Uozo hospitali ya Amana

raisi2020

Member
Mar 4, 2016
82
83
Kwa kiongozi yeyote atakayesoma thread hii kama utakuwa mzalendo wa kweli naomba ulifanyie kazi, jana nimekwenda hospital ya Amana, kwa kuanza tu mapokezi kuna mkaka mmoja amenipa namba na kunisikiliza vizuri sana.

Akaniambia nizunguke kwa nyuma katika hiyo hiyo mapokezi kuna wapokezi wengine kwa ajili ya kulipia registration fee, kuna dada mmoja mweupe anajifunga ushungi kama wakiarabu flani lakini si mwarabu huyu dada customer service yake ni mbovu mbovu.

Pia mbele yake kidogo kuna kaka mwengine yeye anachajisha pesa pia hafai kabisa anahadithia movie huku wagonjwa wamesimama dirishani, huyu dada nae ukimwongelesha kama hakuoni anakutupa kwa huyo mkaka then kaka nae anakutupa kwa dada, mgonjwa unabaki huelewi kabisa. Tukija kwa doctors utaratibu ni mbovu sijapata kuona wagonjwa mnajipanga wenyewe pasi usimamizi wa nesi anayemsaidia doctor, kwenye foleni ugomvi mtindo mmoja,

Naomba usalama wa taifa, viongozi wa nchi yangu Tanzania tufanye kazi na si masihala watanzania wanapata shida katika hospitals hizi, watumishi hawajui kilichowapeleka pale.
 
Mimi nahitaji anuani ya posta na namba ya simu ya hospitali ya Temeke, mwenye nayo anipe msaada
 
Pole

Ila watanzania mmezidi upole

Kama mtoa huduma hakupi hiduma yupo busy na movie sijui simu direction hazieleweki muwakie tu....
 
Pole mkuu nadhan wahusika wamepata pa kuuanzia! Watawafanyia surprises visiting!
 
Nafikiri kuna haja ya kuweka somo la Huduma kwa Wateja kwenye shule zetu maana hili ni tatizo la kitaifa
 
Siku hiyo nampeleka mama hospitali (siyo iliyotajwa na mleta uzi) usiku saa mbili nafika nakuta chumba cha daktari hakina daktari na kuna watu wamepanga foleni.

Hapo mama kashaanza kuimba zile nyimbo za wazee wakiwa wanaumwa.

Nawauliza wenzangu alipo daktari wananionesha yupo kibarazani anaongea na wenzie. Yaani watu zaidi ya 20 wamekaa kwenye foleni na wanamuona daktari.

Nikamfuata yule jamaa, baada ya salamu nikamuuliza mbona haupo ofisini wakati watu tumeganda pale, akajibu yeye kuna mtu alimuacha hajui kama ameondoka au la.
Nikamwambia basi huyo mtu atakua kaondoka nina mgonjwa wangu kazidiwa.

Nikaongozana na jamaa, kwa uzembe wa wale niliowakuta nikawapita wote hadi ndani.

Dada ananiambia ulivyoondoka wenzako wakawa wanasema huyu anajifanya mjanja ngoja dokta agome kumhudumia amuweke wa mwisho.

Uoga wetu ni shida pia.
 
Yule jamaa na dada wakifanya masihala nitawaweka live humu,hiki ndio kiwe chanzo cha habari kwa wao,wasijaribu kuchafua serikali ya tz kwa uzembe wao,pale ni sehemu ya huduma kwa wateja tena wagonjwa
 
Back
Top Bottom