Ungeuliza "Twende Kilioni" ni nini kama hujui, sio kufanya kile watu wa Mombasa wanachoita "kudandia kishazi m.atako wazi"...
Umeambiwa ufuate masharti kwa vitu usivyo asili navyo, au na Twende Kilioni ni kutoka Bara Ulaya?!
Kwanza nikueleweshe kuwa chochote kinachofanywa na Chadema, CCM, CUF, NCCR au chama chengine chochote cha kisiasa ni "my business" kwa mujibu wa sheria za nchi hii huru ya Tanzania.
Mbali ya katiba ya nchi kutoa haki ya opinion, jukwaa hili lipo hapa mahsusi kwa kazi hiyo.
Watanzania mnalilia demokrasia na utawala wa haki na sheria lakini hamuwezi ku-tolerate mtu kusema tu kuwa mavazi ya chama yanapingana na taratibu na heshima za uvaaji cap.
Si mkipata nchi mtataka kutupiga marufuku hata kupumua kwa sauti, ati ni kuonyesha kukimwa?
Na kwa Chadema kuwa na washabiki wa aina yako, ni kuiaibisha tu kuwa haiwezi kusikiliza mawazo tofauti hata kwa mambo madogo.
Aibu