Unyama wa kutisha kisiwa cha Lubodo

Unyama wa kutisha kisiwa cha Lubodo

mgomba101

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
1,822
Reaction score
711
*Askari wamtoboa mvuvi makalio kwa singe, aoza nusu mwili, yuko hoi hospitalini Geita

MVUVI mmoja mkazi wa kijiji cha Mganza Wilaya ya Chato, katika mkoa wa Geita, yuko hoi hospitalini baada ya kushambuliwa kwa kutumia vitako vya bunduki, marungu na kuchomwa singe na misumari matakoni na baadhi ya askari wa hifadhi ya taifa wa kisiwa cha Lubondo, wilayani Geita.

Mvuvi huyo, Benedicto Thomas (31) alikamatwa na askari hao wa kisiwa hicho waliokuwa doria Aprili 18, majira ya usiku na alianza kupatiwa mateso Aprili 19 mwaka huu, siku moja baada ya kukamatwa usawa wa boya za hifadhi hiyo akiwa ameelemewa na upepo wa ziwa.

Kutokana na kipigo hicho, mvuvi huyo ambaye kwa sasa amelazwa wod namba nane katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, ngozi ya mwili wake kuanzia miguuni hadi matakoni imeanza kubanduka.

Mvuvi huyo sasa hawezi kutembea, kukaa wala kuongea kwa ufasaha, kwa sababu ngozi yake imejaa maji kutokana na wadudu waliokuwa wameanza kumshambulia baada ya kucheleweshewa matibabu.

Imeelezwa baada ya kukamatwa Aprili 18 majira ya usiku, alipelekwa moja kwa moja hadi ilipo kambi namba moja ya kisiwa hicho iitwayo Mulaga, ambapo siku iliyofuata alipelekwa kwenye kambi nyingine ya Lugeye alikoanza kupatiwa mateso ya kila aina na askari hao kwa muda wa wiki moja kuanzia Aprili 18-25 alipofikishwa katika kituo cha polisi Wilaya ya Geita kwa hatua zaidi.
 
Askari wanyapori wanaacha kulinda tembo,twiga wetu wanatesa na kuua raia wasio na hatia.
 
Sasa huyo mvuvi au jangili? usiku tena peke yako maeneo ya hifadhi unatafuta nn kama sio kufanya shughuli za ujangili? Hawa ndio wanaua tembo wetu mnawasingizia wazee wa watu.
 
mambo hayo kama ccm na serikali yake wakiyafanyia kazi kwa kuwashunhgulikia wote waliofanya unyama huo,wangekuwa wanarudisha imani ya yatu kwenye chama na serikali. lakini watakachofanya ni kuficha kilichofanyika na kumuandama aliyetoa habari hii. wanashindwa kujua kwamba itawarudi baadae na kuka kwao
 
Sasa huyo mvuvi au jangili? usiku tena peke yako maeneo ya hifadhi unatafuta nn kama sio kufanya shughuli za ujangili? Hawa ndio wanaua tembo wetu mnawasingizia wazee wa watu.
atakuwa alituimwa na katibu mkuu wetu nini atubela.
 
Mbona adhabu aliyopewa huyo jangili ni ndogo sana alitakiwa auwawe hapo hapo ktk eneo la tukio!
 
wewe umeishaua majangili wangapi? Hata kama ni jangili hakuna sheria? Adhabu aliyopewa inaendana na kosa? Hajakutwa na nyara. Utamuhukumuje?
 
Back
Top Bottom