Upasuaji wa kwanza wafanyika duniani bila ya Daktari

Upasuaji wa kwanza wafanyika duniani bila ya Daktari

Kikokotoo tu ni shida, sembuse hii teknolojia!!!

Tanzania kila kitu tunashika
Wenzetu wanajitahidi kushika kitu kimoja,
India wanewekeza sana kwenye Elimu hasa ya science
 
Kwa maisha tunayoishi?

Inabidi Vitoweke vizazi vyetu complete
Walau watakuja wanaofikiria vizuri
We unaambiwa mwanadamu wa kwanza aliishi Olduvai Gorge; yaani Mbongo Pyua!! Wakati jamaa waliwepo hapo miaka milioni kadhaa iliyopita; sisi kizazi chake kilichokuja miaka milioni kadhaa baadae ndo kwanza ukiwa na cherehani 2 unaambiwa una kiwanda!!
 
Majaribio kama haya yaendelee kufanyika kwenye nchi hizohizo zenye idadi kubwa ya vichwa vya binadamu.
Bado tupo kwenye kikokotozi kinatutoa jasho je huko tutafika?

Wasomi wetu waliotakiwa wawe maabara ndiyo kwanza wapo magate ya ofisi za vyama vya kisiasa wanapigana vikumbo vya kupata nafasi za kugombea
 
Walete tu hayo marobot wayasambaze kwenye vijji vyetu ni jambo zuri kwakweli. Sio tunahangaika kuwasomesha madaktari alafu wanafeli bila kulipa mikopo yao
 
We unaambiwa mwanadamu wa kwanza aliishi Olduvai Gorge; yaani Mbongo Pyua!! Wakati jamaa waliwepo hapo miaka milioni kadhaa iliyopita; sisi kizazi chake kilichokuja miaka miloini kadhaa baadae ndo kwanza ukiwa na cherehani 2 unaambiwa una kiwanda!!

Nimecheka kama mazuri vile
 
Mhindi kamzidi mzungu mmmh naamini kagundua mzungu ila machine kazifunga India

teknolojia Hii haiwezi kukosekana New York ikapatikana ahamabad huko
Utaelewa tu.
Wazungu wanavyopenda sifa waache kufunga kwanza mashine hizo kwao waende kufunga ugenini?
Unawachukuliaje Wabhaharat? kama wabongo wenzio?
 
Ni jambo zuri sana ninachokiona tunakokwenda ni dokta yuko Bara jingine anafanya upasuaji mgonjwa yuko Bara jingine na baadae Robot pekee ndio zitakua zinafanya shughuli
 
Nchi zetu shida sio vichwa shida ni njaa, tugange njaa ikipungua hivyo vichwa automatically vitaonekana tu, hiv unafikiri kutengeneza hilo robot mpaka kufika hapo ni sh. Ngapi je kichwan ukiwa na wazo lakufanya hicho kitu sio rahisi kukata tamaa hata kabla hujaanza? Kwasasa tugange njaa kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maana yangu mimi ni idadi kubwa ya watu na sio akili
 
Back
Top Bottom