Mkungo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 222
- 134
Ndugu wana jamvi napenda kupata ufafanuzi wa jambo hili hapo juu.
Uongozi wa serikali ya mtaa wa Tegeta A kata ya Goba umepiga marufuku usafiri wa Bajaj na pikipiki kwenye barabara ya kutoka Mbezi Luis kupitia Tegeta A mpaka Goba mpakani. Sababu iliyotolewa ni kuwa watu wenye daladala wanakoswa abiria na vile vile Bajaj na pikipiki zinatoza abiria elfu moja badala ya mia tano!
Je hii haipingani na sera za vijana? Je utaratibu wa kutoza nauli uweje na nani aseme hapo umbali huu uwe ni shilingi ngapi na vigezo viwe ni nini?
Tunapinga watu wenye kipato cha kati kubinafsisha barabara na kuvuruga ajira za vijana. Vile vile tunatumia Bajaj na pikipiki kibinafsi kuwahi sehemu tuendazo, kuokoa dharura za mtu kama anaumwa au kupata msaada na pia kama usafiri binafsi wa mtu kulingana na hali aliyonayo.