Upanuzi wa barabara Mwanza

Upanuzi wa barabara Mwanza

Enzymes

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
4,332
Reaction score
3,018
Jameni Watanzania wote tu mashahidi wa kazi nzr za Mhe: Dr. John Pombe Magufuli nchi nzima. Big up mheshimiwa.

Licha ya kazi yako nzr kuna mapungufu madogo madogo ya kiutendaji au ya kiubinadamu- kwani wanadamu wote hatuko 100% perfect!

Jam aka msongamano wa Jiji la Dsm nilidhani ingekuwa ni fundisho tosha kwa Wizara yako, Wizara ya Ardhi (Mipango miji na makazi) na TAMISEMI kwa ujumla. Ama kweli hii Tanzania, mambo yako tofauti kabisa na udhaniavyo!

Nadhani Jam hii ingekuwa chachu ya kupangilia miji kama Mwanza, Arusha, Mbeya na hata Tanga.

Jiji la Mwanza lina barabara kuu 2! Mwanza-Shinyanga na Mwanza-Musoma. Maajabu ya Jiji hili ni upanuzi unao endelea kufanyika. Ni wa ajabu sijawahi kuona duniani ktk karne hii ya 21!

Mwz-Musoma-wanapunua njia3 , kwa baadhi ya maeneo tu na si kote. Hivyo hupanua kwa kuruka ruka! Yaani ni viraka hata sielewi inatoka wapi inaenda wapi! Hivyo ni vigumu kwa dereva kuja na njia ya 3 gafla, njia ikakoma na kulazimika kuunga njia2. Hapa kuna uwezekano wa kujitakia ajali nyingi za kutosha! Na kuishia kuwalaumu madereva bure!

Kwa Jiji kama Mwz kuwa na barabara kuu 2 tu ni ufinyu wa kufikiri kwa TANROADS na Wizara yako kwa ujumla. Hata kama zingekuwa 2 ni bora zingekuwa na njia 8 kila moja. Tatzo la TANROADS MWANZA wamekariri mkandarasi wa barabara kila sehemu NYANZA ROADS hata kama kazi zake ni za ajabu ajabu. Mfano pale Pamba Road, Pepsi, TANESCO, BUTIMBA CORNER, nk

Pale MISSION wanajenga soko la kimataifa. Parking hamna! Kuna Jam kila siku hata kabla ya soko kufunguliwa! Je likifunguliwa hali itakuweje? Soko lenyewe ni ONE direction-magari yote pale.

Maoni:
1. TANROADS na Wizara ya Ardhi mkae chini bunini barabara nyingi mpya ingali fidia ikiwa nafuu.

2. Ujenzi wa barabara si kurundika kokoto au zege na Cement njiani! Zoezi hili linahitaji utaalam wa hali ya juu. Mnaweka matuta barabarani utadhani mñakinga maji! Mf. Barabara ya Mwanza-Malimbe SAUT. Tumieni wataalam.

3. Hizi barabara 3 mnazojenga haziwajali watembea kwa miguu! Hivi watanzania wote wana uwezo wa kumiliki magari? Tumieni mfano wa barabara ya Mwanza-Airport (Nela). Nadhini hii ilijengwa na mzungu. Watanzania tusijifanye wehu wakati akili tunazo!
4. Mpango wa njia 8 uanze mapema. Kama takwimu za Mhe: Mbowe ziko sahihi , za magari 300, 000 huingizwa kwa wiki( sina uhakika sana). Hali itakuwa mbaya sana Tanzania iwàpo hatuna mipango ya kukabiliana na ongezeko hili.

5. Kama ningekuwa Waziri wa Ujenzi au wa Ardhi watendaji wasio wabunifu ningefukuza kazi wote! Jam, na migogoro ya ardhi chanzo ni wao. Macho yote kupiga hela tu. Hivi ni kwani tu act baada ya tatzo? Mfano: Mafuriko ya Dar na ujenzi wa mtaro!

6. Karne hii ya 21 hatuitaji Roundabout za taa au magari kusubiliana. Ni moja ya sababu za Jams Dar. Ziwe pana na moja kwa moja ether juu au chini.

7. Watanzania na walipa kodi wote hatutaki utitiri wa barabara! Bali barabara zenye viwango sahihi na matumizi sahihi. Kuna barabara Ipo Musoma-Tarime ina miaka 10+ ni imara kuliko za Dr. Magufuli za mwaka 2012!

Ni ushauri tu mkipenda muutumie, msipopenda muuache.
 
Enzymes

Umenena mkuu, yaan mwanza inakoenda, yetu macho, na hivi mwanza hakuna alternative roads, ni majanga matupu!
 
