unyago una umuhimu gani katika mapenzi?

janejean

Member
Dec 8, 2011
89
23
Baadhi ya mikoa hapa Tanzania wanawacheza unyago watoto wao wa kike. Unyago unamsaidia nini mwanamke
katika kutunza familia yake? nasikia watu (wanaume) wakienda, kwa waliopitia elimu hiyo ni ngumu kutoka.
 
Ungesema kwanza huko unyagoni hua wanafunzwa nini ili tusiofahamu tuweze kujibu swali lako.
 
najua tu mabinti wanachezwa unyago, wanafanya nini au wanawaambia nini mie sijui. kama wajuzi wapo, watujuze.
 
Baadhi ya mikoa hapa Tanzania wanawacheza unyago watoto wao wa kike. Unyago unamsaidia nini mwanamke
katika kutunza familia yake? nasikia watu (wanaume) wakienda, kwa waliopitia elimu hiyo ni ngumu kutoka.

Mbona mimi wa kwangu hajapitia huko lakini yuko fiti mno na sina kabisa mpango wa kutoka?
 
wanamme wakipitia huko ni ngumu kutoka?
Wanatoka wapi?
Wanakuwa wameingia wapi?
 
Baadhi ya mikoa hapa Tanzania wanawacheza unyago watoto wao wa kike. Unyago unamsaidia nini mwanamke
katika kutunza familia yake? nasikia watu (wanaume) wakienda, kwa waliopitia elimu hiyo ni ngumu kutoka.

Hapo kwenye nyekundu hao wanaume itakuwa wanapatikana kwenu...........

Hamna cha unyago wala jando ila akili kichwani, chochote kinachokutatiza refer google...........
 
Tuwasubiri hao wenye makabila yanayofanyiwa hiyo seminar...watatujuza zaidi.
 
Ungesema kwanza huko unyagoni hua wanafunzwa nini ili tusiofahamu tuweze kujibu swali lako.
akisema wanachofunzwa huko si ndo atakuwa amejua na umuhimu wake.ivi ulipofundishwa kuoga si ndo uliambiwa umuhimu wa kuoga?
 
Hapo kwenye nyekundu hao wanaume itakuwa wanapatikana kwenu...........

Hamna cha unyago wala jando ila akili kichwani, chochote kinachokutatiza refer google...........

Na kwa vitendo zaidi refer kwenye YouTube....
 
kuna tofauti waliopitia wengi wanajua kukata kiuno,milio ya mahaba,kumjali mume maji ya kuoga,chakula,mavazi
 
kuna tofauti waliopitia wengi wanajua kukata kiuno,milio ya mahaba,kumjali mume maji ya kuoga,chakula,mavazi

Mbona hivyo vitu ni common,bila hata unyago watu wanayaweza....unless kuna mengine ya ndani zaidi ya hayo.
 
Kuna mengi KATIKA UNYAGO lakini kila kabila wana unyago wao,mie wa Tanga nimepitia lakini sijapenda kabisa manake nimekula fimbo mwanzoni lakini nimefaidika na mengi sanaaaaa,kuanzia usafi malezi mpaka heshima na mambo yakikubwa ndio oooooh...
 
Kuna makabila hatukuwa tunapelekwa unyago moja kwa moja, lakini yafundishwayo unyagoni tulifundishwa hatua kwa hatua kulingana na umri unavyokwenda, toka tukiwa visichana vidogo hadi tunakua. Kuosha vyombo, kubeba na kulea wadogo zetu/watoto, kulima, kusenya kuni, kufagia, kudeki, kufua, heshima, kunengua pia ilikuwemo. Ukipata mchumba unawekwa ndani na mashangazi, wanakufundisha yale ya kikubwa. Lakini mafundisho ya msingi unakuwa umejifunza wakati unakua toka unapozaliwa.
 
una faida sana ndo mana wazee wa zamani wamedumu kwenye ndoa coz kati ya mambo wanayofundishwa uko ni heshima, busara na uvumilivu. ila wadada wa siku hizi atuna kabisa hivyo vitu ukizingatia umesoma una elimu na kazi nzuri, basi utaki kuwa chini ya mumeo kwenye maswala ya nyumbani.
 
Baadhi ya mikoa hapa Tanzania wanawacheza unyago watoto wao wa kike. Unyago unamsaidia nini mwanamke
katika kutunza familia yake? nasikia watu (wanaume) wakienda, kwa waliopitia elimu hiyo ni ngumu kutoka.

jiulize kitchen part wanawake huwa wanafundishwa nini? ukishajua hilo basi unyago ni an advanced stage ya hiyo kitchen part inayofanyikaga kwa masaa tu
 
jiulize kitchen part wanawake huwa wanafundishwa nini? ukishajua hilo basi unyago ni an advanced stage ya hiyo kitchen part inayofanyikaga kwa masaa tu

Kitchen party za siku hizi si lolote wala si chochote bibi harusi mtarajiwa wanachoangalia ni kupata vyombo tu vya kuanzia maisha sijaona vitu vya maana wanavyofundishwa!!!!!
 
Kitchen party haiwezi kuwa na maana kwa vile ni kitu cha siku moja tu, unless awe bibi harusi mtarajiwa aliwekwa ndani kwa muda. Mafunzo hayo kama nilivyosema kikwetu hayakuwa ya muda mfupi hivyo. Ukishazaliwa tu vibibi vikishangilia ni "msichana!" unaanza mafunzo hapo hapo kulingana na umri, mafunzo ya mambo mengi sana sana. Hadi unapopata mchumba hata kiuno ni laini kuzungusha kwa vile utakuwa umeanza mazoezi ya kunengua taratibu kadri unavyokua, mnapokwenda kutafuta kuni, mnapokwenda visimani, mnapocheza wenyewe, mausia ya wamama wakubwa, jinsi ya kuketi kama msichana sio kutanua miguu ka dume. Mzungu alipokuja akasema ni ushenzi, vikatupiliwa mbali, matokeo yake ndo hayo, balaa tupu haijulikani nani HE nani SHE ndani ya nyumba. Mafunzo hayo yalikuwa na bado ni muhimu. Yoooteee kumhusu mama kama mwanamke yalifundishwa kulingana na umri wa mtoto wa kike. Ati leo yanafundishwa kwa masaa??? Mwe! Utaelewa nini? Matokeo kiuno kigumu ka milingoti ya reli, hujui hata kupakata watoto, huelewi mume ndio nini, hujui usafi wala heshima wala hofu ya Mungu. We haya weeee!
 
Back
Top Bottom