Upande wa pili wa kisa cha Mama Mjane aliyemlilia Rais Magufuli kuhusu kudhulumiwa Mirathi

Status
Not open for further replies.

kiumbe kipya

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
2,831
1,303
Wakuu, nimekutana na haya maelezo sehemu. Nikaona nije kushea hapa tukune vichwa.

Ni kuhusu sakata zima la yule Mama Mjane aliyemlilia Rais Magufuli na kudai anadhulumiwa mirathi na kutishiwa maisha na kunyimwa haki yake kisheria ambalo munakasha wake uliletwa hapa > Mama Mjane amlilia Rais Magufuli mbele ya Waziri wa Sheria

Tusome, tujadili kwa umakini pasi na kuharibu mwenendo wa suala zima.
=======

Hii kesi naijua kwa undani sana; wahusika wote nawafahamu.

Kwa kifupi, huyo mama anayelalamika hapo ni TAPELI wa kutupwa. Narudia ni TAPELI wa kutupwa. Mengi aliyosema hapo kwa Raisi ni uongo! Nimefurahi kuona raisi ameagiza uchunguzi ufanyike.

Hii ni kesi ya mirathi. Marehemu Mohamedi Shosi alikufa Oct 2012 na kuacha wake wawili na watoto watano kule Bombo Tanga. Na amewaachia nyumba kadhaa zaurithi lakini kubwa kabisa iko Arusha na ina thamani ya takriban Sh 1B.

Huyu mama anamuita Marehemu Mjomba na ni Wagunya wa Mombasa. Yeye ni Mkenya lakini Marehemu ni Mtanzania. Mama ana watoto wawili ambao mmoja ameza na Mganda na wapili kazaa na MEthiopia.. Alijaribu kuwapenyeza kwenye mirathi akidai kuwa ni watoto wa Marehemu Shosi lakini alipoambiwa ifanyike DNA akarudi nyuma na kudai kuwa alizaa na mtu mwingine lakini marehemu aliwakubali watoto wake, eti alisema kitanda hakizai haram!

Alipoulizwa kwahiyo miaka ishirini alivyo kuwa na marehemu waliishi wapi? Akajibu eti waliishi gesti miaka yote hiyo. Yeye mke halisi amewekwa gesti wale anaowaita vimada anaishi nao kwenye nyumba zake!

Halafu mwezi Dec 2016 Mahakama ya Tanga ilipata taarifa kuwa huyu mama aliolewa tena Singida. Wakambana maswali hapo mahakamani akakiri kuwa alikuwa na mume mwingine wakati huo huo anavyodai ni mke wa Marehemu Mohamed Shosi! Yeye ni nani kuolewa na wanaume watatu kwa wakati mmoja?

Mtoto wa Marehemu aliyepewa usimamizi wa mali na mahakam kihalali kabisa na familia yote imemchagua na kumkubali anaitwa Saburia Shosi. Huyu mama amesuka mpango wa kutaka kupora mali ya mjomba wake ili auze nyumba na kurudi kwao Mombasa na kuwaacha watoto wake bila chochote. Polisi na Mahakama za Tanga zimegundua hilo, ndio maana anazichukia ukisikiliza malalamiko yake.

Mama mzazi wa marehemu ni mzee laki bado yuko hai na akili zake tiamau anaishi Tanga. Polisi wamezungumza mama wa marehemu na anasema hamtambui huyu mama kama mke wa mtoto wake marehemu. Vyeti vya ndoa ni vya kughushi. Kwa mfano siku ambayo inadaiwa wameoana, Marehemu alikuwa Tanga anamzika mtoto wake wa kwanza ambaye alifariki siku hiyo. Ukitaka kukikubali hicho cheti cha ndoa ni lazima uamini kuwa alikwenda Dar kuoa badala ya kuzika mtoto wake. Halafu mashahidi wapo ambao walikuwa na marehemu kwenye mazishi ya mwanae kwahiyo hicho cheti cha ndoa ni cha kughushi.

