Upakaji rangi kucha kwa wakina dada

Upakaji rangi kucha kwa wakina dada

cleverr

Senior Member
Joined
Mar 3, 2020
Posts
141
Reaction score
140
Habari zenu wakuu; kichwa cha habari cha jieleza. Hivyo basi kwa mwenye ideas anipe mwanga juu ya hii fursa at least mtaji, aina za rangi,faida,changamoto n.k
JPEG_20210101_181524_1101342907986273553.jpg
 
1. MTAJI
Hapa inategemea na wewe kama utakuwa unapaka rangi za kawaida tu au pamoja na za Gel, so hapa idadi za rangi unazotaka itategemea na mtaji wako, kwa haraka haraka dozen 2 za rangi za kawaida kkoo wanauza kuanzia 19000 na rangi za Gel chupa moja ya rangi kuna za 5000,10000,pia kuna mashine ile ya Gel ya kukaushia rangi zipo za 50000,100000,150000..Hapa ni wewe tu jinsi utakavyotaka uanzaje na hii harakati.

2. AINA ZA RANGI
Hapa aina za rangi zipo nyingi sana aisee zingine za makampuni ya nje but kuna hizi za wa bongo kuna za Lavy na robiannah ni nzuri sana. Za lavy rangi ya kawaida chupa moja 3000 ya Gel chupa moja 10000 but hao robiannah wana rangi za Gel tu chupa moja wao wanauza 10000

3. FAIDA
Hii biashara ina faida kama zilivyo biashara zingine kikubwa hapa ni inshu ya Location tu iwe na mzunguko wa watu. Biashara yoyote inayohusu urembo wa mwanamke zinalipa sana.

4. CHANGAMOTO
Kila biashara ina changamoto zake hapa ni jinsi tu we mwenyewe unavyoiendesha, Kikubwa tu kuwa serious na biashara yako kwenye hii biashara wateja wako sana ni wanawake wafanye sana kuwa kama marafiki zako mana watakuletea na marafiki zao wengine. Kama umeamua kufanya kwa malengo hii inshu,Usilete umate umate wa mapenzi kwenye hii kazi.

NOTE: Sijui upo Mkoa gani ila Machimbo ya kupata haya mazaga ya Urembo wa kucha mengi yapo Dar kariakoo, Mtaa wote ule wa Jangwani na mafia, mtaa wa congo kule kama sikosei na karibu maeneo ya msikiti wa mtoro.
 
Ahsante sana mkuu mekupata be blessed
 
Back
Top Bottom