Umkondo wa Swize
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 282
- 89
[h=3]MTU MMOJA APIGWA NA KUUMIZWA VIBAYA NA POLISI[/h]
Nyuma ya pikipiki ni jana anayeendelea kupigwa na polisi baada ya kuteguliwa mguu na kupasuliwa usoni huku mkono wake ukiwa umechubuka. |
Na Gustav Chahe, Dodoma
Ni nje kidogo na stendi ya daladala ziendazo Chuo cha Pipango na Nanenane, Polisi walipomkamata kijana mmoja ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja mbele yangu na kuanza kumpiga.
Wakati wanaendelea kumpa kichapo, wananchi walitaka kujua kosa la huyo kijana ni nini ndipo alipojitokeza askari mmoja na kusema ni mlevi.
Wakati hayo yakiendelea nikashuhudia kwa macho yangu askati aliyekua amevaa mavazi ya kiraia akiwa na boriti na kuanza kumpiga kijana huyo miguuni, mgongoni hata mikononi na kumpasua usoni na kumtegua mguu.
Hali hiyo ilinisukuma kuchomoa kamera katika mkoba wangu na kuanza kupoga picha kwa kiicho japo watu walikuwa wengi iawa ni shida kupata picha lakini nilijitahidi kupata picha Fulani.
Nikaona haitoshi nikaamua kumsogelea askari mmoja na kunza kumuuliza ni kosa gain kijana amelikosa kiasi cha kuchapwa kama mnyama.
Wakati nikiuliza hivyo askari huyo akwaita wenzake na kusema huyu ni mwandishi anatafuta nini hapa.
Kibao kilinigeukia nikaoneshwa bunduki ndipo nilipofanikiwa kujichanganya na watu nikakimbia na ananchi wasamaria wema wakaamua kunificha.
Zilisikika sauti za wananchi wakisema mlindeni mwandishi huyo ili akafikishe hayo kwa taifa zima ili watu waone unyama wanaotufanyia polisi.
Muda mfupi walitokea askari wa kikosi cha kutuliza ghasia na kufukuza wananchi kwa kuwatishia bunduki jambo lililowasononesha watu kuwa hawana uhuru.
Akionekana mtu hapa tunamuwasha. Ondokeni hapa mara moja hatuwataki hapa. Jitieni na kimbelembele chenu muone. Potea alisema askari.
Wakati hayo yakitendeka ikatokea gari ya polisi na kumtupia yule kijana na kuondoka naye huku akiendelea kupigwa kwenye ndani ya gari wakati anapelekwa kituoni.
Source: Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima