Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Uchaguzi huu nadhani ulikuwa wa ovyo kimaandalizi kuliko maelezo.
Huwezi amini kwamba viongozi wa nchi hii wanaweza kuandaa uchaguzi na wasiweze kuchapisha karatasi maalumu ambazo si rahisi kugushiwa.
Karatasi zile nilizoona zinatumika hata wewe ungeweza kujitegenezea nyumbani kama una nia mbaya.
Kisha kwa nini ilikuwa mpaka mtu uandike majina badala ya kuweka vema? Watu wengi walikuwa wanafanya vitu vilivyosababisha kura nyingi kuonekana zimeharibika. Nchi hii kwa kweli ni utata mtupu.
Kisha kwa nini waliokuwa wakiandisha wapiga kura ni hao hao viongozi wa Sisi m? Mbona wengi niliona ni viongozi wa kwenye kata na ambao ni wana sisi m vilevile?
Bukoba sisi m imeshinda baadhi ya mitaa na Chadema imeshinda baadhi ya mitaa.
Kuna mtaa mmoja unaitwa Rwagati ulikuwa na mchuano mkali sana! nashangaa hata Karamagi alikuwepo kuongeza nguvu ili mgombea wake wa sisi m apite maana ndio wameshaanza kujiweka tayari kwa ajili ya 2010. Ni kwa nini aliweka kambi pale anajua mwenyewe lakini mwisho wa siku Chadema wameibuka kidedea kwa ushindi wa kishindo.
Ignorance imeonekana wazi kwani wengi hawajui kuandika wala kusoma. Ni ajabu na kweli lakini hiyo ndio hali halisi. Kama uchaguzi wa 2010 nao ukifanyika hivi sijui mambo yatakuwaje.
Kisha matumizi ya pesa kwenye uchaguzi yanatishia usalama wa nchi hii. Kama hakuna ufumbuzi wa jambo hili basi si muda mrefu tutasikia hii wanaita amani na utulivu havipo hata kama polisi wapo.
Siku zote naamini na nitabaki naamini amani haitunzwi na polisi bali watu wenyewe. Nakwambia hata kama utaweka polisi 1000 mahali ambapo watu hawajaamua kutulia na kuwa na amani, basi utawaua wote na bado chaos itakuwepo. Tunao mfano mzuri wa Pemba. Na hii inawezakuwa Tanzania nzima. Tujiepushe na matumizi ya pesa kwenye chaguzi zetu. Polisi wetu wajiepushe na siasa kwenye chaguzi zetu maana haiwezekani mtu anagawa pesa mbele yao na wanaona hawawezi kuchukua hatua. Sijui wako pale kwa maslahi ya nani.
Naishauri serikali na jeshi la polisi kutobweteka kwa hilo la amani na utulivu , labda kama wanahitaji kuwaua wananchi ili wao watawale hapo sina neno. Sijui watakuwa wanatawala miti?