Updates Kutoka kwenye show kali ya LOVE, MELODIES and LIGHTS.

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,148
3,861
Habarini za wikiend wadau.

Kama mnavyojua tena leo ndio ule usiku mubashara usiku wa shoo kali ya kiaina yake na ya kipekee shoo ya karne. LOVE, MELODIES and LIGHTS

Kwa wale wa mjini mnaosikiliza hii redio ya Wafu aaah sory, i mean redio ya Watu clouds FM. Mtakuwa mnajua kuwa leo mkali Ben pol, jux na Baraka da prince watakuwa jukwaa moja wakisindikiza usiku huu wa kipekee kabisa.

Katika shoo hii ambayo kulikuwa na kiingilio mpaka milioni na zaidi lakini ticket ziliwahi kuisha sio mchezo kabisa.

Mwenye updates za huko tafadhali mambo yanavyoenda atuambie. Mambo yamenoga au hayajanoga? Maana clouds ni mabingwa wa kupiga promo halafu unakuja kukuta ni upuuzi tu. Kama ilivyokuwaga Fiesta.

Pia sipatii picha hawa akina Ben Pol maskini watakavyokuwa wamenyonywa kwenye malipo ukilinganisha na faida itakayokuwa imepatikana.

Picha za eneo la tukio kwa hisani ya clouds ni kama zifatazo. Jinsi mambo yatakavyokuwa kwenye maturubai hayo.

80563f83805b84920239b3d2c896a846.jpg

b572f82e508936685bc2840d11b51f8c.jpg

Huo ndio muonekano wa ndani mambo ya Lights hayo

4681de7c823a67dbca6c913eb883aab7.jpg

272990ea2a434e974cbaf6b73bc9a89c.jpg

Hii ndio Red Carpet ya kimataifa. According to wao..

SASA JAMANI ALIYEKO HUKO ATUPE UPDATES TAFADHALI...

UPDATES PLEASE..
 
Huwa sipendi zile nyimbo zao za kawaida wanavyozibadili kuwa za slow!
mfano Baraka akiimba siwezi anavyoivuta utatamani uondoke ukumbini
Nina uhakika leo hakuna watakachofanya. Ni mwendo wa kuboronga tu.. ngoja tusubirie tuone lakini
 
Tatizo la wasanii wetu wanafikiri kuimba live ni kubadilisha tone na melody ya wimbo na hicho ndio hukera kwenye show live za kibongo....Niliona Ditto anaimba wimbo wake wa moyo sukuma damu kwakweli ni utumbo mtupu.
 
Wote mmenyuti hamna tu huku kwenye ubavu wakutoa milioni,ingekuwa ni press conference wangeshajileta, tena wengine wangeanza kupost wakiwa ndani ya mwendo kasi wakielekea huko. Hapaleo mkombozi ni le mbebezz tu , natumahi hatokosa kwakuwa ni super bilionea milioni kwake si pesani mubashara tu.
 
nikajua niko peke yangu mkuu! huwa nakereka sana hiyo tabia
 
Yote hii ni kutolewa povu na EFM
Hakuna siku efm wameweka shoo na hawa jamaa wasiweke
 
Tatizo la wasanii wetu wanafikiri kuimba live ni kubadilisha tone na melody ya wimbo na hicho ndio hukera kwenye show live za kibongo....Niliona Ditto anaimba wimbo wake wa moyo sukuma damu kwakweli ni utumbo mtupu.
Mkuu kile kilikuwa kituko. Mimi kwa kweli kwa usalama wangu siangaliagi live za kibongo flava tu
 
Ushasema una uhakika unasubiri kuona nini zaidi?!

Juma Nature aliwahi kuimba "Unakubali kuungua na JUA kwa ushabiki ulio na kinyongo"
Nasibiria muujiza. Kama unavyojua. Ya mungu mengi
 
Wote mmenyuti hamna tu huku kwenye ubavu wakutoa milioni,ingekuwa ni press conference wangeshajileta, tena wengine wangeanza kupost wakiwa ndani ya mwendo kasi wakielekea huko. Hapaleo mkombozi ni le mbebezz tu , natumahi hatokosa kwakuwa ni super bilionea milioni kwake si pesani mubashara tu.
82e9ec5108856a8d432d3243d921921f.jpg

Ameshafika tayari. Hiyo picha aliposti kuwa hatakosa leo.

Huyu mzee hivi ana umri gani?
 
Back
Top Bottom