Ungetamani Rais afanye nini?

Ahuishe ile rasimu ya katiba ya Warioba na mambo mengine yatakaa sawa kwa mujibu wa hiyo katiba.

Japo ninajua hata hilo hatalifanya kwa sababu katiba aliita ni 'kijitabu' na yeye kujiita CK (Chura Kiziwi)..hata umshauri vipi hatasikia.
 
Samia arudi Kizimkazi atuachie Tanganyika yetu, ameshaharibu sana sasa yatosha.
 
Aunde tume ya uchaguzi inayoaminiwa na vyama vyote. Kusiwe na mteule wa rais anayehusika katika mambo ya uchaguzi kwa namna yoyote.

Tume iwe na watumishi wake watakaokuwa huru kutangaza matokeo ya uchaguzi na sio wakurugenzi au watendaji.

Nb. Hata akileta maendeleo makubwa kiasi gani ,lakini bila kuwa na uhuru wa kisiasa kwangu hafai kuwa kiongozi.
 
Angeachia ngazi Urais haumtoshi watu hawana imani naye
 
Ajiuzuru, aanzishe mchakato wa maboresho ya katiba mara moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…