Uovu ukishinda dhidi ya wema,ole wetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uovu ukishinda dhidi ya wema,ole wetu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Aug 18, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimesikiliza na kupokea kwa mshangao hukumu dhidi ya Zombe.Inashangaza na kutia kinyaa.Sikuwa na wasiwasi wowote kwamba Zombe angefungwa kwa vile ushahidi hata kama ni wa kimazingira, ulikuwa unaonyesha wazi kabisa kwamba Zombe kwa vyovyote vile alihusika kwa njia moja au nyingine na mauaji ya wafanyibiashara wale wa Ifakara.Na hata mauaji ya wazi ya shahidi yule muhimu yalionyesha kwamba kulikuwa na jambo la kuficha.Hakuna shaka yeyote kwamba haya ni matunda ya ufisadi.Ni jinamizi la kutisha ambalo litaitafuna jamii mpaka imalizike kabisa.

  Hukumu hii inaonyesha jambo moja la wazi kabisa,nalo ni kwamba uovu umeshinda dhidi ya wema.Lakini si hilo tu la Zombe,yako mengi ya aina hiyo:
  *Mafisadi kula kuku kwa mrija huku wananchi wakiogelea katika dimbwi la
  umaskini wa kutupwa.
  *Wizi wa mali za taifa usiokemewa na kudhibitiwa,e.g.EPA,RICHMOND,madini
  rasilimali za misitu n.k.
  *Ufukarishaji wa watanzania wa makusudi kabisa kwa kudumaza kilimo,
  kuharibu mazingira,afya za wananchi n.k.
  *Mauaji ya wanachi wasio na hatia e.g.katika mgodi wa North Mara,mauaji ya
  wananchi na polisi ya mara kwa mara.
  *Spika Sitta kuwekwa kiti moto na mafisadi na mengi mengineyo.

  Sipendi kutabiri mabaya,lakini taarifa za kijasusi zinaoyesha kwamba uovu utashinda kabisa ifikapo 2012.Kama taarifa hizo ni za kweli,kitu ambacho sina wasiwasi nacho, basi tuna muda mfupi sana wa kukabiliana na uovu,baada ya hapo kupambana na uovu haitawezekana tena!

  Inawezekana hawa jamaa wanazo taarifa hizi,ndio maana wanakuwa na ujasiri sana.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nafikiri unatakiwa kuelewa kuwa ni Serikali iliyokurupuka na kufungua kesi kisiasa zaidi badala ya kufata taaluma ya sheria.

  hakika kosa walioshitakiwa akina Zombe na wenzake la mauaji ya wafanyabiashara kwa hilo hawana hatia ila kama DPP angetulia vizuri na kuacha kusikiliza wanasiasa wanasemaje na waandishi uchwara wanaandikaje kuhusu kadhia nzima wangeweza kuandaa kesi nzuri ikiwa pamoja na kuweka ushahidi pasi na shaka na hivyo kuwatia hatiani akina Zombe.

  hakika kazi kubwa ya mahakama ni kutafsiri sheria na si kutunga sheria na mahakama inahukumu kwa kosa lile ulioshitakiwa nalo na si vinginevyo.

  FUNZO LINALOPATIKANA HAPO NI OFISI YA DPP KUWA MAKINI KATIKA KUFUNGUA KESI NA SIO KUFATA MATAKWA YA WAANDISHI AU WANASIASA.
   
Loading...