HII bei ilitarajiwa tu na itaendelea kushuka kulingana na mzigo ulivyokuwa mwingi kweny warehouse na Kwa wakulima ndio kwanza hujatoka tunaweza funga msimu na bei za 2000+ Kwa uzoefu wangu
HII bei ilitarajiwa tu na itaendelea kushuka kulingana na mzigo ulivyokuwa mwingi kweny warehouse na Kwa wakulima ndio kwanza hujatoka tunaweza funga msimu na bei za 2000+ Kwa uzoefu wangu
Wakulima wa zao la korosho wa Tandahimba na Newala kupitia chama kikuu Cha ushirika Tanecu Ltd wameuza korosho zao kwa bei ya juu ya sh 3430 na bei ya chini ya sh .3200 katika mnada wa tatu wa zao Hilo uliofanyika Leo October 25 2024 katika ukumbi wa zamani wa halmashauri ya wilaya ya Newala uliopo halmashauri ya mji Newala
Akitangaza bei hizo mwenyekiti wa Tanecu Ltd Karim Chipola amesema wao kama wasimamizi wa mkulima watahakikisha korosho zote zinazopelekwa ghalani zinauzwa hivyo amewataka wakulima kuzikausha vizuri korosho zao ili ziendelee kuwa Bora zaidi
Mnada huo umeendeshwa kwa mfumo wa mtandao unaosimamiwa na TMX ambapo korosho tani 19000 na kilo 73120 katika mnada huo zimeuzwa
Kwa upande wao wakulima walioshiriki mnada huo wamesema wanaridhishwa na bei hizo
Tunataka kuona wakulima wakiendesha V8
Mbona miaka ya nyuma wakulima walikuwa na Peugeot na Land Rover?
Wakulima wa sasa wananyonywa haswa
Labda tutaona mabadiliko kwenye kilimo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.