Uongo na ukweli Wa Tundulisu

Uongo na ukweli Wa Tundulisu

Geniuss

Member
Joined
Jan 19, 2019
Posts
28
Reaction score
202
Nimeona wananchi wakawaida na wasio Wa kawaida Kwa maana ya viongozi ,wamejitosa kujibu hoja za tundulisu .wengi hasa vijana wenzangu wakimkosoa vikali na kusema analisaliti taifa.
Lakin wengi pia wanamuunga mkono Kwa kauli zake.
Niulize maswali elekezi machache.
Kama ungekua Tundulisu Leo ukiwa umepigwa risasi zote hizo,kumbuka ni risasi za moto sio za maji Wala vumbi.
1.camera zitolewe eneo la tukio pasipo taarifa rasmi kutoka
Je ,utasema waliotoa camera ni wazalendo ?
2. Hakuna formal process za kusaka wahusika wa tukio
Je wewe utasema huo ndio uzalendo kukaa kimya?
Nadhan tukubali kutokubaliana.
Kuna kizazi Tanzania hii kina majivu kichwan,hasa vijana kadhaa Wa CCM,i hate to say this , haiwezekan mnatetea Kila kitu .
Atakuja kuuawa mtu hadharan mseme hajapigwa risasi Bali kanyeshewa mvua.
It is very stupid indeed naona vijana Wa CCM wengi are going crazy , supporting every move made by some of government elites.
Kuna vijana Wana Akili UVCCM ,lakin wengi ni wajinga na watafuta madaraka.
Wengi wanasoma upepo na sio msimamo,wakisikia katibu mkuu kasema Membe mhalifu wanaanza kuimba wimbo huo huo,
UVCCM leaders mnatudharirisha sana sisi vijana .
Mnafanya siasa za hovyo sana.
Swala la Tundulisu has to be handled with care ,litatulipukia na mtatucost wote.
Sasa hivi Kila balozi kawa msemaj,na ubaya taarifa zinazotoka hazisharabiani .
Can u get the hell out of ur cage and say where the hell do the CCTVs were taken?
What if ndan ya serikal kuna watu wanaoendesha matukio haya ili kumgombanisha Rais na umma ?
Badala ya kuwabaini mmekalia kupanua Mike zenu tu kumtusi mtu aliyepokea risasi 16 mwilini mwake.
Yaan apigwe risasi na Bado hata kuongea hamtaki aongee ?

Ningekua Tundulisu sio tu ningezunguka dunian kuieleza Dunia nadhan ningekua rebel .
Haiwezekan baba mzazi wangu kaona nimeonewa hataki hata kujua nan kanipiga ,Basi naenda Kwa majiran kutafuta msaada.
Tushukuru sana Lisu hana Nia mbaya na nchi ,vinginevyo mngeona vikundi vya kigaidi vingi sana.
Very stupid ,I repeat very stupid Kwa vijana mnaomkejeli Tundulisu eti kisa anaongea
 
Uhaini ni kosa la jinai, kwa tafsiri nyepesi ina maana kwamba ni kosa kubwa ambalo mtu analifanya dhidi ya nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti, mfano wa watu wasaliti wanaojulikana duniani ni Yuda ambaye kidini alimsaliti Yesu, mwingine ni Benedict Anold huyu jamaa aliisaliti nchi yake ya Marekani dhidi ya Mbritishi, wengine ni Vidkun Quisling, na Marshall Pe’tain.

Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.

Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano, kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais, kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya uhaini dhidi ya nchi yetu.

Kwa Hisani ya Mpekuzihuru.
 
Back
Top Bottom