Upasuaji MOI sasa kutumia mtambo wa kisasa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
SHIRIKA la Madaktari wa Afrika kwa kushirikiana na Taasisi ya Sign Group ya Marekani, yamekabidhi mashine ya upasuaji wa ubungo na mifupa, kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI).

Mashine hiyo yenye thamania ya Dola 144,000 za Marekani, ilikabidhiwa jana katika hafla fupi iliyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Blandina Nyoni.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa madaktari kutoka Marekani, Karen Marchrn, alisema msaada huo umetokana na uhusiano nzuri uliopo kati ya wataalamu wa Tanzania na Marekani.

"Tumefarijika sana, awali tulipokuja Tanzania kama kutalii, tuliamua kutembelea hospitali mbalimbali ili kubadilishana ujuzi wa tiba na wenzetu na tulipewa ushirikiano sana,"alisema

Alisema katika ziara hiyo, walishuhudia matatizo yanayowakabili wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji ukiwemo wa mifupa, jambo lililowasukuma kuleta mchango wa mashine ya kisasa iitakayowasaidia madaktari katika kuwatibu wagonjwa hao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili, Profesa Joseph Kahamba alisema mashine hiyo ni ya kwanza kwa shughuli za upasuaji katika hospitali zinazotoa huduma za upasuaji hapa nchini.

Alisema mashine hiyo inatumia upepo, kukusaidia kufungua ubungo na uti wa mgongo.

"Mashine zote tulizokuwa tukizipata huko nyuma, zilikuwa na kutumia umeme, lakini hii ni ya kisasa zaidi," alisema Profesa Kihamba.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,(Nyoni) alisema msaada huo utaipunguzia serikali gharama za kusafirisha wagonjwa kwenda nchi za nje kufanyiwa upasuaji.

Chanzo: Upasuaji MOI sasa kutumia mtambo wa kisasa
 
Haya nyie wapika majungu mnaona kazi ya huyu mama Nyoni toka amekuwa katibu mkuu wizara ya Afya? Acheni majungu mpeni sjfa mtu kwa utendaji wake kazi. Kabla ya mama huyu kufika pale wagonjwa wa kupelekwa nje walikuwa wananyanyaswa sana na maofisa waliohusika na kuwatayarishia safar,i lakini sasa mambo ameyasawazisha hakuna tena upuuzi huo.
 
Back
Top Bottom