Keren_Happuch
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 1,874
- 935
Jamani! Siku hizi imekuwa ni kawaida sana kwa mwanamume na mwanamke(ambao wanategemea kuoana) kuishi pamoja kama mke na mume. Si ajabu ukakuta mwanamke anakaa mkoa X lakini kila weekend au likizo anaenda mkoa Y eti kumsalimia"mchumba wake" ambaye kwa muktadha wa post hii na maadili ya jamii zetu na imani zetu za kidini huyo si mchumba bali ni MZINZI MWENZAKE au HAWARA YAKE. Na mbaya zaidi unakuta wanaishi maisha ya uzinifu kwa muda mrefu then wanaamua eti kubariki ndoa.
Viongozi wetu wa dini nao wanakubali kufungisha ndoa za wazinzi hawa bila aibu. Na si ajabu siku hizi kuona wazinzi wawili(mwanamke na mwanamume) wakiwa wameongozana wakienda ktk ibada iwe kanisani au msikitini. Sijui wanaenda kuabudu au kumkejeli muumba wao.
Kama wewe halijakutokea inawezekana umeliona kwa rafiki, ndugu au hata kwa adui yako.
NINI MAONI YAKO: NI KUMONG'ONYOKA KWA MAADILI AU NI MAENDELEO?
ooohh dearest,kweli unaamini kuishi na mtu kunakufanya umjue vizuri? kama nina lengo langu la kutaka kuolewa nita-pretend hadi niolewe...naamini uhusinao wa kawaida bila kuishi pamoja unaweza kusaidia kumuelewa mwenzi wako vizuri sana....
Ndo uonje mara kumi?Tatizo ni kwamba walioweng wana2mia njia hiyo kuwaharibu wasichana hawana nia
Hahahahahahaha! Michelle sijaelewa hapo kwenye rangi unasema nini....Mwaka 47 hili la kutest kabla ya ndoa lisingekubalika kabisa lakini 2011 sahau kabisa kwa mwanaume kuamua kuoa kabla ya kunanihii.
Kwa kweli mimi sikubaliani haya mambo ya kutest kabla, kwani imekuwa karanga jamani!!??? Sasa utaendelea kutestiwa tu..... mpaka unachakaa!!! Ninaamini ukijitunza na kumwomba Mungu, atakupa mume/mke mzuri ambaye utamfurahia! Kila mtu anavuna kile apandacho!
BAK...ninaamini bado wapo wachache wanaomcha Mungu ambao hawako tayari kuwa tasted kama karanga....LOL
Sio kwamba naamini dearest ila najua kwamba ni rahisi zaidi kumsoma mtu akiwa karibu kuliko akiwa mbali!!One can only pretend so much....itafika mahali mtu atajisahau!!!!
Ni muhimu kumjua mtu kabla hamjaoana!Ndo maana watu wanaobebana tu baadae kila mmoja anaanza sikujua yuko hivi..ningejua kumbe yuko vile!Kidini sio sawa ila katika ulimwengu wa leo ni muhimu sana!
Besides being pleasurable, sex is meant to be a spiritual experience that extends past the marriage bed into the everyday life of a married couple. It is not just setting up house together. The sex act locks the couple together in the purpose that God has set before them. The couple opens up emotionally to each other through the marriage act, which solidifies the continuing unity of the couple in living their lives for God. God intended for sex to help couples work out indifferences between them, along with the need to procreate.
Sex is a good thing. It must be, if God created it! The only way to keep it a "good thing" is to follow God's guidelines. God will reward you if you choose to honor Him, and save sex for its proper time and place - your marriage.
AIZAK
BAK...ninaamini bado wapo wachache wanaomcha Mungu ambao hawako tayari kuwa tasted kama karanga....LOL
Lizzy kuna watu smart sana,sasa tuseme umekaa nae fo four years then anaanza kuonyesha rangi zake,huoni kwamba itakuwia ngumu sana kumuacha mtu ambaye umekuwa nae kila siku ya maisha yako kuliko yule ambaye mna urafiki wa kimapenzi lakini hamuishi pamoja.....manake hapo kwenye kuishi nae muda mrefu hata na ndugu na jamii watakuwa wanajua mnaishi pamoja....its even harder.....unless mwanaume which most of the time ndo decision maker wa muingie hatua ya ndoa au lah,ana commitment kubwa,naona its a very big risk to take!!!
Mambo yamebadilika siku hizi lazima utesti kwanza kama kitu iko fresh ndo unaingia mkataba kama hapana unakula kona "Usijeukauziwa mbuzi kwenye gunia" Mawazo yangu lakini
Ni kweli kabisa KH...lakini kwa dunia tuliyo nayo leo hii unaweza usipate Mume kabisa na pia haina maana utakapoamua kunanihii ndiyo utapata 100% assurance ya kuolewa....maana njemba inaweza kuja na sababu mia kidogo baada ya kuonjeshwa ili mradi tu aingie mitini au aendelee kufaidi bila kuwajibika.
na utaolewa vipi bila kutest? hiyo ni two ways! ha haaaaaaaaaaaa
BAK...siamini hata kidogo eti binti amejitunza vizuri na anampenda Mungu, akose mume wa kumuoa...:A S 13:. Wapo wanaume pia wanaopenda mabinti waliotulia, ambao hawaonjeshi kwa kila mtu, kwa hiyo atapata tu!
Ni kweli kabisa KH...lakini kwa dunia tuliyo nayo leo hii unaweza usipate Mume kabisa na pia haina maana utakapoamua kunanihii ndiyo utapata 100% assurance ya kuolewa....maana njemba inaweza kuja na sababu mia kidogo baada ya kuonjeshwa ili mradi tu aingie mitini au aendelee kufaidi bila kuwajibika.