PostGE2025 UPDATES - OCT. 29, 2026: Hali ikoje eneo ulipo?

PostGE2025 UPDATES - OCT. 29, 2026: Hali ikoje eneo ulipo?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hakuna jambo lolote, mnajipa moyo tu.Hakuna Mtanzania atakayekubali ujinga wenu tena. Enough is enough. Labda wale ma house boy na ma house girl wanane wa wajerumani waliojikusanya kule ujerumani jana.
Wale ni ma house boy na girl wewe ni kenge wa kizimkazi!
 
Updates ni za ibada za kumbukumbu zilizoandaliwa na kanisa katoliki.
 
kuna script moja imechezwa ni katika kila mkoa au manispaa yalipotokea machafuko. hakuna kitu
Hamna script ni kile kibano😀😀wanaochochea wenyewe hawaandamani , watu wako busy kupambana na maisha , wewe eti unakomboa nchi kwa kuvunja duka la mlala hoi mwenzio ...Viongozi hakuna alidhulika wa pande zote , mmebaki matoys kama makondooo ..
 
Kwan leo walisema kutakua namandamano mbona mnajishuku leo nikumbukizi watu wafanye ibada ama chochote kukumbuka mo 29 sasa nashangaa mamwela kila kona wapo
 
Saa 6 Mchana:

Hali katika mikoa yote inaelezwa kuwa shwari kabisa, ikiwemo miji mikubwa na majiji.

Kuna ongezeko la polisi kwenye makutano muhimu ya barabara, taasisi za serikali, na maeneo mengine ya kimkakati ikionekana kama njia ya kuchukua tahadhari katika Mikoa ya Dar, Mbeya, Dodoma na Arusha.

Shughuli zinaonekana kuendelea kama kawaida shuleni, sokoni, vituo vya mafuta, ofisi za serikali, nk.

Saa 12 asubuhi:

Barabara ya Mbezi/Kimara kuelekea Ubungo, Magomeni, Kariakoo, Kituo Kikuu cha Polisi, Posta hali ni shwari, polisi wameongezeka lakini shughuli zinaendelea, hakuna vizuizi. Kituo cha Magufuli na Mwendokasi vinafanya kazi kama kawaida. Magari yameripotiwa kuwa machache na movement ni ndogo, lakini usafiri bado unapatikana.

Polisi wapo wa kitosha lakini hakuna ghasia zozote, pia kuna magari kama saba hivi maeneo ya Coco Plaza.
Hali n̈i kuzagaa kŵa washika mitutu a.k..a chinǰachinja wa kumbùkizi ya mmwaka moǰa ya maùaji ya kimbarri pale jamhùi yaMalawi.Kìla makutano ya njia panda mizunguķo ya barabara unaoona roboti kadhaa zìkificha sura huku zimeshikilia gobori za kukuulì tembo🐘
 
Back
Top Bottom