Upandishaji madaraja umeishia wapi?

Upandishaji madaraja umeishia wapi?

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Rais aliagiza watumishi takribani 59 elfu wapandishwe daraja kufikia mwezi wa 11 mwaka huu, na kuna barua ya katibu mkuu utumishi akiwaagiza maafisa utumishi warekebishe mishahara ya watu mwisho ilikuwa 30/11/2017,nilitegemea kuona mabadiliko yoyote kwenye mshahara wa mwezi wa 12 lakini hakuna nyongeza yoyote.
Mheshimiwa rais aliwadanganya watumishi.
 
Kama kila mwaka mnatoa hela mnawapa ccm , mnawekwa wasimamizi mkishirikia na ma ded mnaiba kura mnawapa ccm , kila hovu baya mnapanga na ccm mi naomba aendelee kuwanyoosha mpate akili na ubongo wenu uamke. Pambaaf sana nyie watu.
 
Ingekuwa nchi ya wenzetu rais angeshatakiwa kwa kudanganyA watumishi tena kwenye media,huoni Trump anajifanya anakuwa na maamuzi ya kwake lkn hakimu na wasaidizi wake huwa wanamgomea hadi sasa mambo yake yamekwama
 
Nilikuwa na mpango wa kusoma ili nipandishiwe mshahara lakin kwa hali hii.
Aaarghh! Siendi kusoma!
 
Kweli hii ni pole ya wote japo wengine wana mawazo mgando katika hili kwa kuwashambulia watumishi na kusahau faida zao. Mtumishi wa umma ni mteja mzuri sana wa wakulima wa aina zote, mamalishe, madaladala, wauza pombe, wenye maduka ya bidhaa na mavazi na niseme sekta zote za uuzalishaji zinamtegea mtumishi wa umma anunue bidhaa zake. Lakini wale wasio na uelewa wanawaponda na kuwatia hasira kwa uvumilivu wao huku wakizishangaa biashara zao zikiwadodea!
Ni kweli mkulu alilizungumza hili jambo mra mbili au tatu maeneo tofauti ila utekelezaji wake unasuasua kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa serikali. Kuweni na subira watumishi wetu huenda marekebisho yakaja kwenye salary ya January.
 
Rais aliagiza watumishi takribani 59 elfu wapandishwe daraja kufikia mwezi wa 11 mwaka huu, na kuna barua ya katibu mkuu utumishi akiwaagiza maafisa utumishi warekebishe mishahara ya watu mwisho ilikuwa 30/11/2017,nilitegemea kuona mabadiliko yoyote kwenye mshahara wa mwezi wa 12 lakini hakuna nyongeza yoyote.
Mheshimiwa rais aliwadanganya watumishi.
Kwani na wewe umo miongoni mwa watumishi 59 waliokusudiwa?
 
Back
Top Bottom