Uongozi wa Magereza Mbeya waeleza sababu za kumzuia Mbunge Joseph Haule 'Prof. Jay' kumuona Sugu gerezani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Uongozi wa Magereza ya mkoa wa Mbeya umetoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kumzuia mbunge wa Mikumi, Joseph ‘Profesa Jay’ Haule kuwaona Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda za Juu Kusini, Emmanuel Masoga walioko mahabusu ya gereza hilo.

Profesa Jay akiwa ameambatana na mkewe Grace jana walifika katika gereza hilo wakitaka kuwaona viongozi hao wa Chadema wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli lakini walishindwa kufanikisha kusudio lao.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Magereza mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Paul Kijida amekiri kuwazuia na kueleza kuwa kiutaratibu haikuwa siku ya kuwaona wafungwa.

“Ni kweli walikuja hadi ofisini kwangu lakini taratibu hiziko hivyo. Siku za kawaida kama hizi huwa tunamruhusu mtu aliyempelekea chakula au ataruhusiwa pale mfungwa au mahabusu anaumwa, au mwanasheria wake anaruhusiwa kama tu kuna kitu muhimu,” alisema Kijida.

Alifafanua kuwa siku ya kuwaona wafungwa kwa watu wa kawaida ni Jumamosi na Jumapili pekee na sio vinginevyo.

Jana, Profesa Jay alieleza kushangazwa na hatua ya kuzuiwa akidai kuwa anachofahamu ni kuwa mbunge hazuiwi kuwaona wafungwa, kinyume na kilichomtokea.

Leo, Profesa Jay amefanikiwa kuwaona Sugu na Masoga waliofikishwa Mahakamani na kuzungumza nao kama alivyoahidi jana kuwa hataondoka mkoani humo hadi atimize azma yake.

Chanzo: Dar24

Soma zaidi kuhusu Mbunge Joseph Haule kuzuiliwa kumuona mbunge mwenzake hapa=>
Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay) akataliwa kumuona Joseph Mbilinyi (sugu)
 
Sote ni Watanzania na tusisahau kuwa furaha ya mwenzio ni neema kwako, nashangaa pale tunapofurahia huzuni ya jirani!
 
Acha kuandika utumbo hapa, una data zozote zinazoonesha mfungwa amepewa mimba na askari wa kawaida achilia mbali Mkuu wa Magereza
Naona nimepiga palepale!!

Majuzi wakati wa maadhimisho ya Sheria, haki, nk mkuu wa Magereza nchi alisema takribani wafungwa 115 ni waja wazito....
 
Yaani ni hatari sn..

Mkuu wa Magereza nchini majuzi tu kasema idadi kubwa tu!!
Hali inatisha kwa kweli. Serikali kupitia vyombo husika inabidi wapitishe sheria ya Wakuu na askari wa Magereza ya wanawake kuhasiwa ili kupunguza mimba magerezani. Maana hakika hao wanawake sio Bikira Maria kupata mimba bila kutafunwa.
 
Hali inatisha kwa kweli. Serikali kupitia vyombo husika inabidi wapitishe sheria ya Wakuu na askari wa Magereza ya wanawake kuhasiwa ili kupunguza mimba magerezani. Maana hakika hao wanawake sio Bikira Maria.
Mm kuhasi siyo vzr! Coz wengine ni wake za watu na wengine bado hawajaolewa na wana ndoto za kuwa na familia baada ya maisha ya gerezani. Cha mhimu ni nidhamu kazini tu!!

Hii ni rushwa ya chakula, kupunguziwa kazi, nk gerezani.
Nadhani tujifunze kwa nchi zilizoendelea. Wao walidhibiti vp hii kitu?

Ila mkuu wa gereza akitimuliwa kwa ujinga huu. Anae kuja hata kubali upuuzi kama huu uendelee
 
Yana mwisho hayo makamanda , endeleeni kupambana tu
 
Izo mimba sio kama wamezipata wakiwa ndani ya jela,Isipokuwa wamekuja nazo baada ya kupatikana na hatia nasio wakati wakiwa ndani
 
Back
Top Bottom