Uongo wa mwanaume faraja kwa mtoto wa kike

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,525
Wanaume wamelazimika kuwa waongo kwasababu ni hitaji la wanawake wengi, (uongo) ukitaka ujuwe wanawake wengi hawapendi ukweli. Ukiwa mkweli ni ngumu kumpata mtoto wa kike, maana wengi wanachotaka kusikia ni ulaghai tu na si ukweli na ukiwa mkweli basi jua watakwambia huna mvuto huna ushawishi.

Imana ushawishi na mvuto ni kuwa na maneno ya uwongo?

Vijana wengi wastarabu wakweli wanakosa wanawake kwa kuwa wakweli au mahusiano yao kuvunjiaka kwa kuacha. Na vijana wengi maplayer kila siku wanabadilisha vimwana na ndomana kuna siku moja dada mmoja aliniuliza swali;

Hivi kwanini wanaume waongo?

Nikamjibu; Sababu wanawake mnapenda kuongopewa.

Wengi ambao wanakataa uongo ni wale ambao washachoka, inamana washakuwa na mahusiano na watu kibao mpaka imefika mahali kachoka sasa anatafuta mahali atulie.

Ukimkuta mtu kama huyu, ukimwambia nimeoa atakujibu sawa.

Ukimwambia mnawatoto sita atakujibu haina shida.

Mke wangu wa kwanza alikufa gafla.

Atakujibu mipango ya Mungu

Kwanini wanawake mnakuja kuutaka ukweli baada ya kuhangaika sana kwanini msipendelee ukweli toka mwanzo?
 
kweli kabisa!! nasema ni kweli kutokana na yanayotokea katk family yangu kwa sasa, ninamgogoro mkubwa sana na mke wangu kwa sababu yakua mkweli.
mkuu ukiona kitu nimeandika hapa basi ujuwe nishakitafiti sana mkuu pole sana
 
mkuu matatizo ni mengi sana kwa sisi wanaume tunaongea ukweli !!. nashindwa hata nieleze vipi maana ni mkasa mrefu sana! ila naona tumefikia kutengana kutokana na kua mkweli ndugu yangu. ninavyo andika haya tuna kama siku 5, hatuongei kabisa wala hafanyi chochote kile. mda huu anapaki nguo zake aondoke.
 
mkuu matatizo ni mengi sana kwa sisi wanaume tunaongea ukweli !!. nashindwa hata nieleze vipi maana ni mkasa mrefu sana! ila naona tumefikia kutengana kutokana na kua mkweli ndugu yangu. ninavyo andika haya tuna kama siku 5, hatuongei kabisa wala hafanyi chochote kile. mda huu anapaki nguo zake aondoke.
Kwanza mkuu nikupe pole japo kwa kirefu sijui hasa tatizo nini ,ila kama binadamu lazima tupeane pole.

Nikukumbushe kitu mitihaani ni sehemu ya maisha ,na hii dunia si pepo kusema utaishi kwa raha na wala si moto kusema utaishi kwa tabu ,vitu vyote mungu amevibalance .

Pia kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu mitihaani ipo mingi sana katika mahusiano .

Yapo mambo unaweza mkakaa mkayazungunza na mkayamaliza na yapo mambo yanashindikana na suluhu pekee ni kupeana muda..

Na kuna wakat mtu hawezi kujuwa umuhimu wako wakati uko naye .na ni heri aende ili akajifunze hata siku akirudi atakuwa na adabu
 
Back
Top Bottom