Mahakamani wamekiangalia wakakitupila mbali -- ndio bifu yake hiyo kwakuwa anajua kesi hii ya mirathi atashindwa kwahiyo alichofanya ni desperation attempt kuomba raisi amhurumie. Umesikia mlolongo wa vigogo ambao eti wote hawataki kusikiliza. Kuanzia IGP, DPP, DCI, Jaji Mkuu, Polisi Tanga, Mahakama Tanga, Hospitali Bombo Tanga etc. Wote hawa wanamuonea au yeye ndie mwenye matatizo?

Kumbe huyu mama aliolewa Buguruni - imegundulika baada ya uchunguzi. Mwezi wa May 2012, huyu mama alikuwa ameshinda kesi ya mirathi ya mumewe (mume mwingine huyo) anaitwa Sefuali Mombo wa Buguruni. Yeye huyu mama aliomba usimamizi "kama mke halisi" wa marehemu Sefuali Mombo wa Buguruni na akashinda kesi ya mirathi akapewa usimamizi.

Hiyo ilikuwa May 2012. Ilipofika October 2012 ndipo Mohamed Shosi wa Tanga ambaye anamuita Mjomba alifariki baada ya kuugua kwa miezi takriban mitatu. Alikufa kwa Lukimia. Ndipo akajitokeza huyu mama kudai kuwa yeye ni mke halisi (tena) wa Mohamed Shosi kwahiyo akadai usimamizi wa mirathi baada ya kupora mirathi ya Buguruni miezi michache tu iliyopita.

Wakati anadai mirathi ya Tanga, ili kesi ya Buguruni ilikuwa haijulikani. Akatokea msichana mmoja ambaye anafaham utapeli wa huyu mama akailekeza familia Buguruni ambako wakapata ushahidi wote kuwa aliolewa na Sefuali Mombo na sio Mohamed Shosi kama alivyojibadilisha kwa kutaka kupora mirathi kutokana na thamani ya mirathi ya Tanga.

Tamaa imemponza mimi nahisi pia kutokana na vitendo vyake, akili yake sio timamu. Lazima ana kichaa kufanya anavyofanya. Uchunguzi ukikamilika itabidi akanyee debe!

Naweza kuandika gazeti zima kuhusu kesi hii kwa kuwa nawafaham wahusika. Ila itakuwa vizuri kama tutapata mwandishi wa gazeti akazungumze na familia ili wapate upande wa pili wa hii stori.

Kama kuna mwandishi wa gazeti anataka kuifuatilia stori hii naomba anitumie email. Nitampa contact zote na makabrasha na Mahakama yanayo thibitisha utapeli wa huyu mama. It will be a very good investigative journalism piece.

Nakuhakishieni tena kuwa huyu mama ni tapeli; kulialia kote huko ni geresha kutafuta sympathy ila ni tapeli wa kutupwa! Msimuonee huruma hata kidogo!!

Mkisikia ushahidi wa upande wa pili mtapata kichefuchefu.
======

Karibuni.
 
Yule mama kwa jinsi alivyoingia pale tu nilihisi tu dishi limecheza na si yeye halisi.... kawadhalilisha IGP, DCI, AG, na mahakama zote kwa ujumla....anapaswa kuchukuliwa hatua ambazo zitakua mfano kwa wapiga dili wenzake... Nashukuru Rais alitumia busara, na IGP akafunguka kibusara pia
 
Kama ni tapeli imekula kwake.Rais sio anaeamua kesi japo anajaribu kuelekeza mahakama lkn mwisho wa siku hukumu itaamua
 
mimi nahisi mwandishi wa hii mada nae ni tapeli..

sitaki kuamini huyu mama anaweza kuwa na guts za kumtapelii magufuli
 
Ila nawewe sjakuelewa mara kaolewa singida mara buguruni kipini kipi ss halafu umeandika kwa hasira
 
Haiji akilini, anamuita mjomba marehemu na still a claim mirathi kama mke? How?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom