Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Watanzania waishio nchini Msumbiji wapo katika wakati mgumu kutokana na kufukuzwa kwa nguvu ikiwemo kunyang'anywa mali zao, kupigwa na wanawake kubakwa. Msikilize Mtanzania huyu aitwaye Wille Katulunga anayeishi mkoa wa Cabo Delgado akielezea kupitia Planet FM ya Morogoro kuhusu sakata hilo
KUHUSU YANAYOTOKEA MSUMBIJI
Ni vema sasa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikachukua hatua dhidi ya mauaji,utesaji,unyanyasaji,ufilisiwaji unaofanywa kwa Watanzania waishio Msumbiji!
Watanzania wananyang'anywa mali zao na askari wa Msumbiji,wanapigwa,wananyanyaswa,wanabakwa na kulawitiwa bila hatia yoyote!
Kuna vizuizi vikubwa vya kibiashara vimewekwa Msumbiji kukandamiza Watanzania ilihali wao wanafanya shughuli zao vizuri Tanzania bila kubugudhiwa
Hakuna ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji,wema ni sisi tu,wao wanatushambulia utadhani sisi ni magaidi!
Ni vema serikali yetu iweke mazingira magumu kwa watu wa Msumbiji ili kila mtu afanye kazi katika eneo lake!
Njia za kidiplomasia zimetumika mara nyingi lakini hazijaleta matunda yoyote!
Msumbiji haina utawala wa sheria inaongozwa ovyo!
Ni vema serikali ikalichukulia hatua kali suala hili!