UNZIJUA HAKI ZA BINADAMU kisha tujitathmini Tanzania tumepatia wapi na tumekosea wap?

Nesto E Monduli

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
247
155
Tukumbushane Tamko la Klimwengu juu ya [HASHTAG]#HakiZaBinadamu[/HASHTAG] "Universal Declation Of Human Rights" ambalo nchi yetu Tanzania tulisaini pia,kisha tujitathmini kama wazalendo wa taifa maarufu kama "kisiwa cha amani" penye mapungufu tuambiane na penye usahihi tupongezane bila ubaguzi kwa kuwa sote ni binadamua.

Azimio la ulimwengu juu ya haki za binadamu (pia: Tangazo la kilimwengu la haki za binadamu; kwa Kiingereza: Universal Declaration of Human Rights) ni tamko la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu lililotolewa tarehe 10 Desemba1948. Ilikuwa kati ya maazimio ya kwanza kabisa ya UM.
Msingi wa haki hizi uko katika kifungo cha kwanza kinachosema "Watu wote wamezaliwa huru, wakiwa na hadhi na haki sawa. Wamejaliwa akili na dhamiri na kupaswa kutendeana kwa roho ya kidugu".

Haki zilizomo katika tangazo hili si sheria ya kimataifa moja kwa moja jinsi zilivyo, lakini zimekubaliwa na kila taifa lililojiunga na UM.

MAWAZO YA MSINGI:
Mawazo ya msingi ya tangazo la haki za binadamu ni pamoja na:

-Kila mtu ana haki ya maisha, uhuru na usalama.

-Kila mtu ana haki ya elimu.

-Kila mtu ana haki ya kazi.

-Kila mtu ana haki ya kufuata utamaduni wake.

-Kila mtu ana haki ya kutotendewa kinyama au kikatili.

-Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake au kuchagua.

