Uongozi wa kanisa KKKT utoe tamko haraka kuhusu yaliyojiri Jana Kimara

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,104
Salam,

Kwa Muda wa zaidi ya wiki mbili huku mitandaoni kumekuwa na mjadala mrefu unaozungumzia utata wa elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar. Ninaamini hichi ndicho kilichopelekea mkuu huyo kusimama jukwaa la kanisa la KKKT Kimara katika jitihada za kujinasua kwenye shutuma hizo ambazo mwisho wake sio mzuri endapo itabainika kuwa ni kweli.
Sisemi kuwa shutuma hizi ni za kweli na wala binafsi sina ushahidi wa uhakika sana juu Hilo.

HOJA YANGU:
Naomba uongozi wa kanisa langu KKKT waliopo pale Luther house Dar wanifafanulie uhalali wa kutumia madhababu ya kanisa katika jitihada za kujisafisha kisiasa. Kwenye hili saga tumeshaona baadhi ya viongozi wengine wa kidini wakijitoa kusema wazi kuwa shutuma hizi za mkuu wa mkoa ni za kweli kabisa. Je, aliyempa mamlaka mchungaji wa Kimara kumsimamisha mkuu wa mkoa ili ajisafishe ni nani?? Ninalijua vizuri kanisa langu kuwa Lina uongozi makini na sio rahisi kwa mtu yeyote Kufanya Chochote kanisani bila uongozi husika kujua..... Na hasa mtu mkubwa Kama mkuu wa mkoa. Swali langu, je uongozi wa kanisa unahusika kwenye hili?
Kama hauusiki tafadhali naomba uongozi utoe tamko mapema sana. Kwa sababu ikiwa muhusika ataanguka inaweza ikaathiri heshima ya kanisa kwa namna moja au nyingine.

Ni Hilo tu.
Mimi muumini wa KKKT mwenye Kadi namba 881.
 
WANALI CHAFUA HEKALU LA BWANA
KKKT Sio sehem ya wanasiasa sijui kujisafisha kwa kuhubiri
YAani Hadhi Ya KKKT inaanza polomoka uwezi ona mambo kama haya RC
Kutoa salam fupi hatukatai lkn mtu sijui ni kuhubiri sasa si aende kusomea uchungaji kuliko kubadili sauti (kinyonga Bashite) kama Mwl Mwakasege
 
Hivi jana bashite alipewa muda wa kuhubiri kabisa au ni nini? Maana haingii akilini mtu anatoa salaam fupi kwa lisaa lizima. Kitendi chake cha kulia madhabahuni inaashiria wazi ana vyeti vya kufoji. Aache kutapatapa atoe vyeti au aombe radhi full stop
 
Hapa ndipo mtu unapoanza kukata tamaa na kanisa hili ambalo limenikuza tokea mdogo hadi leo na mimi ni mtu mzima,kanisa halipaswi kutumika kisiasa namna hii na sidhani kama makonda ni mlutheri!!Yule mchungaji alinibore sana jana kwa kweli,anadanganywa na mifuko ya cement!Mbona kila mara watu tunachanga kwa ajili ya ujenzi wa makanisa?Wakikaa wanahubiri watu wanakimbia makanisa ila kwa uppuzi huu kwanini watu wasikimbie?
 
ishawah tokea kama hii kwenye mbio za urais 2015 mbona hamkuomba matamko
 
Salam,

Kwa Muda wa zaidi ya wiki mbili huku mitandaoni kumekuwa na mjadala mrefu unaozungumzia utata wa elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar. Ninaamini hichi ndicho kilichopelekea mkuu huyo kusimama jukwaa la kanisa la KKKT Kimara katika jitihada za kujinasua kwenye shutuma hizo ambazo mwisho wake sio mzuri endapo itabainika kuwa ni kweli.
Sisemi kuwa shutuma hizi ni za kweli na wala binafsi sina ushahidi wa uhakika sana juu Hilo.

HOJA YANGU:
Naomba uongozi wa kanisa langu KKKT waliopo pale Luther house Dar wanifafanulie uhalali wa kutumia madhababu ya kanisa katika jitihada za kujisafisha kisiasa. Kwenye hili saga tumeshaona baadhi ya viongozi wengine wa kidini wakijitoa kusema wazi kuwa shutuma hizi za mkuu wa mkoa ni za kweli kabisa. Je, aliyempa mamlaka mchungaji wa Kimara kumsimamisha mkuu wa mkoa ili ajisafishe ni nani?? Ninalijua vizuri kanisa langu kuwa Lina uongozi makini na sio rahisi kwa mtu yeyote Kufanya Chochote kanisani bila uongozi husika kujua..... Na hasa mtu mkubwa Kama mkuu wa mkoa. Swali langu, je uongozi wa kanisa unahusika kwenye hili?
Kama hauusiki tafadhali naomba uongozi utoe tamko mapema sana. Kwa sababu ikiwa muhusika ataanguka inaweza ikaathiri heshima ya kanisa kwa namna moja au nyingine.

Ni Hilo tu.
Mimi muumini wa KKKT mwenye Kadi namba 881.
Hiyo kadi unatoaga sadaka kwenye bahasha au ni urembo tu?
 
WANALI CHAFUA HEKALU LA BWANA
KKKT Sio sehem ya wanasiasa sijui kujisafisha kwa kuhubiri
YAani Hadhi Ya KKKT inaanza polomoka uwezi ona mambo kama haya RC
Kutoa salam fupi hatukatai lkn mtu sijui ni kuhubiri sasa si aende kusomea uchungaji kuliko kubadili sauti (kinyonga Bashite) kama Mwl Mwakasege
Kuna yule wa kule kwetu umasaini yeye 2015 alitumia madhabau kutaka kutugawa watz kidini akadiliki kusema tz haijawah kua na rais mluther
 
Wakuu wa makanisa jaribu kuwa makini na wanasiasa.Kwanza kama alivyosema yeye siyo muumini wa dhehebu hili,Bali mke wake.Kwanini apewe nafasi na kuanza kujiliza ovyo,mnadhalilisha MADHABAHU YA BWANA.
 
Lutheran ilikuwa enzi za akina askofu Kolowa,Mshemba,Sendoro,Mshana etc,upuuzi huu sidhani kama ungetokea,wale wazee walikuwa makini na hawayumbishwi kijinga.
 
Back
Top Bottom