Afya ya Mzee Mandela, imeendelea kuwa siri kiasi kwamba hali inatisha. Ukweli kwamba kaburi limekwishachimbwa unaashiria huyu mzee hatunaye tena, ama itakuwa kitu cha ajabu kwa mila na desturi za mwafrika iwapo kaburi litakuwa limechimbwa wakati Mzee akiwa hai. TUNAOMBA TU IWE KITU CHA AJABU this time acha mila za mwafrika zisimame kidogo, eh mora twakuomba.
Kuna uwezekano kuwa Mzee Mandela alikufa akiwa anapelekwa hospitali wala hakufika hosptalini akiwa hai. (kumbuka stori kuwa ambulance ilipata hitirafu, harafu fikirikwanza) Ukweli kwamba imekuwa siri na mzozo mkubwa tangua afikishwe hospitali kuhusu nani anaweza kumwona na nani hawezi, ukweli kuwa familia yake kokote iliko dunia imekwisha rejea south Africa, ukweli kuwa wajumbe wa ANC hawawkuruhusiwa kumwona, ukweli kwamba eti rafiki yake wa siku nyingi sana badala ya kumwombe swahiba yake apone, alikubali aachwe afe apumzike unaashiria kuwa Mzee this time ametutoka.
Tatizo langu sio Mzee kututoka, japo nafahamu wazi pengo lake sio pengo bali ni kinywa kizima hatuwezi replace hata kidogo, Kama ilivyo kuwa kwa Nyerere mara hii South Africa nayo imefanya hivyo hivyo kwa malengo ya usalama zaidi kuliko historia, najua kama mzee Mandela alivyokuwa muwazi asingependa mambo ya uongo uongo kwenye suala la kifo chake, lakini nyota iliyong'ara afrika na duniani sasa inazima.
Zaidi ya yote Mzee wetu katangulia, tutamkumbuka daima na milele, najua kama kuna maisha baada ya kifo watapenda wakutane na Nyerere kwa sababu moja au nyingine.
Kwa uchungu sana , tutalazimika kusema kwa heri Mandela mara itakapotangazwa rasmi, kipaji alichokujalia Mungu, hakika umekitumia kwa manufaa ya watu wote duniani, hususani waafrika ambao kwa mapenzi ya mungu huyo huyo historia ya ukoloni haitafutika.
Viva Nelson Mandela, Vivaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!