Updates za Corona Tanzania

Updates za Corona Tanzania

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,051
Reaction score
828,857
Natambua umahiri wetu wa kuvifanya vitu serious kuwa mizaha. Natambua ujuzi wetu wa kuyageuza majanga kuwa manufaa ya kisiasa.

Hivi ni kipi kikubwa tumekifanya kama taifa cha serious kujikinga na hili gonjwa linalotaka kuwa janga la dunia?

Nimemsikia Waziri wa Afya akikutangazia umuhimu wa kutoshikana mikono wala kukumbatiana wakati wa kusalimiana kama ilivyo jadi yetu. Wanasiasa wakalibeba hili mzobe mzobe. Mengine yote sidhani kama yamepewa kipaumbele.

Waziri katangaza kila mkoa utenge maeneo maalum ya kuchunguza wenye dalili na viashiria vya huu ugonjwa.

Je, hili limetekelezwa?
Je, kuna vifaa ya kutosha kwenye hili?
Je, bajeti imetoka wapi?
Je, kuna wahudumu wa dharura wenye uelewa na huu ugonjwa wameandaliwa?
Je, sahihi ni kutenga vituo kila mkoa ama kila wilaya?
Je, mpaka sasa ni mikoa mingapi imelitekeleza hili?
Je, kuna changamoto yoyote?
Je, kuna kipindi maalum kwenye vyombo vya habari kutoa mapya ya kila siku kuhusiana na huu ugonjwa?

Hakika maswali ni mengi sana. Lakini nilichokiona kwenye huu ugonjwa ni mizaha na kukosa umakini. Hatuna takwimu rasmi zozote mpaka sasa za chochote kuhusiana na huu ugonjwa. Hatujaona umakini wowote kwenye maandalizi ya dharura. Chukulia mfano mkoa wa Pwani kutoka Mkuranga mpaka Bagamoyo utenge kituo kimoja tu cha ukaguzi wa corona, inawezekana kweli!?

Kinachopigiwa chepuo sasa ni kusalimiana bila kushikana mikono, eti kugongesha miguu. Mmh! Tumeiona kwa viongozi, lakini nyie msioshikana mikono sasa si mlikaa chumba kimoja kwa madakika mengi tu? Je, mlitumia viziba midomo na pua?

Hivi kwani corona ni ugonjwa wa ngozi? Iweje wachezaji uwanjani wazuiwe kusalimiana kwa kushikana mikono eti ni mojawapo ya kampeni ya kupambana na corona wakati huo huo wachezaji haohao watakuwa pamoja uwanjani kwa dakika 90+ wakishikana, wakivutana, wakiangukiana wakipumuliana? Vipi na wale mashabiki watazamani kwa maelfu walio majukwaani? Tuna abiria kwa maelfu wanasongana kwenye vyombo vya usafiri. Kwenye masoko. Kila mahali.

Bado hatuko serious na mizaha ndio imetawala kupitia siasa. Mungu pekee ndio anatubeba. Kitengo cha dharura kitaifa hakijasema chochote. Kipo kimya kabisa. Vyombo vyetu vya habari ni siasa na wanasiasa mwanzo mwisho. Viziba pua na midomo vimepanda bei maradufu. Box lilikokuwa linauzwa elfu 10 piece 50 sasa hivi linauzwa elfu 40 na hapo ugonjwa haujachanganya. Ukithibitika upo nchini na tukatakiwa kutumia hivyo vifaa tutafanyaje?

tapatalk_1583345397653~2.jpeg

Jr
 
Tuna natural resistance na huu ugonjwa la sivyo ingekuwa muda huu tunaongea mengine

Jr
Mungu anajua hali zetu sisi ngozi nyeusi ugonjwa kama huu ukitua dar karibu nusu ya watu wamaweza ambukizwa, ile nyomi la mwendokasi, daladala za mbagala na gomz, msongamano wa kariakoo!! tunaponaje hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumezoea utani na kila kitu kumuachia “Mungu” hatakama ni jukumu letu kutatua jambo utasikia ‘Mungu atuepushe’
Ukiona BBC wanavoonyesha hatua za hizo nchi zingine zinavuchukua unaweza kusema pengine sisi tuko sayari nyingine ndio maana tume relax.

Washington juzi kuna mtu alikua Diagnose na hiyo kitu walifunga Metro, Shule zilizokua Karibu na barabara ya yeye alipopita pamoja na kufanya Fumigation ya mahali pote alipokanyaga.

Kwetu sisi ni maigizo kwenye Daladala kugusana lazima bado pantoni, Kariakoo misongamano daily. Kingine ni mtu akiwa na dalili au akiwa ametoka kwenye hizi nchi zenye haya milipuko inapaswa akae Quarantines kwa siku 21 kujua kama anao au la, pale JNIA wanapima temperature tu ikiwa normal unasepa kama unao dalili utaenda kuzipata nyumbani kwako.
 
Nakili waziwazi kusema kuwa Tanzania ipo ipo tu yaani inajiendea jiendea tu ilimradi miaka uende bhas tujulikane duniani tu kuwa kuna nchi Afrika ya Mashariki inaitwa Tanzania. Hakuna sera/ vipaumbele vya nchi kama nchi katika sakata zima la kuutokomeza umasikini nchini.

Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu, ndio sector iliyoajiri watanzania wengi kuliko sector yeyote inazidi kudidimia na hakuna njia wala mikakati ya kurevive. Kilichobaki ni kilimo cha subsistence tu.

Afya hapa ndio kiini kikuu cha mada husika, masikhala mengi juu ya afya ya mtanzania. Kwa macho yetu tunaona tahadhali na mikakati mbalimbali ambayo nchi nyingine wanachukua dhidi ya huu ugonjwa, lakini sisi tupo tupo tu na kauli za kisiasa.

Ugonjwa huu utakapogonga hodi hapa nchini, tujiandae kuona death toll ikiizidi hata ya China ugonjwa ulipoanzia. Siombei mabaya ila nasema hivi kwasababu ya masikhala yetu katika kujihadhali na huu ugonjwa.

Mungu tusaidie
 
Mungu anajua hali zetu sisi ngozi nyeusi ugonjwa kama huu ukitua dar karibu nusu ya watu wamaweza ambukizwa, ile nyomi la mwendokasi, daladala za mbagala na gomz, msongamano wa kariakoo!! tunaponaje hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Bill Gates katabiri vifo milion kumi kama virus vya huu ugonjwa vikifanikiwa kupenya Africa.. Manake hatufanyi juhudi zozote zaidi ya matamko yasiyo na tija2.. Na mengi yakiwa ni ya kisiasa zaidi

Jr
 
Na wewe unaamini kweli tutakufa milion 10! Wakati Hadi Sasa vifo vimefika 3200 kwa Dunia nzima na hakuna mwafrika hata mmoja.

Nani kakwambia mwafrika anakufaga kwa mafua?

Corona it's just a flu.. Relax mpiga tunguli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ugonjwa unasababisha failure ya mapafu pamoja na figo halafu wewe unadai kuwa ni ugonjwa wa mafua? Upo serious mkuu?!
 
Back
Top Bottom