Habari za wikiendi bana ndugu,hali ya uchumi kwa wakulima wa ufuta imekuwa ngumu mno mwaka huu,ufuta umepatikana lakini bei ni ya chini sana,kwa kawaida zao hili huuzwa kati ya sh 2000-2500,lakini mwaka huu hali ni ngumu sana kwa huku kusini maana huuzwa kwa sh 1500-1600,na kwa kawaida wakulima huuza zao hili na hukimbilia kununua sanlg na ndani ya kijiji ilikuwa huwezi kukosa pikipiki mpya angalau 3.
Kwa bahati mbaya mwaka huu nimetembelea kata ya chikonji iliyopo Lindi mafundi pikipiki wanalalama kukosa kazi maana kipindi hiki cha msimu hakuna watu wanaoleta kazi mpya, ni mimi mkulima wa ufuta toka kusini.