Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,322
- 33,127
ali inayoweza kutafsiriwa kuwa ni hatua nzuri katika vita dhidi ya VVU, tafiti zilizofanywa na watafiti huko Marekani na Uingereza zimeonesha kuwa unywaji wa chai ya kijani (green tea) waweza kuwa na manufaa makubwa katika kuzuia maambukizi dhidi ya VVU.Matokeo
ya awali ya tafiti hizo ambayo yamechapishwa katika jarida la tafiti lijulikanalo kama Journal of Allergy and Clinical Immunologyyameonesha kuwa chai ya kijani ina kiasili ambacho kina uwezo wa kuzuia VVU kuzaliana kwa wingi ndani ya damu ya
muathirika.Utafiti wa awali uliofanywa katika maabara umeonesha kuwa kiasili hicho kijulikanacho kitaalamu kama Epigallocatechin gallate (EGCG) kina uwezo wa kunata katika chembe chembe nyeupe za damu zijulikanazo kama CD4 ambazo kwa kawaida hutumiwa na VVU
kuzaliana na hivyo kuzuia uwezekano wa VVU kuingia ndani ya chembe chembe hizo na hivyo kupunguza kasi yao ya kuzaliana.Mmojawapo wa watafiti hao, Profesa Mike Williamson wa Chuo Kikuu cha Sheffield cha nchini Uingereza alisema katika mahojiano kuwa, utafiti wao
umeonesha kuwa unywaji wa chai ya kijani unaweza kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU na pia kupunguza uwezekano wa VVU kuzaliana na kuongezeka katika damu ya muathirika.Hata hivyo watafiti hao wameonya kuwa ni mapema mno kwa jamii kuanza
kuyatumia matokeo ya utafiti huo na kwamba tafiti zaidi hususani zinazohusisha binadamu au wanyama zinapaswa kufanywa ili kuyapa matokeo ya utafiti huo uzito unaostahili. Tafiti za afya