Last edited by a moderator:
Kusema mwanza ina barabara kuu 2 ni uongo ziko 3, kusema pale mission lile soko halina parking ni uongo, ile mall ina parking 600
 
kusema mwanza ina barabara kuu 2 ni uongo ziko 3, kusema pale mission lile soko halina parking ni uongo, ile mall ina parking 600

Hata hizo 3 zinatosha? nimezaliwa na kukulia Mza hapo Nera, kila nikija Mza baada ya miaka kadhaa nakuta mabadiliko hasa kuanza kutokea kwa traffic jam lkn barabara hasa highway zitashindwa kuhimili mzigo.

Hapo kwenye mall mpya huwa kuna foleni kubwa asbh na jioni, pale mabatini palikuwa kimeo sijui kwa sasa! Angalau wangeanza kujenga highways za njia 4, hiyo barabara ya Musoma, ya kwenda Airport na ya Shy.

Jana huku DSM ilifungwa highway ya Mandela sababu ya ajali. Ilikuwa shughuli pevu kutoka TMK kwenda Ilala na K'ndoni. Watu walifika makwao saa 8 usiku. Mwanza wajifunze hapo.
 
Enzymes

Kaombe kazi uwe engeneer maana naona consultant sijui wa nini vileeeeeeeee.......
 
Last edited by a moderator:
Ww hujitambui eti lile jengo halina parking?!!! huijui mwanza vizuri ww,hujui barabara za mawe za kupita bugando?!! hujui barabara ya kupita pansians ukielekea nyakato?!! Miundo mbinu mwanza iko vizuri sana dakika 20 uko twn! shika nani yako ww tena ,watu tunakula bia diamond kona ya bwiru kila siku bda ya dk 20 tuko home bukumbi
 
Nahisi ufinyu wa barabara mwanza ni sababu ya ziwa na miamba mingi kwa maneno mengine ni natural disadvantage kwa hili jiji.

Upanuzi wa njia ya igoma ulilenga zile sehemu ambazo zilikua korofi kwa jam(kutoka lango mpaka maeneo ya national) na kwa kiasi fulani wamefanikiwa ukiangalia pia kituo cha buzuruga kilikua kinaleta jam sana jioni sababu ya hiace kujaa pande zote na kubana njia na tayari kimehamishwa.
 
kusema mwanza ina barabara kuu 2 ni uongo ziko 3, kusema pale mission lile soko halina parking ni uongo, ile mall ina parking 600

Ya tatu ni ipi? Si uitaje hapa! Inatoka wapi na inaenda wapi?

Kwa sasa tu pale Mission japo soko halijafunguliwa kuna Jam toka saa 9 jioni hadi saa2 usiku. Na barabara ni ya gari 2!

Una data au una ongea tu? Jambo zuri ni kutumia ardhi yetu vzr. Mfano ghorofa zote hapa mjini- ili ramani ipitishwe wangewaambia wawe na underground parking.

Ghorofa zote za Mwz magari yote hupaki nje ya majengo! Hii hupunguza barabara ya gari 2 na kubaki ya gari1. Wao ni kwenda juu tu bila kutumia ardhi ya chini vzr!

Nairobi Supermarkets kubwa karibu zote zina underground parking.

Tatizo hili si langu tu hata ww ndg!
 
ww hujitambui eti lile jengo halina parking?!!! huijui mwanza vizuri ww,hujui barabara za mawe za kupita bugando?!! hujui barabara ya kupita pansians ukielekea nyakato?!! Miundo mbinu mwanza iko vizuri sana dakika 20 uko twn! shika nani yako ww tena ,watu tunakula bia diamond kona ya bwiru kila siku bda ya dk 20 tuko home bukumbi

Utakuwa na akili za vijijini! Hujawahi kutembea majiji makubwa na kujionea barabara kubwa na nzr!!

Yaani barabara ya Mawe ya Bugando yenyewe ni ya njia 1, magari mawili kupishana ni issue. Gari moja likiharibika katikati wote hampiti!

Pia hutumika tu iwapo kuna Jam pepsi.
 
Enzymes

mkuu pokea pongezi kwa uzi mzuri! ile barabara ya Musoma -Tarime ilijengwa na kampun ya kiitaliano ijulikanayo kama "kojfa " haijawai hata kuchubuka! hiz za kichina na wazee wa 10% ndio zenye matatizo!!
 
Last edited by a moderator:
Hata hizo 3 zinatosha? nimezaliwa na kukulia Mza hapo Nera, kila nikija Mza baada ya miaka kadhaa nakuta mabadiliko hasa kuanza kutokea kwa traffic jam lkn barabara hasa highway zitashindwa kuhimili mzigo.

Hapo kwenye mall mpya huwa kuna foleni kubwa asbh na jioni, pale mabatini palikuwa kimeo sijui kwa sasa! Angalau wangeanza kujenga highways za njia 4, hiyo barabara ya Musoma, ya kwenda Airport na ya Shy.

