Updates: Mkutano wa Zitto Kabwe Lindi

Updates: Mkutano wa Zitto Kabwe Lindi

Danny Massawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
1,299
Reaction score
765
Nitawapa updates kutoka Uwanja wa Ilulu Lindi.

Mpaka sasa 15:30 watu wanaingia uwanjani kwa uchache, Mkutano unatarajia kuanza saa 16:00

Uingiaji watu ni mdogo na inatokana na wananchi kitokupata taarifa ya uhakika

Vyombo vya kuongelea vinatestiwa Afande Sele atakuwepo pia

Mpaka sasa kuna watu takribani 1500

Mwenyekiti wa Jimbo la Mtama wa ACT ndio anaongea anawafundisha slogan ya act na anasemah ZZK anakaribia kufika.


Bado zzk hajafika wala afande selle

Imewekwa nyimbo inayomsifia kwa kupambana wkt wa opereshen tokomeza na escrow

Bado wenyeviti wa wilaya mbalimbali za mkoa wa Lindi wanaongea ....wanamsifu zzk kuwa ndio mkombozi ccm cuf na chadema wameshindwa

Kweli act wanakazi maana hawa viongozi wa wilaya hawawezi kuongea inaelekea hawana uzoefu inabidi wajengewe uwezo sana

Hakuna zomea yyt iliyotokea...
Ila hakuna maana kinachoendelea watu wana msubiri kiongozi mh zzk

Zzk bado hajafika

Ndio zzk anaingia msafara wake umeanza na bodaboda kama 30 hv na magari mawili aina ya land cruiser

Moja yupo zzk ingine afande selle

Watanzania wanaopenda democrasia wamsapot zzk na act maana hata magari yao yamechoka vyombo vya mziki navyo vinasuasua

Bado hawajaanza mike zinazingua

Bodaboda wamelipwa na wameondoka

Mike zimekubali na mjumbe wa kamati kuu MAMA TERRY anongea....mike zimezingua tena

kidogo mama anajua kuamasisha anachangamsha kidogo

Anashukuru watu kihudhiria

MAMA TERRY anasema act italeta amani na usawa....anasema ni chama cha wanyonge tikichahue ili watatue matatizo

Mama ansema wataboresha sekta ya afya na elimu

Mama anasema tatizo la nchi yetu ni kichagua viongozi wabovu....anasema tisiwapigie kura mafisadi

Afande selle amepanda jikwaani kuongea

Anasema amejufunzia maisha Lindi

Anasema atakuwa mbunge wa kwanza mwenye rasta bungeni

Afande anasema kuwa atagombea ubunge moro..

Wanamsifu mbunge wa Lindi mh Barwani..

Anasema Lindi kwanza na chama baadae

Anasema act hawaitani waheshimiwa Bali wanaitana NDUGU

Ndg zzk anapanda jikwaani

Anasema ni Mara ya kwanza kifanya Mkutano Lindi

Anasema ameitetea sana Lindi na mtwara bungeni

Ansema mikoa hii iko nyuma kimaendeleo

Anasema mungu ametupa utajiri wa gesi ila kuna watu wanawanyonya watu wa Lindi na mtwara

Zzk anasema sheria za gesi zote ni mbovu kwa sababu hazikushirikisha wananchi

Tusikubali kuwa maskini wakati tuna utajiri

Tuwaambie viongozi wetu hatutak kunyonywa

Anaelezea azimio la tabora

Anasema kansa ya nchi ni ufisadi

Anasema inabidi kuwe na sheria Kali na miiko ya viongozi

Kwenye azimio la tabora Luna miiko ya viongozi

Hakuna kuchanganya uongoz wa uma na biashara

Anasema watangaza nia wa ccm wote ni wala rushwa na kila mmoja

Anasema lowassa ajieleze kihusu Richmond

Mwandosya aliharibu pia

Magufil amekula ela ua mabehewa

Membe aeleze juu ya ela za gadafi

Zzk anaendelea watangaza nia wamekuwa serikalin na wameshindwa na hawafai

Anakemea udini na ukabila

Anasema wanarejesha modernised azimio la arusha

Anasema amefukuzwa chadema ndio maana ameunda act

Wanamsifu lipumba anasema ni mwalimu wake na anamuheshimu
Anasema act wanasiasa safi hakuna matusi
Anasema ameleta chama na tuamue wenywe

AMEMALIZA
 
Mkuu huyu mkuu ZZK kishafika au bado ananusa upepo na kumtanguliza mwenyekiti kama kawa ?
 
Mcubic njoo ndugu yangu watu wanaingia kwa uchache huku. natarajia picha itapigwa kwenye kachochoro kenye majengo na watu wapo chobingo hammudu viwanja
 
ni upuuzi kulinganisha chama kilichoanza tangu 1992 na chama kisichozidi umri hata wa miaka miwili
 
Act chama imara kilichoonyesha mwelekeo wa kweli ktk ukombozi wa Tanzania
 
Taratibu Naanza kukikubali hiki chama,Kina siasa za amani na utulivu sio ile saccos ya wachaga wao bila vurugu na umwagaji damu hawaendi
 
Zomea inadharirisha bavicha kuwa hawajiamini.
 
Back
Top Bottom