Until then , africa (tanzania) is never independent! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Until then , africa (tanzania) is never independent!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Revolutionary, Apr 20, 2011.

 1. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila leo tunasikia serikali inaboresha mazingira ya wawekezaji wan je, japo serikali hii pia inajitahidi kwa mwendo wa kujikongoja kutimiza matakwa ya msingi (basic), jitihada ambazo haziridhishi bado kufikia mahitaji halisi ya wananchi.

  Ingawa kifungu cha nane cha katiba yetu inayotumika sasa inatoa nguvu na mamlaka yote kwa mwananchi ta Tanzania lakini kimsingi FIRST PRIORITY kwa Serikali yetu ni MWEKEZAJI WA NJE.

  Hii inatokana na msingi huu wa uchumi wa Kibepari (Capitalism) ambao uko centrally controlled na World Bank na IMF pamoja na dhana ya misaada kutoka Nje katika nchi wahisani (Foreign Aid)

  Mfumo huu wa kifedha na kiuchumi umeundwa kimkakati kabisa kuweza kuwafanya mabepari na nchi zao (za Magharibi, zikongozwa na Marekani) kuendela kuendesha (control) uchumi wa dunia kuwa ndio wamiliki wakuu wa mtaji (Capital) njia za uzalishaji (production) na kutufanya sisi nchi za dunia ya tatu kama tu namna za kuwezesha ubepari wao ushamiri,. Hivyo basi wao hututumia sisi kama Source ya Raw Material na Soko la uhakika kwa kwa bidhaa zao. Watu hawa kamwe hawataki kutuwezesha Africa ili tuwe washindani kibiashara ili tuje tuwape competition wao. Kamwe!

  Ni Juhudi zetu binafsi za kimapinduzi (revolutionary) tu na viongozi wetu ndizo zitakazotukomboa.

  Leo hii eti serikali inahaha kutwa kucha kuwaboreshea mazingira wawekezaji, Mfano mzuri katika Kufana hilo katika mkutano huu ulioisha jana Rais Kikwete katangaza kufuta kodi kwa Cement toka nje nchi , ili kuvutia wawekezaji tangu miaka mitatu iliyopita, What a poor thing!

  Tena juzi juzi tu kafuta ushuru wa sukari, eti ili kupunguza ukali wa bei kwa mwananchi, Mkakati dhaifu kabisa. Tena Rais asema hizo ni njia ndogo ndogo tu za kuwavutia wawekezaji, mengi yapo na yatafuata.

  Pia katika hilo anadai wazalishaji wa ndani wameshindwa kukidhi mahitaji ya soko! Wataweza vipi kama wawekezaji hawa wa ndani (tena ambao ni wazawa wachache) hawawezeshwi na kutengenezewa mazingira mazuri kama sera, mikopo ya riba nafuu, soko, kodi n.k? Haya ndio mambo ya kuongoza nchi kwa kutegemea kudra za mwenyezi Mungu!

  Rais anasema hivi.... "President Kikwete asserted that Tanzania's investment policies were very clear, noting that the country would never go back to the era of Ujamaa (socialism) during which private businesses were nationalized.
  "Nationalisation of corporations will never happen again in Tanzania and this is rightly provided for in our laws… we are bound by international covenants and we are ready to face judgement at an international court in case there is an investment dispute," he stressed".

  Tena anaongeza na hivi..... "On cutting down bureaucracy, President Kikwete said Tanzania's socialism background was partly to blame for existing red tape in some quarters of government business. However, he said, the problem is bound to end as new blood finds its way into senior public service positions"

  Sisemi turudi kwenye ujamaa lakini ili kuweza kuwa na maendeleo Tanzania na one day kuweza kuja kuwa super power (offcourse) Huyu rais anaelewa sisi kama taifa tunatakiwa kufanya nini?? Hivi anaelewa anachokiongea huyu JK!

  Hebu someni hii Article ya The Citizen

  JK reassures investors

  Tanzania (na Africa) tunatakiwa tujitengenezee industrial base ya kutosha, ili tuwe wazalishaji na siku moja tuweze KUCOMPETE kwenye WORLD MARKET, sio kuwa wanunuaji, kila siku tunakimbilia KUIMPORT bidhaa mbofu mbofu toka CHINA na VIJIBAJAJ toka India, we are such a SORRY NATION.

  China na baadhi ya nchi za Asia walikaa kimkakati na kimtazamo hadi kufika hapa walopo leo. Hadi sasa Marekani wanakosa usingizi kuogopa kuzidiwa kiuchumi na China ambayo tena bado hajafikia kushindana in full force. Tunajifunza nini toka kwao???

  Enzi hizo walikataa UBEPARI na MISAADA toka nchi za Kibepari. Kwani Siku zote lengo la Misaada (Foreign Aid) na mikopo toka nchi za kibepari inalenga kutuCONTROL kwenye kila kitu, Kuanzia; Idadi ya ajira katika nchi > kwa kua kampuni zinazoongoza kuajiri ni za mabepari toka nje, Hebu taja Benki, Migodi, Taasisi, Makampuni n.k Tanzania ujionee, leo hawa wote wakitangaza kuwa wanafunga makampuni yao patakalika hapa nchini?. Watanzania wangapi watakosa ajira? Ndio maana serikari haina lolote la kusema kwa wawekezaji wan je! Ni kufyata mkia tu, wanaoendesha Uchumi wetu ni wao na Nchi zao. Halafu leo hii tunaendelea kujikaanga na eti kuwatengenezea mazingira mazuri kwa kuwafutia kodi. This is reeeediiiiculuss

  Hizi foreign Aid ndio zinazowafunga midomo viongozi wa Afrika leo they can't say nothing tunavamiwa Afrika, tunaingiliwa, tunapigwa tunagombanishwa tunahukumiwa..........., najua mnaelewa sana hili, "THEY CAN'T BITE THE HANDS THAT FEEDS THEM"


  SERIKALI ZETU AFRIKA ZIKO KWA AJILI YA KUWAFURAHISHA WAWEKEZAJI SIO WALIPA KODI.


  Nina mengi sana katika Hili na wala sitamaliza leo, kwa sasa niishie tu hapa kwa leo.


  TANZANIA TUNATAKA RAIS MWENYE MLENGO WA KUFANYA NCHI YETU IJITEGEMEE KIUCHUMI, MWENYE MIKAKATI NA MITAZAMO YA KUPUNGUZA NA KUFUTA KABISA UTEGEMEZI WA KIFEDHA, MADENI NA MISAADA TOKA NCHI ZA KIBEPARI, ILI KUIWEKA HURU KIUCHUMI TANZANIA
  (NI JUKUMU LA AFRIKA NZIMA)


  UNTIL THEN , AFRICA IS NEVER INDEPENDENT!
   
Loading...