[HASHTAG]#Kanuni[/HASHTAG] za Azimio la ulimwengu la haki za binadamu.
Kifungu cha 1.
Watu wote wamezaliwa huru, hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yapasa watendeane kindugu.
Kifungu cha 2.
Kila mtu anastahili kuwa na haki zote za uhuru wote ambao umeelezwa katika taarifa hii bila ubaguzi wowote. Yaani bila kubaguana kwa rangi, taifa, wanaume na wanawake, dini, siasa, fikara, asili ya taifa la mtu, mali, kwa kizazi au kwa hali nyingine yoyote. Juu ya hayo usifanywe ubaguzi kwa kutegemea siasa, utawala au kwa kutegemea uhusiano wa nchi fulani na mataifa mengine au nchi ya asili ya mtu, haidhuru nchi hiyo iwe inayojitawala, ya udhamini, isiyojitawala au inayotawaliwa na nchi nyingine kwa hali na namna yoyote.
Kifungu cha 3.
Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya uhuru na haki ya kulinda nafsi yake.
Kifungu cha 4.
Mtu yeyote asifanywe mtumwa au mtwana; utumwa na biashara yake ni marufuku kwa kila hali.
Kifungu cha 5.
Mtu yeyote asiteswe, asiadhibiwe, asidharauliwe au kutendewa kinyama au kikatili.
Kifungu cha 6.
Mbele ya sheria kila mtu ana haki ya kutambulika kama mtu.
Kifungu cha 7.
Mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za kulindwa. Wote wana haki sawa ya kulindwa kutokana na ubaguzi wowote unaoweza kuvunja taarifa hii na mambo yoyote yanayoweza kuleta ubaguzi huo.
Kifungu cha 8.
Kila mtu ana haki ya kutetewa na baraza la hukumu kwa makosa ya kuvunjiwa haki zake za asili anazostahili kwa mujibu wa kanuni na sheria.
Kifungu cha 9.
Mtu yeyote asikamatwe, asifungiwe au kuhamishwa kutoka nchi yake bila sheria.
Kifungu cha 10
Kila mtu ana haki kamili ya kuhukumiwa vyema hadharani na baraza lililo huru na lisilo na upendeleo katika kutoa uamuzi wa haki zake na wajibu wake na wa makosa yoyote yanayo-mhusu.
Kifungu cha 11.
1. Kila mtu anaeshtakiwa kwa kosa la kuvunja sheria ana haki ya kuangaliwa kama si mkosefu mpaka imethibitishwa kisheria, kwa kuhukumiwa hadharani, kwamba ana hatia.
2. Mtu yeyote asitiwe hatiani kwa tendo lolote au jambo lolote halikupinga sheria ya taifa au ya kati ya mataifa wakati alipotenda. Wala asipewe adhabu kali zaidi kuliko ile iliyokuwamo katika sheria wakati alipofanya kosa.
Kifungu cha 12.
Kila mtu asiingiliwe bila sheria katika mambo yake ya faragha, ya jamaa yake, ya nyumbani mwake au ya barua zake. Wala asivunjiwe heshima na sifa yake. Kila mmoja ana haki ya kulindaw na sheria kutokana na pingamizi au mambo kama hayo.
Kifungu cha 13.
1. Kila mtu ana haki ya kwenda mahali anapotaka kuishi katika kila nchi.
2. Kila mmoja ana haki ya kuhama kutoka nchi yoyote, hata nchi yake mwenyewe, na ana haki ya kurejea katika nchi yake.
Kifungu cha 14.
1. Kila mtu ana haki ya kukimbilia na kustarehe katika nchi nyingine kwa ajili ya kuepukana na udhalimu.
2. Haki hii haiwezi kuombwa kwa udhalimu ambao hautokani na makosa ya mambo ya kisiasa au na makosa ya maazimio na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Kifungu cha 15.
1. Kila mtu ana haki ya utaifa
2. Mtu yeyote asinyang’anywe utaifa wake bila sheria wala asinyimwe haki ya kubadili taifa lake kama akitaka.
Kifungu cha 16.
1. Watu wazima, wanaume kwa wanawake wana haki ya kuoana na kuunda jamaa bila ya kizuio chochote kwa sababu ya rangi, taifa na dini. Wana haki sawa ya ndoa wakati wa maisha yao ya ndoa na wakati wa kutenguka ndoa.
2. Ndoa inaweza kufungwa tu kwa hiari na mapatano kamili kati ya hao wanaotaka kuoana.
3. Jamaa ni kiungo cha asili cha jamii ya watu, na inastahili kulindwa na watupamoja na serikali.
Kifungu cha 17.
1. Kila mtu ana haki ya kuwa na mali yake binafsi au kwa kushirikiana na watu wengine.
2. Mtu asinyang’anywe mali yake bila sheria.
Kifungu cha 18.
Kila mtu ana haki ya uhuru wa mawazo, dhamira na dini; haki hii inahusu pia uhuru wa kubadili dini yake au imani, na uhuru wa kubainisha hadharani au faraghani -akiwa peke yake au na watu wengine- dini yake kwa kufundisha kwa vitendo, kuabudu na kwa kuadhimisha.
Kifungu cha 19.
Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa kushikilia maoni yake bila kuingiliwa kati na uhuru wa kutafuta na kutoa habari na moni kwa njiayoyote bila kujali mipaka.
Kifungu cha 20.
1. Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika mkutano na chama kwa hali ya amani.
2. Mtu yeyote asilazimishwe kuwa mwanachama wa chama fulani.
Kifungu cha 21.
1. Kila mmoja anayo haki ya kushiriki katika serikali ya nchi yake yeye mwenyewe binafsi au kwa njia ya mjumbe aliyemchagua kwa hiari.
2. Kila mmoja anayo haki sawa ya kufanya kazi katika serikali; matakwa hayo huonyeshwa katika uchaguzi halisi unaofanywa muda baada ya muda ambao kila mt hupiga kura na ambao hufanywa kwa kura ya siri na kila mtu hiari yake.
3. Matakwa ya watu ndio yatakuwa msingi wa utawala wa serikali;hali itajidhihirisha kwenye chaguzi za haki kwa watu wote na ambazo zinafanyika kwa siri au namna nyingine ambayo itahakikisha uchaguzi kuwa huru.
Kifungu cha 22.
Kila mtu, kama raia, anayo haki ya kutunzwa na anastahili kupata haki zinazotokana na uchumi, starehe na utamadun-ambazo ni lazima kwa hali bora na maendeleo ya nafsi yake-kwa njia ya juhudi ya taifa na ushirikiano kati ya mataifa na kwa mujibu wa utaratibu na utajiri wa kila nchi.
Kifungu ch 23.
1. Kila mtu ana haki ya kufanya kazi, ya kuchagua kazi aipendayo, ya kuchagua yenye masharti mazuri na ana haki ya kulindwa asikose kazi.
2. Kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa na wengine wenye kazi ya namna moja bila ubaguzi.
3. Kila mfanyakazi anayo haki ya kupata mshahara wa kufaa na unaopendeza utakaomwezesha yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake kuishi katika hali bora, na ahifadhiwe-ikiwa lazimamaisha yake kwa njia nyingine.
4. Kila mtu anayo haki ya kuunda au kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi kwa ajili ya kulinda haki zake za kazi.
Kifungu cha 24.
Kila mtu ana haki ya kupumzika na kufanya kazi kwa kiasi cha saa zinazostahili.Pia ana haki ya kupata likizo, kwa kipindi na kupokea mshahara kama vile angekuwa kazini.
Kifungu cha 25.
1. Kila mtu anayo haki ya kupata hali bora ya maisha yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake na kupata chakula, mavazi, nyumba, matibabu na hifadhi za lazima kwa maisha yake. Pia ana haki ya kutunzwa wakati wa kazi, wakati wa ugonjwa, wa kutojiweza, ujane, uzee au anapokosa riziki yake kwa kutoweza kujisaidia.
2. Akina mama na watoto wanastahili kutunzwa na kupewa msaada maalum.Watoto wote-wawe wamezaliwa katika hali ya ndoa ama hapana-lazima watunzwe vyema.
Kifungu cha 26.
1. Kila mtu ana haki ya kuelimishwa. Elimu yapasa itolewe bure hasa ile madarasa ya chini. Elimu ya madarasa ya chini ihudhuriwe kwa lazima. Elimu ya ufundi stadi iwe wazi kwa wote. Na elimu ya juu iwe wazi kwa wote kwa kutegemea sifa ya mtu.
2. Elimu itolewe kwa madhumuni ya kuendeleza barabarahali ya binadamu, na kwa shabaha ya kukuza haki za kibinadamu na uhur wake wa asili. Elimu ni wajibu ikuze hali ya kuelewana, kuvumiliana na urafiki kati ya mataifa na kati ya watu wa rangi na dini mbalilmbali. Kadhalika ni wajibu iendeleze shughuli za Umoja wa Mataifa za kudumisha amani.
3. Ni haki ya wazazi ya kuchagua aina ya elimu ya kufunzwa watoto wao.
Kifungu cha 27.
1. Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika maisha ya utamaduni ya jamii yoyote, na ana haki ya kufurahia ustadi wa kazi na kushiriki katika maendeleo ya mambo ya sayansi na faida zinazotokana nayo.
2. Kila mtu ana ya kulindwa kwa kila hali kutokana na mambo ya sayansi aliyoandika, aliyochora au aliyogundua.

