ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,894
- 6,876
Wilaya ya GEITA pamoja na kuwa na rasilimali za madini katika ardhi yao, bado maisha na unyanyasaji kwa wananchi na watumishi wa umma uko juu sana kuliko wilaya nyingine za mkoa wa Mwanza.
Kilichonisukuma leo kuwapa taarifa na kutaka maoni yenu ni juu ya Halimashauri ya wilaya ya Geita kuwa na kiburi na kufanya unyanyasaji wa wazi kwa watumishi wake hasa WALIMU.
Kwa walimu walioanza kazi 2010 October, hawakulipwa pesa yao ya kujikimu kwa mda mrefu mpaka walipotaarifiana na kukusanyika HALIMASHAURI na kufanya fujo, uongozi mwovu uliopo ukawaita POLISI na kuwasambaratisha walimu hao waliokuwa wakidai haki zao ambazo walinyimwa na mazingira ya kuwadhulumu yalikuwa wazi.
Aliyezima dhuluma hiyo ni waziri mkuu alipotangaza kwamba wilaya zote zilisha pewa pesa ya waajiriwa wapya kujikimu na kuwataka wakurugenzi kuwalipa watumishi stahili zao mara moja ambapo WALIMU geita walilipwa pesa zao April 2011 badala ya October/November 2010. Hata hivyo hawakulipwa zote, walidhulumiwa pesa hiyo hadi 120,000/= .
Sasa watumishi wa halimashauri hiyo, wameingizwa na kulazimishwa kuhesabu sensa ya watoto tangu tarehe 26-09-2011 mpaka leo wanahesabu sensa hiyo. Kinachosikitisha, hawalipwi chochote na halimashauri hiyo, waratibu wa elimu wa kata ndio wanaopiga mkwara walimu wao na kuwahimiza kukamilisha zoezi hilo kabla ya kufika kesho ijumaa ya 30.09.2011.
Utata,
1. kwa nini sensa iendeshwe bila bajeti?
2. Kazi ya walimu wawapo kwenye vituo vyao vya kazi ni kuhesabu wa watu wa vijiji wanakofanyia kazi?
3. Je hii sensa ni ya Tanzania nzima au ni maalumu kwa halimashauri ya GEITA na hasa kata ya CHIGUNGA ambapo walimu wa kata hizo wamelazimishwa kuacha kazi yao ya kufundisha na kuwa maafisa wahesabu watu-NGOSWE katika vijiji vyao?
4. Ni haki kwa mfanyakazi kufanya kazi ambayo haimuhusu tena bila kumlipa chochote?
Mwenye majibu ya hili atujuze,
nawasilisha.