Unguja: Moto wateketeza nyumba, watano wanusurika

Unguja: Moto wateketeza nyumba, watano wanusurika

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,309
Watu watano wamenusurika kifo baada ya nyumba wanayoishi kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 25,2018 eneo la Mitondooni wilayani Magharibi B, Unguja.

Chanzo cha moto kinaelezwa kuwa ni hitilafu ya umeme ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amesema moto ulitokea saa moja usiku.

Mayasa Makame aliyenusurika katika janga hilo amesema moto ulizuka ghafla walipokuwa wakipika.

Amesema wamepoteza kila kitu kilichokuwamo ndani.

Kuhusu chanzo cha moto imeelezwa huenda ikawa ni hitilafu ya umeme kwenye jokofu.

Mayasa ameiomba Serikali na wananchi kwa jumla kuwasaidia kwa kuwa hawana chochote kwa sasa.


Mpekuzi
 
Nimesikia kwamba nyumba nzima walikuwa wanakaa wanawake watupu,,,,, ndio maana wakishindwa kuokoa hata vitu vichache kwa kuwa wanawake ni waoga sana.
 
Back
Top Bottom