Update za mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Update za mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALEX PETER, Jun 26, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mgomo wa madaktari jijini Dar es Salaam umeanza kushika kasi ambapo katika baadhi ya hospitali ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wagonjwa walikosa huduma na kuishia kutangaziwa warejee nyumbani hadi watakapopata taarifa kuwa mgomo huo umeisha.

  Katika uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika hospitali za jijini hilo, umebaini kuwa mgomo huo umeshika kasi zaidi Muhimbili na Hospitali ya Amana ambako baadhi ya vitengo vya huduma za afya vilifungwa ili kuongeza nguvu ya madaktari katika vitengo vya dharura.

  Katika Hospitali ya Muhimbili, gazeti hili lilishuhudia wagonjwa wakiwa wamezagaa na kujazana hasa katika Kitengo cha Mifupa (MOI) huku wengine wakiwa wamekata tamaa ya kupatiwa huduma.

  Gazeti hili lilishuhudia mmoja wa watoa huduma za kupokea wagonjwa akiwatangazia wagonjwa waliojazana katika eneo la mapokezi hospitalini hapo kuwa waondoke hadi watakaposikia mgomo umeisha kwa kuwa sasa hakuna huduma yoyote.

  “Mimi mtoto wangu ana matatizo ya kichwa kuwa kikubwa leo tulitakiwa kuja kuonana na daktari, lakini tangu asubuhi nimefika hapa nimekuta umati mkubwa wa watu wakilalamika kukosa huduma, hadi tulipotangaziwa kuwa tuondoke hakuna huduma,” alisema mkazi wa Morogoro, Martha Said.

  Naye Khalfan Juma mkazi wa Kigogo alisema anasumbuliwa na miguu na amefika hospitalini hapo tangu asubuhi lakini hakupatiwa huduma yoyote kwani daktari aliyekuwapo ni mmoja wa watoto na hadi kufikia saa tano mchana alisitisha naye huduma.

  Katika maeneo ya wodi za hospitali hiyo, hali ilikuwa mbaya kwa kuwa wagonjwa walilalamika kutopata huduma yoyote ya matibabu zaidi ya madaktari na wauguzi kuwapitia na kuwaulizia hali tu huku wauguzi wengine wakitoa lugha za kashfa.

  HabariLeo ilijaribu kuwatafuta wasemaji wa hospitali hiyo ambao ni Jezza Waziri na Almas Juma bila mafanikio kwa kuwa ofisi zao zilikuwa zimefungwa huku kukiwa na ulinzi mkali wa askari ambao waliishia kugombana na waandishi wa habari.

  Kwa upande wa Hospitali ya Amana hali haikuwa nzuri kwa kuwa kulikuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa huku madaktari wakiwa wachache hali iliyosababisha huduma kudorora kwa wagonjwa wa nje na ndani.

  Mmoja wa maofisa wakuu hospitalini hapo aliyekataa jina lake kutajwa gazetini kwa kuwa si msemaji, alilihakikishia gazeti hili kuwa mgomo wa madaktari upo kwa kuwa madaktari wengi wa hospitali hiyo jana hawakufika kazini na kusababisha baadhi ya vitengo kufungwa.

  “Tumeamua kufunga vitengo vya kliniki kwa akinamama kutokana na upungufu wa madaktari waliofika kazini leo ili kufidia maeneo mengine ya dharura na huduma zinaendelea ingawa ni kwa kusuasua,” alisema Ofisa huyo.

  Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti katika hospitali za Mwananyamala na Temeke ambako gazeti hili lilishuhudia madaktari wake wakiendelea na kazi bila dalili yoyote ya mgomo.

  Easther Sufian, mkazi wa Tandika alithibitisha ndugu yake kupatiwa huduma katika Hospitali ya Temeke huku akikiri kuwa na hofu wakati wakienda hospitalini hapo ya kukosa huduma.

  Lakini pia gazeti hili katika Hospitali ya Mwananyamala lilishuhudia wagonjwa wakitibiwa. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dk Amaan Malima, alisema hali ya hospitalini hapo ni shwari na hakuna mgomo kwa kuwa madaktari wote wameripoti kazini na amewashuhudia wakiendelea na kazi.

  Kwa upande wake Katibu wa Hospitali ya Mwananyamala Edwin Bisakala, alisema kazi zinaendelea kama kawaida hospitalini hapo hakuna daktari wala muuguzi ambaye hayuko kazini kwa sababu ya mgomo
   
 2. j

  jigoku JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hilo gazeti sina imani nalo,maana taarifa nilizo nazo kutoka kwa daktari ambae ni mtu wangu wa karibu sana anasema hali ni mbaya sana katika hospitali zote za DAR,isipokuwa Temeke kuna madaktari 3 ndio waliokuwa wanaedelea na kazi,mikoani kama vile Dodoma,KCMC,Bugando na Mbeya mwendo ni ule ule.kinachoonekana hapa ni vyombo vya habari kufanya propaganda na kuandika vitu wasivyovijua,wakikuta watu wamevaa koti jeupe wanajua ni madaktari,iko hivi wanaoendelea na kazi ni ma-AMO.madaktari wako kwenye mgomo,tusemeni ukweli badala ya kuudanganya umma.na wao wanasema ngoma hii wanaipiga kimya kimya,na wanawasilana zaidi kupitia forum yao ya MAT.ambayo kui-visit mpaka uwe member na ina password,na kuwa member ni mpaka uwe daktari.ukiingia huko ndio utaona wanavyopeana habari.
  Mgomo upo na wacha uendelee kuwepo.
   
 3. O

  Online Brigade Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mkulu dhaifu, wananchi twataabika. Nimeangalia taarifa ya jana ITV, wengi waliohojiwa wamesema hawajapata huduma. Hali hii mpaka lini na mwenye nchi keshakwea pipa. Naamini kabisa suala hili lingeweza maliza kikubwa kabisa, tatizo watendaji wamegubikwa na siasa na hawataki kukubali ukweli.
   
 4. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,297
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  naishi maeneo haya ya muhimbili,mgomo upo na unaendelea,ila kinachoonekana baadhi ya vyombo vya habari vimepigwa marufuku na serikali kitangaza hali halisi
   
 5. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,084
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  Kuna mgonjwa mmoja ktk gazeti anaumwa jino SIJUI HAKUJUA MaDr. wamegoma... Badala ya kung'oa jino bovu Dr. wa zahanati kamng'oa meno 3 mazima.... nadhani mgomo unaanza kulipizia wagonjwa.... kaaahh
   
 6. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hii ni kuwaumiza Watanzania wanaopoteza maisha kila kukicha, pia ni haki ya Daktari aliesoma miaka 7 kua hapo alipo kulipwa vizuri. Hii ni dedication of their life to live that way to save us plz wasikilizwe.
   
 7. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  mficha uchi hazai, mficha ugonjwa....!
   
 8. e

  ellyjr8 Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
  Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu"SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
  HALI HALISI HOSPITALINI:
  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
  Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
  1. Madai ya madaktari yalianza lini?
  2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
  3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
  4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
  5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

  SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
  Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

  VYOMBO VYA HABARI:
  Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
  Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
  Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
  Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
  MKAKATI:
  Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
  1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
  2. Wanatumia pesa ya nani?
  3. Last‘episode" walileta wanajeshi,
  KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
  KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

  MAKOLIGI (colleague)??
  Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
  Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government's responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
  ..Solidarityforever..
   
Loading...