UNYAMA: Mtanzania asimulia unyama waliyofanyiwa Msumbiji

Tumfukuze balozi wa Msumbiji mara moja. hata kama hawataki watanzania basi wawarudishe
 
Watanzania wapo wengi sana (makumi kwa maelfu) Msumbiji wanaingia bila vibali kuchimba madini na kuvuna mbao kupitia daraja la Mtambaswala na kingo za mto Ruvuma. Hakuna haja ya kulialia tuwaelimishe watu wetu wawe na vibali muhimu.
Hilo hakuna mtu analopinga...

Ila kinacholalamikiwa ni njia zinazotumika kuwakamata, vile wanavyopigwa kama wezi, wanawake wanavyobakwa sisi ndio tunalaani.

Tumia akili kabla ya ku-comment.
 
Hivi hiyo picha ndio hali huko Mozambique? Maana niliiona tu imeandikwa man utd akirudishwa nafasi ya sita........
 
Tatizo ni kubwa Mozambique wale jamaa ubinadamu hakuna nashangaa sisi wabongo tunavyojipendekeza kwao,wana roho mbaya sana !
 
Toka Jana nilisema, ningekua Mimi ndo Mwenye Mamlaka, ningemrudisha Nyumbani balozi Mozambique!

Lakini kwa vile sisi Watanzania ni dizaini nyingine! Mkuu mtoa mada vumilia Tu, nothing will change hasa Kama umesikia kauli za Waziri husika!
 
Punda hata umfadhiri vipi hana shukrani nyingine zaidi ya mateke,vijana wetu na watoto wamepoteza maisha kwa ajili ya kuwapigania watu wa msumbiji,wananchi wa msumbiji wamehifadhiwa na kulindwa Tanzania akiwemo Rais wao wa kwanza lakini leo watanzania wanafadhiliwa kwa kupigwa mateke.
 
Hao nao wanaenda hizo nchi kutafuta ninii si bora wabaki nyumbanii jamani
 
Watanzania waishio nchini Msumbiji wapo katika wakati mgumu kutokana na kufukuzwa kwa nguvu
[/QUOTE]Sahihisho: Watanzania waishio nchini Msumbiji KINYUME NA SHERIA wapo katika wakati mgumu kutokana na kufukuzwa kwa nguvu.

Hivi tunapowafanyia Sisi wageni(tena majirani zetu wa Afrika ya Mashariki) kwa kuwafukuza na kuwafungulia mashtaka , kuwafunga na hata kuwalipisha faini kwa kosa la kuishi nchini bila kufuata sheria za uhamiaji huwa ni halali na tunapofanyiwa sisi huwa mwao na haramu? Tuwe wa kweli. Tuhuma za kijinga eti wa wamebaka watu, hivi kwetu hayo hatufanyiani, au tumezoea?
 
Serikali itume ndege kuokoa rasmali watu yetu mapema tutapoteza ndugu zetu wakati huo ikiangalia chanzo cha kufukuzwa na kuchukua hatua stahiki.
Unadha tz ni israel, uingereza au marekani? bongo haina taimu wala upendo na wananchi wake walioko nje, ndio maana hata watuhumiwa wa unga amesema wanyongwe tu.
 
Hili jambo linaonesha kuna mapana ndani yake ambapo, ama waTZ hatupewi taarifa sahihi za kwanini siri-kali haiwi aggressive kwenye jambo kama hilo ilhali ushahidi halali upo au pengine kuna malalamiko ya Wamsumbiji kunyanyasika ndani ya TZ ambayo na wao wanalalamikia nchi kwao bila sisi kusikia.

Zipo kesi za wageni kukamatwa na watu wa uhamiaji, na baada ya kuonesha vibali vyote halali, walipewa kesi ya kukutwa na BANGE na wengine kuambiwa hawaruhusiwi kufanya kazi hapa ilhali wamekamatwa wakiwa kwa mama lishe wanajipatia mlo wa siku. Wanafikishwa mahakamani na kuishia kulipa milioni moja tzs.

Nitoe mfano mdogo: Mji wa Dar kwa sasa askari wa barabarani wamepewa zile mashine za EFD, akikusimamisha na kukuta na kosa basi utakatiwa tiketi yako ukalipe faini. Tatizo ni hili; Nimesimamishwa na huyu askari mwenye mashine, cha kwanza anakwambia, 'naomba leseni yako nikague', unampa, hapo sasa anaizuia na kuanza kutafuta makosa. Lakini hata kama hakuna kosa, ano uwezo wa kukuandikia tiketi kwakuwa tayari anayo namba ya leseni yako. Sasa ukubali kuipokea tiketi au ukatae, mwisho wa siku utakutana na ile PENALTY siku ya ku-renew leseni yako TRA. Sina elimu ni vipi nitaipinga faini hiyo kama kosa nimebambikwa? Zamani ilikuwa unagoma kusaini au unasaini kwenye kutokukubali kosa kisha unaenda mahakamani, leo unafanyaje kupata haki ilhali umeshaandikiwa?

Kwa mfano huo tu ambao umenikuta wiki iliyopita, kama mgeni akifanyiwa hivi na ilhali anajua anatendewa ndivyo sivyo, hawezi kulalamika nchini kwao? Wakiwa wengi wanalalamikia jambo moja, hawatahemkwa kama sisi sasa hivi? Nini kitafuata?

Pia, wengi wanakimbilia kule kwaajili ya kutafuta maisha, shughuli zitajazwo kuwa wengi wanazifuata kule ni pamoja na uchimbaji madini na mama lishe. Hivi ni kweli kuna haja ya kuikimbia nchi yenye kila aina ya madini kwenye ardhi kwenda kuteseka ugenini? Hatuna migodi? Kama issue ni kutotendewa sawa na watawala wetu nyumbani, ugenini ndio utathaminiwa kuliko mzawa?

Tutafute taarifa za kina kabisa ili tujiridhishe pasi na shaka; ni sababu zipi zipelekeazo ndugu zetu wanyanyaswe ilhali wana vibali halali. Kisha tuanzie hapo ili tusijejuta. Kwanini sasa?
 
Inauma sana kusikia au kuona ndgu zako wanaumia,wanateseka,huku hakuna juhudi yeyote
Hawa msumbiji tumewasaidia wenyewe FRELIMO,ukija south africa halikadhrika india ndugu zetu walipigwa wakateswa wakadhallishwa TUPO KIMYA TU.Wakija kwet wanakula bata na kujiachia tu

lazima ifikie kipindi tufanye ambushi kama hzo za kibabe kila mtu arudi kwao tu tusiwe waoga kihvyo kwanza kwetu wamejaa kibao wengi wanakaa kimazabe tu inakera sana aisee.

BALOZI WA TANZANIA MSUMBIJI NI WAKATI WAKO SASA NDUGU ZETU WANAPATA SHIDA HUKO NA WAMESHAWEKEZA HUKO HATA KAMA WENGINE HAWAJAINGIA KIHALALI BASI ITUMIKE NJIA SALAMA CHEZA NAFASI YAKO SASA INGILIA KATI HILO SWALA
 
Najuta kuchangia damu yangu mwaka 1974 ili kuwasaidia waliokuwa ndugu zetu wa Msumbiji katika mapambano yao dhidi ya ukoloni mkongwe wa Ureno. Ama kweli tenda wema wende zako, usingoje shukrani.

jino kwa jino tu hapa tuanze msako wa kuwakamata wa mozambique tulipize kisasi hakuna namna tena
 
Darkness cannot drive out darkness, only light can do that,
Hate cannot drive out hate, only love can do that.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom