipokwisha. Wakawa wanagugumia maumivu ndani Kwa ndani.
Hata hivyo wapo viburi ambao husingizia mbegu hizo sio za ukoo wao Bali ni mbegu za aidha ukoo wa mwanaume au mwanamke basi ilimradi kujifariji lakini haiondoi ukweli kuwa hao ni watoto wako.
Wakati unawadharau wasiosoma kisa upo chuo na unamadigrii ya kutosha, Dunia itakufundisha kozi maalumu ya kumheshimu kila mtu. Sio ajabu ukashangaa wasiosoma ndio wenye mafanikio kukuzidi, au pengine Watoto wako WA kike wakapewa mimba na hao wasiosoma tena binti yako akawa Kara kaoza huku akitishia kujiua kisa hao uliokuwa unawadharau😊.
Kama hiyo haitakuumiza sio ajabu Mkeo akawa anachepuka na mtu wa ajabu ajabu asiye na elimu yoyote. Hayo ndio Maisha. Usipojifunza kuheshimu watu yenyewe yata-take Role kuhakikisha unafaulu somo la kutokudharau wengine.
Wakati unamlaumu Mumeo kuwa ni kibamia na Hakuridhishi kitandani, tena ikafikia hatua ukamuacha Kwa maneno ya shombo, nakuhakikishia Dunia itakupa somo zuri Sana ambalo litakukumbusha na kukufundisha kuheshimu na kuvumilia watu wengine. Hata kama ni miaka 20 ijayo lakini somo lazima likufikie. Raha ya Dunia inatabia ya kutohairisha kozi, yaani utafundishwa tuu bila kufuata Ratiba😂😂.
Siku Vijana wako wa kiume wakilalamikiwa kuwa hawana nguvu za kiume na Wakamwana wako vile utakavyojisikia vibaya kuona Vijana wako wakiume wakiteswa Kwa maneno makali na wake zao(wakamwana wako) hapo ndipo utajifunza kuheshimu hata Hali za Fedheha za watu wengine.
Jinsi unavyomdharau Mkeo labda anamapungufu Fulani, labda Hana shepu nzuri, au anamaji mengi, au anauke mkubwa, au kanenepa Sana au anakasoro nyingine yoyote Ile. Ukamponda na kumpa maisha magumu bila kumstahi na kumvumilia.
Nakuhakikishia Dunia itakufundisha tuu vile ambavyo ulipaswa kufanya.
Dunia haipendi Dharau Hilo weka kichwani, dunia haipendi Kibri na majivuno.
Majibu yake utayapata Kwa wale unaowapenda Kama wewe hutojijali Sana.
Angalia wanawake wanaojiona wazuri wenye Dharau Kwa wanaume alafu angalia watoto wanaowazaa yaani ni Copy na paste ya Wale waliokuwa wanawadharau.
Halikadhalika na wanaume.
Huko uzunguni na jamii zenye Ubaguzi wa rangi Kwa Waafrika ni kawaida Sana Mabinti wa kizungu kuzama kimapenzi na Waafrika kutokana na vile wanavyotuona tunavutia. Hii hupelekea maumivu makali Kwa Watangulizi wao kuwa waliowadharau Leo ndio wanatoka na Watoto wao. Hali hiyo inasababisha mauaji au matokeo mabaya zaidi kufanyiwa Waafrika.
Maisha haya lazima uende nayo Kwa step. Kila unachofanya uwe nacho macho.
Unadharau Walevi alafu wao ndio siku moja watakupa msaada. Hakuna maumivu mabaya Kama kusaidiwa na mtu uliyekuwa unamdharau. Inatesa na inaumiza Sana.
Heshimu kila mtu. Na Kama huheshimu kila mtu basi jifunze kuficha Dharau zako Kwa watu.
Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam