Uongo unaangamiza taifa

Uongo unaangamiza taifa

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,036
Reaction score
20,031
Uongo imekuwa siyo tu tabia ya viongozi na serikali imegeuka kuwa sehemu ya maisha yetu. Hii ndiyo sababu tumefika hapa tulipo: taifa likiendeshwa kwa hila na uongo badala ya ukweli. mfano ni huu uchaguzi wa mwaka huu unadhani ulikuwa huru?

Tunasema mshindi alishinda kwa kura milioni 32 kati ya 36 — lakini je, hiyo ni ukweli au hila na uongo kisa madaraka kila mtu anajua hilo.

Machafuko, mauaji, na ukweli unaofichwa, Watu wameuawa, lakini wanasema waliokuwa waandamanaji walikuwa ‘wageni’. Miili haipo, ushahidi hauonekani ni mwendo wa uongo na hila wanajaribu kuhalalisha yote haya bila uoga hata kidogo.

Dhambi ya uongo ni nzito Kukubali uongo kuna gharama kubwa zaidi kuliko tunavyodhani. Inaangusha imani yetu, kuharibu miundombinu ya haki na kupelekea kizazi kimoja au zaidi kukosa msukumo wa kujenga taifa.

Nini cha kufanya kama taifa

Kama tunataka taifa lianze kupona, lazima tuweke ukweli mbele kwenye serikali, viongozi wawe wakweli daima kwenye vyombo vya habari, vyombo vya ulinzi na ndani yetu wenyewe sisi wananchi. Bila ukweli, tunajenga taifa la kijinga la vituko, hila na uongo..!
 
Hii tabia ni sugu na ina kera. Kama taifa tuna tatizo la malezi labda kuanzia ngazi ya familia.

Aisee viongozi ni waongo sijapata kuona.
 
Back
Top Bottom