Uongo, Unafiki na Uzandiki wa CCM!

Uongo, Unafiki na Uzandiki wa CCM!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,168
Reaction score
27,772
Inasikitisha kuona kwamba CCM wamekuwa mstari wa mbele kuwadanganya wananchi kwamba uendeshaji wa serikali 3 ni ghali kuliko serikali 2 huku wakiwa hawatoi takwimu za kuonesha ughali huo unakujaje. Swali la kujiuliza ni kwamba ikiwa serikali 3 ni ghali na kama kweli CCM wana nia njema ya kupunguza matumizi ya serikali ni kwa nini basi tusiende kwenye serikali 1? Hapo ndipo unapogundua kwamba Dr Antipas Lissu alipowaambia CCM kwamba wamezoea kuishi kwa uongo hakuwa amekosea hata kidogo. Ndivyo CCM walivyozoea kuishi.

Hii hesbau ni rahisi sana. Leo nilikuwa namuuliza mtoto wangu anayesoma chekechea kama 1 na 2 ni ipi kubwa, akaniambia kwamba ni 2! Sasa swali rahisi kama hili kwanini CCM wanashindwa kulitatua wakati mtoto wa chekechea anaweza? Ndani ya CCM kuna maprofesa lukuki lakini wote wameacha taaluma zao na kuchagua kutumikia uongo. Ndugu zangu, wote ni mashahidi na mnafahamu kwamba 1 ni ndogo kuliko 2 ila CCM wameng'ang'ania serikali 2 ambazo ni ghali kuliko serikali 1 kwa sababu zina manufaa kwao kisiasa. Ndio maana wanajenga hoja mufilisi kwamba serikali 3 ni ghali kuliko 2 huku wakisahau kwamba 1 ni nafuu zaidi kuliko 2! Pia serikali 1 zitaimarisha muungano na umoja zaidi kuliko hizi serikali 2 za kulazimishana. Hili hawalioni ila wamebaki kukomaa na serikali 3!

Halafu, ni lini CCM walikuwa na huruma kwa wananchi? Sote tunajua na tunafahamu jinsi pesa za umma zinavyofisidiwa watu wa CCM na kutumiwa na serikali kununua na kuendesha magari ya kifahari huku wananchi wakila majani pamoja na kukosa huduma za kijamii kama matibabu, maji, elimu, miundombinu, nk. Hiyo huruma ya CCM imetoka wapi ghafla hadi wafikirie kupunguza idadi ya serikali kwa manufaa ya wananchi? Hiki ni kichekesho cha mwaka.

Uongo mwingine wa CCM ni dhana potofu kwamba serikali 3 zitavunja muungano. Hii ni hoja ya kitoto na kizezeta kabisa. Kinachosikitisha na kushangaza zaidi ni pale CCM wanapolazimisha na kuwatia hofu wananchi kwa kuwaaminisha kwamba uwepo wa serikali 3 (serikali ya Tanganyika, Zanzibar na MUUNGANO wa Shirikisho) eti ni kuvunja muungano. Muungano utavunjikaje wakati katika hizo serikali 3 imo serikali ya Muungano (Shirikisho)? Hivi hawa INTARAHAMWE hawana haya? Mtaji wa hawa watu ni ujinga watanzania walio wengi. Kuna wajinga wachache ambao wanakubali uongo huu lakini wengi wetu tunaupuuzilia mbali.

Hivi jamani mtu ukiwa na nyumba yako ambayo haikidhi mahitaji, ukiamua kuifanyia renovation au ukaibomoa na kujenga nyumba mpya iliyo kubwa, imara na bora zaidi, tatizo liko wapi? Ni nini hofu ya CCM katika uwepo wa serikali 3 hadi waanze kuwatisha raia kwamba ikiwa serikali 3 zitaruhusiwa jeshi litachukua nchi? Kama ndivyo basi, sisi raia tunaoteseka chini ya utawala wa CCM tunalikaribisha jeshi kwa mikono miwili lije litawale badala ya kuendelea kuishi ndani ya utumwa wa serikali ya CCM.

CCM hawahawa waliwaaminisha watu kwamba vyama vingi vya siasa vikiruhusiwa, nchi itaingia vitani kama ilivyowahi kutokea huko Rwanda. Walifikia hatua ya kutembea nchi nzima wakionyesha video za vita ya Rwanda na intarahamwe ili kuwatisha wananchi kuhusu ujio wa vyama vingi. Ni zaidi ya miaka 20 sasa tangu vyama vingi viruhusiwe nchini lakini hatujawahi kuona nchi ikiingia vitani. Ama kweli CCM wamezoea kuishi kwa UONGO, ukweli hawauwezi! Propaganda zao hizi tumezizoea, hawakuanza leo wala jana.

