Unyonyaji, unyanyasaji na ukatili unaofanywa na halmashauri zetu kwa watumishi wa umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyonyaji, unyanyasaji na ukatili unaofanywa na halmashauri zetu kwa watumishi wa umma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by janejean, Dec 13, 2011.

 1. j

  janejean Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote watanzania tunapigania nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma. lakini kabla hatujafika huko, kuna malipo yanatolewa na serikali kwa watumishi hao lakini halmashauri hazilipi hizo hela. Badala yake wanakaa vikao vingi kati ya wakurugenzi {DED}na maafisa wake, alafu wanazilipa kiasi kidogo kukiambatana na upendeleo. Na zingine zilizobaki wanazirudisha hazina hili wapate "HATI SAFI" Lakini waheshimiwa hawa wana "STANDING ORDER" ninafikiri watakuwa wanasoma kitabu hicho kama hadithi za kwenye gazeti.

  UKATILI;
  Pesa wanazosafishia wao hati zao mwishoni mwa mwaka wa fedha, ndio zile zilizotolewa na serikali angalau kumpunguzia mtumishi wa umma hasa wa ngazi za chini na za kati ukali wa maisha. wanazirudisha hazina na kuwaacha watumishi hao wakiteseka na wao wanapongezana au wanajipongeza!

  Fedha hizo ni kamavile za kujikimu, usafiri {nauli}, mizigo, matibabu, likizo na wategemezi. Kutokana na mishahara yao kuwa midogo, fedha hizo zingeweza kumsaidia mtumishi wa umma hasa wanaoanza kazi kujiandaa vizuri katika maisha yake ya kazi. Na wale wa siku nyingi, ni zao na ni haki yake itamsaidia katika mambo yake ya kila siku. Anastahili kulipwa.

  UNYANYASAJI;
  Majibu yanayotolewa kutoka kwa wakurugenzi hao na maafisa wao kwa watumishi wapya ni;.
  1. wanaanza kazi sasa wategemezi hao wamewapata wapi? Hawana wategemezi.
  2.mizigo wameipata wapi wakati walikuwa vyuoni? haiwezekani wakawa na mizigo ya kusafirisha.
  3. Halmashauri haina hela.
  4. Tupo kwenye mchakato wa ugawaji wa hizo hela.
  5. Hela zilizokuja ni chache hivyo hatuwezi kuzigawa hadi tupate muongozo. Hadi mwaka unaisha, wanakuja wengine wapya.
  6.majibu ya vitisho ikiwepo kufukuzwa kazi iwapo wataendelea kuwafuatilia.
  7. Wale wa muda mrefu wanajibiwa arudi kazini na shida yake inafanyiwa kazi. lakin ukweli hawajui hata liko kabati gani huko masijala.

  UNYONYAJI;
  Wanaufanya kwa serikali na wananchi kwa kushindwa kusimamia kazi zao kikamilifu. Wanashindwa kudhibiti upotevu mkubwa wa pesa za umma. kwa kufanya yafuatayo;.
  (a) kulipa watumishi wanaoripoti halmashauri, wanalipwa fedha ya kujikimu, hawafanyi kazi na wanaondoka bila kuchukuliwa hatua yoyote na jambo endelevu.
  (b)Kulipa watumishi waliopangiwa vituo au halmashauri zaidi ya moja. Na niwengi sana wa aina hii.
  (c)kuendelea kulipa watumishi ambao wameacha kazi.

  Lakini TANZANIA kuna vyama vya wafanyakazi. Na viongozi wake ni 'brain drain' sijui wanakuwa wapi kutolijua hili?
  Watumishi wapya wanakaribia kutangaziwa ajira. Kazi kwenu wahusika.
   
Loading...