Deo Luhamba
New Member
- Oct 26, 2010
- 4
- 0
Kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu unyanyasaji ndani ya ndoa. Taarifa hizi zinaonesha kwamba vitendo vingi vya unyanyasaji vinafanywa na wanaume dhidi ya wanawake. Hili kwa kiwango kikubwa ni kweli.
Kwa bahati mbaya vipi vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na wanawake dhidi ya Wanaume, lakini kwa sababu kadhaa havipewi umuhimu unaostahili. Jamii imemuandaa mwanamume kama mtu anayeweza, asiyeshindwa. Kwa hiyo pale anaposhindwa anapokelewa na dharau kwa hiyo si ajabu hata yeye akashindwa kujitokeza kusema ukweli. Leo, so jambo la ajabu kuona mwanamke akimwambia mumewe kwamba kusomesha watoto n kazi ya mwanamume hata kama wote wawili wana shughuli za kuingiza kipato. Ikitokea mume ameteteleka kipesa, no wazi hawezi kutekeleza majukumu ya awali. Je mwanamke anapoendelea kusimamia hoja yake ni sahihi? Na je, huo siyo unyanyasaji?
Nini mawazo yako mdau?