Acha Uvivu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 525
- 131
Pinda apelekwe The Hague maana tayari kashaua watz wengi kwa kauli za ubabe na aliposahau umuhimu wa diplomasia katika kutatua migogoro.
wakuu naweka hii thread ili wale wote walioko kwenye eneo la tukio watupe updates za kikao cha majadiliano kati ya waziri mkuu na madaktari walio kwenye mgomo.nimepata habari hivi punde kuwa mh waziri Pinda ameshaingia hospitali ya taifa muhimbili...........more to come
updates;mapendekezo ya serikali
- inaelekea serikali inaratibu kila kitu,yaani meza kuu imeanadaliwa kwa ajili ya PM na wakuu wa wizara ya afya.
- yule hasimu wa mponda dr ulimboka stephene aka 'bwana ulimboka' yupo frontline kwenye kikao hiki.
- imepita dakika 51 baada ya muda uliopangwa kuanza kwa kikao lakini bado pinda hajaingia CPL,madaktari kwa upande wao wameijaza CPL ile mbaya.
- kuna taarifa kwamba madaktari bingwa na wafanyakazi wa MNH wamepewa viti vya mbele.sijui ile kamati imepewa nafasi gani?
- hatimaye mh Pinda na ujumbe wake wameingia CPL ni saa 9:54 asubuhi
updates
- interns warudi muhimbili
- madaktari wapewe nyumba na green cards lakini hajasema kivipi
- call allowance kwa specialists iwe 25000
- call allowance kwa madaktari wa kawaida 20000
katibu mkuu na chief medical officer OUT!
mponda na Nkya watashughulikiwa na Rais!
Pinda mamlaka ya kumfukuza Nyoni kayapata wapi? kwa Jairo si alisema ni presidential appointee naye hana uwezo huo...?
Halafu eti anapumzishwa kufanya uchunguzi.. ni uchunguzi gani wanaotaka kufanya jamani? mbona tunafanyana mazuzu namna hiii?
jk NI KAMA MTOTO MDOGO,Hao walioachiwa JK awawajibishe yaani waziri na naibu wake, kwa historia ya Jk ilivyo hana ujasiri wa kuwawajibisha japokuwa ndie aliyewateua. Atakwepa kama alivyokwepa kutekeleza maazimio 23 ya Bunge na kusababisha mzozo ndani ya serikali usioisha. Kama huamini maneno yangu subiri ujionee mwenyewe.
.
Kauli za Huyu mtoto wa mkulima huwa hazina Mashiko, Kumbuka wakati wa Jairo alisema kama angelikuwa na uwezo angechukua hatua ila akamgojea mkuu wa Kaya, matokeo yake tunayajua mpaka jamaa kastaafu kwa heshima.
Sitaona ajabu Waziri na Naibu wake wanapewa heshima ya kuwa mabalozi kwenye nchi fulani.
Hii nchi yetu sijui nani alitupa ujasiri wa Kondoo kila wakati kuwa KAFARA.
Jambo lingine utujuze Huyu mtoto wa Mkulima anahutubia kwa staili ya MBWEMBWE au amekuwa na Nidhamu ya kawaida.
Pia Katibu Mkuu na Chief Medical watashtakiwa au nao wanapewa heshima kama Jairo? Amefafanua au anataka kupigiwa makofi tu? Hapa hatufanyi siasa wakati wenzetu wamepoteza maisha, naye amejiweka kundi lipi kwa jeuri aliyoonyesha awali?
Baada ya kukata viuno hapa na vidole juu ndio sasa unataka tujiulize?Labda tu nikujuze kidogo.
Kumbuka kuwa duniani kooote hospital za jeshi ndio hospital kuu na mara zote zinakuwa na kila kitu na wataalamu wengi sana na wenye uwezo mkubwa na zinakuwa ni za rufaa. Hata viongozi wa nchi wakiumwa mara zote wanatibiwa katika hospital za kijeshi kutokana na usalama na weledi wa maDr wao.
Nakumbuka hata Tz , Jeshi lilisomesha sana madaktari wake enzi hizo na kuiimarisha hospital yao ya lugalo.
Pasi na shaka yoyote huko Tz lugalo ni hospital ya rufaa pia kijeshi. Hakuna mtu anayeweza kupewa uhamisho toka lugalo kwenda muhimbili kwa matibabu zaidi.
Hata mgomo wa 2003 wa madaktari hao hao wa Lugalo walishika muhimbili na kuiendesha mpaka mgogoro ulipoisha
Chunguza hilo.
Mimi nashauri ni lazima waTz murejee katika mila na desturi zenu na kuachana na hizo za kizungu.
Nakumbuka toka zamani kulikuwa na kuto kuelewana kunakoweza kutokea katika jamii mbali mbali mfano wakti nipo Chuo kikuu UDSM tulikuwa tuna mogogoro mara kwa mara na chuo au na Serikali. Lakin mila zenu ilikuwa wanafunzi woote mnakusanyika pale Nkuruma hall na viongozi wanakuja na kukaa kitako kuanza kujadili matatizo yenu mpaka mnafikia kukubaliana na baadae mnarudi darasani.
Siku zote viongozi walikuwa wepesi kufika na kuongea na wanafunzi na kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano mezani na sio kuandamana.
naona sasa utamaduni huu huko Tz umepotea kabisa. Viongozi wanajiona ni miungu watu hawataki kabisa kuwasikiliza wanaowaongoza na kupenda kutumia ubabe katika kutatua migogoro.
hakika ubabe na ubinafsi ni sumu sana katika uongozi. Kiongozi kumbuka bila kuwa na unaowaongoza wewe huwezi kuwa kiongozi. Na mnaongozwa acheni lugha za kebehi na kashfa kwa viongozi wenu. Hishma ni muhimu sana na utii wa sharia zenu mlizojitungia.
Nawasihi tena waTz rudini kwenye mila na desturi zenu za kukaa kitako na kujadili matatizo yenu mezani na sio kwa kuandamana na kutusiana.
Loh naifananisha Barza ya JF sawa na Mzee Punch wa Udsm enzi hizo.