:yield:
 

Attachments

  • shangingi.jpg
    shangingi.jpg
    34.5 KB · Views: 550
  • fisadi.jpg
    fisadi.jpg
    43.3 KB · Views: 487
  • shivji.jpg
    shivji.jpg
    16.1 KB · Views: 470
  • maisha bora--kunywa uchafu.jpg
    maisha bora--kunywa uchafu.jpg
    6.7 KB · Views: 1,756
  • maisha--maji bora.jpg
    maisha--maji bora.jpg
    63.4 KB · Views: 494
  • maisha bora.jpg
    maisha bora.jpg
    17.2 KB · Views: 488
Huo ni uzandiki, ccm wangeogopa gharama wangetumia sh. 8.2 bilion kutengeneza ukumbi wa bunge pekee? Barabara vijijini hazipitiki, wananchi wanakesha majiani kwa kukosa barabara nzuri, wakati huohuo interahamwe wanalipana 300000 kwa siku kwa mipasho, kejeli,matusi na kuchakachua maoni ya wananchi kuhusu katiba waitakayo!
 
Dah hapa umewamaliza kabisa. Shoka linaendelea kuukata m'buyu muda c mrefu utaanguka. Big up
 
Halafu wehu kama MSALANI A4. bado wananyanyua pua kuwasemea vizuri hawa majambazi wachumia matumbo yao ccm.
 
Last edited by a moderator:
Halafu wehu kama MSALANI A4. bado wananyanyua pua kuwasemea vizuri hawa majambazi wachumia matumbo yao ccm.

hii ni sehemu ya kikundi cha makasuku ambao huropoka kila kitu walichokaririshwa. kiongozi wa kikundi hiki cha intarahamwe ni Lukuvi--ambaye alidiriki kuwatukana na kuwadhalilisha waislamu akiwa ndani ya kanisa. hawa wehu watakuja kutusababishia mauaji ya kimbari.
 
Last edited by a moderator:
Katika hoja makini kama hii, huwezi kuwaona INTARAHAMWE wakitoa maoni yao--wanapita tu kama vile hawaoni. Hivi nyie CCM mpo wapi hasa? Njoeni mtupe ufafanuzi kuhusu ughali wa serikali 3 ukilinganisha na serikali 1. Njoo pia mtuambie ni jinsi gani jeshi litachukua nchi ikiwa serikali 3 zitapigiwa kura na wananchi. Yakhe, hamna khaya!????????????
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa Afrika ni mafisadi na haijalishi ni chama gani kinaongoza nchi. Kauli zinazotolewa bungeni hivi sasa na hata ninavyosoma hoja hizi ni za uchochezi na zina kera sana. Ninaona tunaelekea pabaya na mdomo yetu. Vurugu zikianza hazita chagua chama.
 
Na siku ikifika CCM ikichoshwa na matusi na hizi kejeli hakuna rangi tutaacha kuona. Ni mtazamo wangu tu.
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa Afrika ni mafisadi na haijalishi ni chama gani kinaongoza nchi. Kauli zinazotolewa bungeni hivi sasa na hata ninavyosoma hoja hizi ni za uchochezi na zina kera sana. Ninaona tunaelekea pabaya na mdomo yetu. Vurugu zikianza hazita chagua chama.

hakuna vurugu au vita iliyowahi kuua/kumaliza watu wote! acha hiyo vita ije tuuane watakaobaki wataheshimiana kuliko sasa! hata mabondia wasipodundana huwezi kupata mshindi kila mmoja atajigamba kwa maneno!
 
Na siku ikifika CCM ikichoshwa na matusi na hizi kejeli hakuna rangi tutaacha kuona. Ni mtazamo wangu tu.
Umesahau kuwa waliotwaa medali za dhahabu kwa matusi nchini mwetu wote wanatoka chama cha magamba, ambao ni k
Kibajaj, Serukambaaaa, na Mkamia maji, yule mheshimuwa sana kutoka kule Kondoa!!
 
Matusi hayajengi tujenge hoja makamanda tusiwe kama hawa machizi kina ifweero,msalani,lusungo,abakorakamo
 
Asilimia kubwa ya viongozi wa Afrika ni mafisadi na haijalishi ni chama gani kinaongoza nchi. Kauli zinazotolewa bungeni hivi sasa na hata ninavyosoma hoja hizi ni za uchochezi na zina kera sana. Ninaona tunaelekea pabaya na mdomo yetu. Vurugu zikianza hazita chagua chama.

Mkuu wewe unashauri nini kifanyike maadam viongozi wengi wa Afrika kama unavyosema ni mafisadi bila kujali chama wanachotoka?

Tujikalie tu kimya maisha yetu yote tukiendelea kuburuzwa na hao mafisadi wachache kwa kuogopa vurugu?!
 
MOSSED II matusi hayajengi bali yanabomoa. Kuwaita Chadema machadema au Chadomo na kuwaita Maccm au mafisadi hayatatusaidia. Inadhihirisha ubutu wa kufikiri.
 
hakuna vurugu au vita iliyowahi kuua/kumaliza watu wote! acha hiyo vita ije tuuane watakaobaki wataheshimiana kuliko sasa! hata mabondia wasipodundana huwezi kupata mshindi kila mmoja atajigamba kwa maneno!

Mara zote mdomo hauna ushirikiano na maeneo mengine ya mwili. Shauri yako ukipata nafasi tena utakuja omba msamaha hapa.
 
Back
Top Bottom