Kifungu cha 28.
Ni haki kila mtu alindwe na taratibu au kanuni za jamii na zinazohusu mataifa mbalimbali ambazo ndani yake uhuru na haki zilizoelezwa katika taarifa hii zinzweza kuhifadhiwa barabara.

Kifungu cha 29.
1. Kila mtu ana wajibu kwa watu wa jamii yoyote ambao kati yao tu ndio yanaweza kupatikana maendeleo kamili ya hali ya maisha yake.
2. Katika kutumia haki na uhuru wake, kila mtu itambidi kufuata kanuni zile tu zilizowekwa na sheria kwa ajili ya kulinda heshima inayotakiwa juu ya haki na uhuru wa watu wengine, na kwa ajli ya kuhifadhi kanuni za haki, usalama na hali njema ya maisha katika jamii ya kidemokrasia.
3. Uhuru na haki hizi kamwe visitumiwe kinyume cha maazimio na kanuni za umoja wa mataifa.
Kifungu cha 30.
Hakuna maneno yoyote katika taarifa hii yanayoweza kubashiriwa kwamba yanaruhusu nchi yoyote, kikundi cha watu au mtu fulani kufanya au kushughulika na jambo lolote ambalo nia yake ni kuharibu haki na uhuru zilizoelezwa humu.
 
Back
Top Bottom