Jana huku DSM ilifungwa highway ya Mandela sababu ya ajali. Ilikuwa shughuli pevu kutoka TMK kwenda Ilala na K'ndoni. Watu walifika makwao saa 8 usiku. Mwanza wajifunze hapo.

Mkuu pale mabatini kwa sasa hamna Jam. Jam ilikuwa inasabishwa na wavuka kwa miguu (kwa sasa kuna daraja kubwa la juu kwa juu).
Kwa sasa Jam imehamia Buzuruga Stand (Kona ya Mecco na barabara iendayo Nyakato-hapa ni lazima Traffic awepo nyakati za jioni na filimbi).
Hii barabara ya njia 3 inayo jengwa hajaainisha ni njinsi gani watembea kwa miguu watavuka!

Tatzo hapa kuna watu wanaifikiria Mwanza kama kijiji! Tunahitaji barabara za kukidhi mahitaji 50-100 years to come.
 
Mkuu pale mabatini kwa sasa hamna Jam. Jam ilikuwa inasabishwa na wavuka kwa miguu (kwa sasa kuna daraja kubwa la juu kwa juu).
Kwa sasa Jam imehamia Buzuruga Stand (Kona ya Mecco na barabara iendayo Nyakato-hapa ni lazima Traffic awepo nyakati za jioni na filimbi).
Hii barabara ya njia 3 inayo jengwa hajaainisha ni njinsi gani watembea kwa miguu watavuka!

Tatzo hapa kuna watu wanaifikiria Mwanza kama kijiji! Tunahitaji barabara za kukidhi mahitaji 50-100 years to come.

Nilifika hapo mwaka jana, maeneo ya Nyakato shule (kama unaenda Mecco), nikashangaa sana kuwepo kituo cha daladala Buzuruga na stand ya mabasi kwa mbele kdg, jam kubwa. Watu wa mipango miji sijui wapo wapi. Hizo njia 3 wangeweka angalau mabango yanayoonesha ni muda upi upande upi utatumia njia 2 nyingine 1.
 
Foleni zingine mwanza ni za makusudi tu, waendao aiport/pasiansi walikua hawana haja ya kupita katikati ya mji wakitokea igoma.
Mimi nina miez 2 tu hapa mwanza lakini shughul zangu ni mitaani, so i know all the roads in mwanza. Believe me kuna jam kubwa sana inakuja barabara ya nyegezi/buhongwa to town....sioni alternative give me one to two yrs to prove this.

Barabara matuta mengi sijawahi kuona....hiyo ya malimbe ndio worse. Worse zaidi matuta yalijengwa baada ya barabara na nadhani na mkandarasi tofauti. Yanaumiza gari sana. Ule mlima kitonga njia ya iringa mbona hauna matuta kuna haja gani ya matuta njia ya SAUT?

Matuta ni tatizo kanda ya ziwa yote nadhani, tazama njia ya mwanza-shinyanga-nzega-singida-dom yaani matuta tuuu tuuu nilikua sijawahi kupita huku ni shida. Bora kubook flight ni mateso kupanda gari.
Mwanza itakua na jam kama za dar soon.
 
Hivi ww unakaa wapi? huzioni barabara mwanza? usagala-fela-kisesa iko hatua za mwisho, kwel ww mgeni. au ndo kumchafua kutangaza nia?

Ww ndio unafikiria siasa! Wengine hapa hatuko kisisia.

Kama watanzania tutaendelea kufikiri ktk mtizamo kama wako huu, inatuhitaji miaka 1000 kujua hata jinsi ya kutengeneza Plug za magari/Generator.

Hiyo barabara ya Usagala-Kisesa ni gari zipi zinapita hapo kwa sasa?

Hata kama hiyo route itakuwa ya Lorry, nk. Je barabara ya Kisesa - Mwz ina ukubwa gani wa kutosha kuhimili magari ya Igoma-Buhongwa, Igoma-Airport, Igoma-Bwiru na Buhongwa - Kisesa, + Basi zote za Mwz-Tarime/Musoma/Magu/Bunda/Lamadi/Serengeti + Private Cars?
 
Enzymes

Tatizo wanapenda contractors wanaotender kwa hela ndogo matokeo yake ni magumashi site bora project iishe, zile barabare imara zote ktk inchi hii zilijengwa na Contractor wakizungu.

Wachina ndo wanaopewa kazi kwa bei ndogo nakujenga feki roads, life span ya barabara ni 10 years nakuendelea kabla yakufanyika repair yoyote,leo hii miaka mitano ni mingi utakuta wanafanya patching. ONDOA CCM 25 OCTOBER.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom