Updates uchaguzi serikali za mitaa - mtaani kwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Updates uchaguzi serikali za mitaa - mtaani kwetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mayolela, Oct 25, 2009.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu tupeane updates

  Mie nimetoka kupiga kura lakini,nimeshindwa utaratibu ni mbaya kupita kiasi.
  Oroadha ya majina ya wapiga kura ambayo ilibandikwa jana imelowa yote na mvua ya jana-mpaka sasa zoezi zima la kupiga kura bado alijaanza-na kwa maaantiki hii watu wengi sana awatapiga kura leo kutokana na kasoro za urodheshaji wa majina kwenye mbao za vituo.
  Mimi ni natakiwa nipige kura Buguruni Kisiwani-kwa mantiki hii sipewi fursa ya kuchagua mwenyekiti wa serikari ya mtaa wangu ,kwa sababu ya uzembe wa watendaji katika Manispaa husika.
  Naomba update mitaa mingine.

  Mdau wa Lusungo Ipinda Kyela.
   
 2. j

  jonbalele Member

  #2
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania inazidi kuelekea kubaya. Nchi zingine zinazidi kuendelea mbele kwa kuwa zina mikakati thabiti sisi tunaendelea kwa kurudi nyuma!!! Oooh Mungu tusaidie... Nani ataiokoa? Mambo haya yanayofanyika ni ya ajabu sana. I hate. Inabidi tushikamane tupigane unless nchi itazidi kubaki mikononi mwa wachache wenye tamaa ya fedha, ufisadi na madaraka....
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  ccm na chadema wanakabana koo maeneo mengi mnu.....
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Watumishi wengi wa manisapaa wanasema wazi wazi kwambva CCM inatumia Piolisi na wakuu wa Wilaya kushinda na si kwa kupendwa hapana . CCM wanatumia vitisho na wizi pale ambapo wanaoneka hawakubaliki na ndiyo maana tangia mwanzo Pinda hakuwa tayari kuweka wazi mambo haya maana alijua Chamma chake hakitafiuta mbali . Thanks for the update maana watu hao wa mtaani nawalinganisha na watu wanao chonga hapa JF wana elekeza kila kitu lakini hawajawahi kujiandikisha kupiga kura wala kaidi mpiga kura hawana .Wanakuja baada ya stress za maisha ughaibuni.Talking from JF alone will not save my dear Country japokuwa ni ukwelo pia kuna issues nzito JF imezisimamia na impact nahata changes zimeonakana.

  We need to do more
   
 5. T

  Tewe JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Wakuu, na vijiji vitano huko Kilimanjaro ambako imetangazwa hawatafanya uchaguzi kabisa kwakuwa wagombea wa CCM hawajapata wapinzani ni sahihi kweli?

  Mimi nadhani wananchi wangepewa uhuru wa kupiga hata kwa hao wagombea wasio na wapinzani.
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa ufupi tu nawajulisha maendeleo ya uchaguzi kwa wilaya mbili nilizozipitia asubuhi mkoani Kigoma;

  Nikianzia Kibondo naona mchuano utakuwa wa wastani kati ya Chadema na CCM ila watu si wengi waliojitokeza vituoni kupiga kura.

  Baada ya mizunguko yetu ya Kibondo, mida ya saaa 3 tulielekea wilaya ya Kasulu na bado tupo huku kwa hivi sasa; huku ndio ni maajabu ya mwaka. Watu ni wachache mno katika vituo vingi sn, sasa sijui kwa vile leo ni Jumapili wapo kanisani au ndio hawakujiandikisha.

  Ila tulijaribu kuwahoji baadhi ya watu hasa vijana na wale wa rika la kati na kati; wengi wao wamesema hawakujiandikisha kwa sababu kadhaa; mojawapo ni muda mchache waliopewa wa kujiandiksha, vituo kuwa mbalimbali sana na maeneo wanayoishi (vituo vyote tulivyotembelea vipo ktk shule za msingi.

  Kwa eneo la Kasulu mchuano unaonekana utakuwa ni wa CCM na NCCR Mageuzi {nampongeza mwana mama fulani hivi kwa kujitolea kwa hali na mali kuzunguka maeneo mengi kuwapigia debe wagombea wake; huyu mwanamama aliwahi kugombea ubunge na wakachuana vikali na nzansugwanko (mb)}

  Nawasilisha....
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa mara ya kwanza niliamua kushiriki kwa karibu uchaguzi huu lakin i nimeambulia kukata tamaa kubwa sana mpaka sasa natufuta pa kutokea tu. Nashukuru leo ni jumapili na ilibidi niombewe ili niwee kurudi katika khali yangu ya kawaida
   
 8. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #8
  Oct 25, 2009
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Duhh..Hii kali sasa nini kimekutokea ndugu yangu? Na vipi kule kwetu Kyela mambo yamekwendaje? Yule Injinia wetu kawa kimya sijuhi amepatwa na nini
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Wanajua walichopanga na wanajua jinsi ya kutekeleza ila siku moja midomo itawabaki wazi
   
 10. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mie naona huu uchaguzi ni usanii mtupu kutoka kujiandikisha mpaka upigaji kura kwa kuandika jiana la mgombea. hela zimetumika katika uandishaji feki na zinakosekana za kuchapisha karatasi za kupigia kura za kueleweka, kwa nini tusingetumia tu vitambulisho vyetu vya mpiga kura ili kusevu pesa.

  kwa mtindo huu, tunasubiri tu ushindi wa sunami wa ccm
   
 11. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Wizi mtupu!
  Nimekwenda kupiga kura hapa Sinza. Wagombea katika nafasi zote 7, wakiwa kama 14 ni wa CCM. Ina maana hakuna hata mmoja kutoka upinzani mwenye sifa? Maelezo niliyopata ni kwamba wengine wameenguliwa.

  Nimepiga kura, lakini sijamchagua yeyote.
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ngoja na mimi nikapige kura ndo nije humu.... naona kila mmoja ana kuja na hoja za siku nyingi na sis za leo...!
  TUKAPIGE KURA.....MUDA UNARUHUSU...!
   
 13. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mhhh! Mwaka huu. Nilidhani ni wagombea tu wanaenguliwa! Mimi kama mpiga kura nilienguliwa kwa sababu za kiufundi. Sikuweza kujiandikisha kwa sababu ya muda uliowekwa sikuwa katika jimbo lango/eneo langu la uchaguzi! Huu ni uvunjwaji wa haki zangu za msingi!
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Ina maana huamini wasemayo wananchi hawa ama una maana gani ?Habari za zamani means what /
   
 15. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mambo ya uchaguzi huku ni moto juu ya moto, mbavu za kati kuna Ccm na Cuf, mh! Hatoki mtu mpaka kieleweke, pande za kigamboni huku hapatoshi kivilee! Nafasi i chache na hewa i ngumu, watu wengine wamezimia kisa kimuhemuhe cha kuvote, japo kuna matatizo kwa wale kina maimuna dah! Mtu anatafutiwa jina, anapigishwa kura na n.k, sioni kama kweli wanapata haki yao, mpaka sasa hali ni kukabana koo, kila chama wanajaribu kutumia muda huu mchache ulobaki kurekebisha mambo, nafkiri tutazidi kujuzana yanojiri hapa... Kisiwani...kigamboni.... Inshaallah...
   
 16. E

  Engineer JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Samahani mkuu, unajua inaudhi sana, tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu na kazi zetu kulalamika tu.

  Huku vijijini kuna watu wengi wanataka mabadiliko lakini hakuna nguvu kubwa ya vyama ya kuleta ujumbe wenye matumaini.

  Wengine tunajaribu kuwaelemisha lakini haitoshi.
   
 17. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #17
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Naungana nawe katika kumpongeza kwa jitihada zake, mpongeze zaidi baadaye endapo jitihada hizo zitazaa matunda. Ni Mhe.Zaituni Buyogela?
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  huyu anayejiita engineer sijui ana matatizo gani
   
 19. E

  Engineer JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa Kyela mjini CHADEMA wameshinda vitongoji viwili walivyokuwa wanagombea.

  Ushindi mkubwa ni wa mzee Kungaipi (CHADEMA) ambaye amemshinda mpambe wa Mwakyembe anaiyeitwa Kilumbu (CCM). Mbunge alikuwa hapa wiki nzima kumpigia kampeni lakini haijasaidia.

  Wacha nikanywe na kubeba sanduku la Kilumbu. Huyu ndiye yule mwandishi habari fake anayeshirikiana na Mwanakatwe kutuma habari za uongo Nipashe.

  Nyie CHADEMA mungefanya kampeni kwenye kata nyingi hapa Kyela, mungeweza kupata wajumbe wa kutosha. Tumechoshwa na hawa CCM na ugomvi wao kila sehemu na migawanyo mingi.
   
 20. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hiyo nafuu ndugu yangu. Taarifa za hakika zilizo tufikia hivi punde ni kuwa Katika Manispaa ya Iringa Mkurugenzi na timu yake wamevuruga kabisa uchaguzi wenyewe. Leo kulikuwa na maandamano CCM na vyama vya upinzani wamekwenda kumuona Mkuu wa Mkoa. It seems Mkuu wa Mkoa anataka uchaguzi urudiwe lakini haijulikani kwa gharama ya nani na sijui kama wananchi watajitokeza tena. Mbaya zaidi RC mwenyewe hakuwepo Iringa hadi siku ya kupiga kura. JK anakwenda huko kesho. Kama kawaida watakachofanya waungwana ni kumdanganya Rais wetu.

  Kingine kinachoshangaza ni utaratibu wa TAMISEMI kufuatilia uchaguzi kwa simu badala ya kutuma wataalamu kwenda mikoani kujionea hali halisi na kutoa ushauri wa mara kwa mara kama wafanyavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Aibu.
   
Loading...