Unlimited Internet is finaly Here!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unlimited Internet is finaly Here!!!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kang, May 5, 2009.

 1. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Zantel imetangaza Unlimited Package at just 90,000 shillings per Months, 6,000 per day or 30,000 per week. Habari zaidi iko Michuzi Blog, ila sijaweza kuelewa kama ni GSM au CDMA.
   
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unaposema at just 90,000/= unalinganisha na nini? Viwango vya huduma ya mtandao Tanzania bado ni rip off, 90,000/= kwa mwezi popote duniani ni rip off, sasa tusitake kutangaza biashara ya Zantel yenye viwango vya kilanguzi kwa lugha za "at just 90,000 shillings." Watanzania wengi ambao mambo yao mazuri huwa wanasahau hali halisi ya wengi, completely out of touch. 90,000/= kwa mwezi ni rip off. Kang, usiwapambe Zantel.
   
 3. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Mbona wale Benson Communication pale oposite na Ubalozi wa Ufaransa wanatoa Unlimited connection ya internet for 60,000/= per month, 180,000/= for three months. I have used few months a go is very good speedwise.
   
 4. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Benson ukitaka nikupe hata BURE njoo uchukue. Wahindi wale wahuni sana. Hiyo 180,000/= wizi mtupu. Kale ka simu wanakupa kakipata moto tu basi umeliwa, kanaanza kuji-restart kila mara, kama ulikuwa in middle of something unalia tu.

  Nimetumia huduma yao hiyo for 6+ months na nimepiga chini, hawana contract ya kueleweka.

  Zantel kwanini wasitangaze hapa JF? Kuna walakini katika wanachotangaza au wanachagua pa kutangaza? Hebu tupe hiyo package tuichambue.

  Nothing UNLIMITED kwa Bongo, they must be kidding around I can bet
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hivi mbona bado 180,000 ni pesa nyingi sana kwa Mtz wa kawaida?

  Sii sasa wanatandaza wire? Je nilidhani gharama zingezidi kuwa za chini!
   
 6. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wire bado ujarushwa ndo maana watu wanataka kulizana za mwisho mwisho..once the seacom cable is active ndo tutajua the true price of getting internet in bongo!! Nimependa seacom walivyo kuwa sio wabaguzi ISP's wote wamekaribishwa kununua bandwith ..tutaona true competition .
   
 7. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Haya matangazo mengine ukiyaangalia tu unajua kuna gimmick tupu.

  60,000 X 3 = 180, 000. Sasa mtu akikutangazia package mbili, moja ni 60,000/= kwa mwezi, na nyingine ni 180,000/= kwa miezi mitatu, tofauti ya hizo package mbili ni nini? Gimmick za uongo na kweli hizi. Tunalalamika tunalanguliwa kumbe tunaingia wenyewe mikenge kama hiyo...aaaah
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hii ni Wireless 3G service, so ukiifananisha na mitandao mengine ya nchi za nje itakua sio sawa.
  3g ya Zain bongo ni 2GB per months for 100,000 ambayo ndo natumia.
  So hii 90,000 ni ndogo sana ukifananisha. Cable ikija nadhani mambo yatakua mazuri zaidi.
   
 9. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani Internet Service Provider anauza simu au anauza huduma ya kuufikia mtandao? Huna simu au PC yako?

  Mara simu ndo mbovu, mara hawana contract ya kueleweka, shagalabagala, contract hukuielewa lakini uliisaini anyway? Hapo sidhani kama kosa ni la "Wahindi wale" zaidi ya wazawa wale, kina Pimbi.
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kulikua na ukosefu wa zile modem zao wakati nataka kununua, plus wakadai nikununua Modem kwa mtu mpaka waicheki kama ina madeni, sasa nikashindwa kuelewa hayo madeni yananihusu vipi?, labda wamerekebisha mambo now.

  Kama hii Zantel ni GSM itakua safi sana maana tunaweza tukatumia simu zetu hakuna haja ya kununua kale kamodem kao.
   
 11. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Benson hauwezi kutumia simu yako lazima ununue yao, hilo ndo tatizo.
   
Loading...